Sijui atakuwa ametumia kigezo gani kuwaita wenzake ni mbwa wapumbavu, labda yawezekana yeye ni nguruwe mwerevu. Na nguruwe mwerevu ni yule anayewala watoto wake , huku waliosalia wakizidi kumsogelea mama yao wakiamini anawapenda, wakati ni suala la muda tu na wao wafikiwe.
Ulimwengu utakuwa ni mahali pazuri kwa kila mmoja, siku ambayo wagombea hao watakapotambua kuwa wote ni wana wa Mungu, na aliyewaumba akawapa fikra na upeo tofauti, alikuwa na sababu za msingi kuliko wao wanaopenda wanadamu wote wakubaliane katika yote, kwenye mema na mabaya.