Rais Samia, kuna mtu mmoja tu hapa Tanzania anaweza kukusaidia kuuvuka huu mtihani wa DP World na TEC - muite, ongea nae, msikilize, ufanye atachosema

Tunataka mkataba utekelezwe tu hayo mengine hayatuhusu
 

Hakuna mtu mwenye uwezo wa kutatua biashara za kihuni na kitapeli, mhusika inabisi aache utapeli, au atafute msela wake aende ongea na wahusika wamwonee aibu wamsikilize.
 
Nafikiri ame base kwenye hayo aliyokwisha kuyafanya na aliyoyataja. Japo siyo kwamba amemaanisha hakuna wengine Bali ndiye mtu potential anayemfahamu.
 
Kivipi tufafanulie.
akiwa waziri wa mawasiliano TTCL ilibinafusishwa Kwa kampuni iliyokuwa inamiliki Airtel kabla haijauzwa, mkataba ule ulikuwa hauna maslahi kwa Taifa lakini yeye kama waziri mwenye dhamana alikuwa anawakingia kifua.
Baadae iligundulika hiyo kampuni iligharamikia scholarship ya binti yake, Kwa kifupi kulikuwa na mgongano wa maslahi.
 
Tuliambiwa alifisadi TTCL kwa kutumia mkataba mbovu na Celtel, je hii ni kweli?
 
Kuna mambo mengi sana amefanya ambayo watu walimsifia kwa busara na hekima zake, ndani na nje ya Tanzania, siwezi kuyaweka yote hapa.
Kuna mwaka yule Profesori wa Buguruni alikuwa mshauri wa Rais mmoja katika mambo ya kiuchumi nchi jirani, watu wakasema kama ndivyo basi ni bora huyo Profesori akapewa hiyo nchi aijenge kiuchumi yeye mwenyewe kuokoa muda, Presidaa wa nchi husika akashtuka
 
Halafu nawashangaa sana maCCM kwa kumtenga na kumbagaza Prof Mwandosya kumbe ni mtu makini hivi. Kazi kwako Bi Mkubwa. Ama uamue kutofuata ushauri uangamie au usikilize ushauri upone. It is up to you.
 
Lazima angestuka kwani huwezi jua akina Okelo wengine watatokea wapi.
 
Kuna watu wa maana na wenye heshima na uwezo kama Prof Mark Mwandosya.
Yeye huwa hamung'unyi maneno na si mnafiki.
Aliwahi kusema hadharani kuwa kitendo cha kumshitaki Sugu na kumuweka ndani si cha kibinadamu, na alienda kumwona jela.
Mwendazake alichukia na kumtimua bodi zote alizokuwemo.
Baadaye ikaonekana kweli Sugu alibambikwa kesi.
Kwa kiingereza, wanasema he is a man of intergrity.
 
Naamini mawazo Yako ni mazuri, Rais ni taasisi kubwa hivyo anaweza akaiona post Yako then akiona inamfaa anaweza kuichukua.Tupo hapa duniani kusaidiana,nchii hii inahitaji msaada na maombi pia Kwa sababu tunapita katika kipindi chenye changamoto kubwa Hasa kwenye issue ya DP WORLD na bandari zetu.
 
Unatafuta ugali tu. Kwani umeambiwa wamekosa busara au mkataba unadhani uliandikwa kwa bahati mbaya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…