Pre GE2025 Rais Samia: Kuna Mbwa Mpumbavu anabwekea maendeleo yetu
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Rais Samia alitoa kauli hiyo wakati alipo muomba Naibu waziri wa Sanaa na michezo maarufu kama Mwana Fa kuimba mashairi wakati akitaka kuanza kuongea na wana Zanzibar katika uzinduzi wa Suluhu Sports Club.

katika sehemu aliyoimba Mwana FA ambaye ni Naibu Waziri wa Sanaa na Michezo alisema "mbwa mpumbavu ndiyo anaweza bwekea ndege". Baada ya hapo Rais Samia ndiyo akaongezea kusema Kuna Mbwa Mpumbavu anabwekea maendeleo yetu.
Hahaha.....wacha tu nicheke.
 
Wapi nimesema watu wote.
Nimesema watu wote wenye akili tunajua Mbwa Mpumbavu ni nani

Kama humjui basi wewe siyo sehemu ya watu ninaowaongelea. Mbona simple tu. 🤣 🤣 🤣 🤣
Hii ni fasihi ya Kiswahili huwezi ukawa na jibu umoja usilazimishe kuwa wewe ndiye mwenye uelewa sahihi, mbona rahisi tu, umeelewa hivyo uko sahihi na mimi nimelelewa hivi niko sahihi hunanhaki ya kutaka nielewe kama ulivyoelewa wewe wapi shida hadi unatoa mapovu?
 
Rais Samia alitoa kauli hiyo wakati alipo muomba Naibu waziri wa Sanaa na michezo maarufu kama Mwana Fa kuimba mashairi wakati akitaka kuanza kuongea na wana Zanzibar katika uzinduzi wa Suluhu Sports Club.

katika sehemu aliyoimba Mwana FA ambaye ni Naibu Waziri wa Sanaa na Michezo alisema "mbwa mpumbavu ndiyo anaweza bwekea ndege". Baada ya hapo Rais Samia ndiyo akaongezea kusema Kuna Mbwa Mpumbavu anabwekea maendeleo yetu.
Watanganyika wamefikia kuitwa mbwa wapumbavu?! Kweli?!!!
 
Hii ni fasihi ya Kiswahili huwezi ukawa na jibu umoja usilazimishe kuwa wewe ndiye mwenye uelewa sahihi, mbona rahisi tu, umeelewa hivyo uko sahihi na mimi nimelelewa hivi niko sahihi hunanhaki ya kutaka nielewe kama ulivyoelewa wewe wapi shida hadi unatoa mapovu?
Nimekuuliza swali. Je wewe ni mmoja wa watu ninaowaongelea?
Nimesema Watu wote wenye akili wanajua Mbwa mpumbavu ni nani.

Fumbo mfumbie mjinga mwelevu ataling'amua. Je, wewe ni kati ya watu ninaowaongelea?
 
Back
Top Bottom