Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Urusi na Marekani japo walikuwa mahasimu waliungana na kumuangusha Hitler kwenye vita ya dunia. Ni jambo ambalo Hitler mwenyewe hakua analifikiria.
Hii inatupa somo kuwa, watu ambao ni mahasimu wakubwa ambao hata hukufikiria wataungana, wanaweza kuungana ikiwa malengo yao yanafanana.
SG na Chadema malengo yao wote ni kumuondoa Samia madarakani 2025. Watu hawa pia siasa zao zinafanana, utawasikia wote wakilaumu serikali kwa bei za vyakula kupanda na kutaka ifunge mipaka.
Utawasikia wote wakipinga tozo, kodi na mikopo. Utawasikia wote wakipinga machinga kuondolewa barabarani. Sukuma Gang hivi sasa nao wameanza kudai Katiba mpya baada ya kundi lao kuondolewa madarakani
Samia anatakiwa kucheza karata zake kijasusi, anatakiwa kuhakikisha watu hawa wanaendelea kuchukiana na kupingana. Ama wakiungana wanaweza kuitoa ama kuijeruhi vibaya CCM.