Rais Samia kuwa mgeni rasmi kongamano la BAWACHA siku ya wanawake duniani

Rais Samia kuwa mgeni rasmi kongamano la BAWACHA siku ya wanawake duniani

Sukuma gang mnatia sana huruma kudadeeki
Mkuu 'Mmawia', ukitaka tuelewane katika mambo haya, achana na ujinga huu.

Wewe siku zote, siku nyingi sana humu tumejibishana mara nyingi tu vizuri, na ninazo 'likes' zako nyingi sana ulizowahi kunipa.
Halafu leo unageuka na kunipa lebo ua u-'gang'.

Hii haionyeshi tabia mbovu kabisa uliyonayo wewe mwenyewe, na kwa bahati mbaya, wengi wenu mlioko huko ndani ya CHADEMA, kwamba ni wachumia tumbo tu, ambao siyo tofauti kabisa na hao tunaowasema hapa kuwa wapo ndani ya CCM?

Hii ndiyo sura halisi ya CHADEMA na sasa imejitokeza bayana, kila mtu ajionee mwenyewe.
 
Ni uthibitisho kuwa Viongozi wakuu wa Chadema wamelamba asali.

Rais anayeendelea kuwakumbatia wanawake 19 waliofoji nyaraka za chama, wakafukuzwa uanachama na bado anawakingia kifua ili wabaki bungeni waendeelee kula kodi za wananchi utamwalikaje kwenye kikao cha wanawake watiifu kwa chama?

Mbowe anaigeuza Chadema kuwa tawi la CCM.

Na ni ushahidi kuwa akina Mbowe wanampigia kampeni ya urais Samia in exchange ya viti vichache vya ubunge watakavyogawana akina Mbowe na genge lake.
Wewe ulipita bila kupingwa
 
Nimependa kusikia kwamba Watanzania sasa wanaishi kama ndugu na wanashirikiana.

Watanzania miaka yote tumekaa pamoja kwenye familia, kwenye mahusiano, kanisani, kazini na maeneo mbalimbali yanayotuleta pamoja.

Lakini Watanzania hao hao tumekuwa maadui kwenye ulingo wa siasa. Maana yake tunaelewana na kusema NI ndugu kwenye kila kitu Ila inapokuja kwenye siasa tunafanya unafiki kwamba Sisi siyo ndugu.

Naamini makubaliano ya Mbowe na Mhe. Rais kuhusu Rais kuwa mgeni rasmi siku ya wanawake yamepokelewa Kwa mtizamo tofauti. Nini maoni yako?

Maoni yangu Mimi NI haya;

Mhe. Rais kuwa mgeni Rasmi kwenye mkutano wa chadema nikutuma salamu Kwa vyombo vya dola kwamba Tanzania sasa NI moja. Nikutuma salam Kwa viongozi Aina ya Muro, Makonda, Mnyeti, Gambo, Nape, Mwigulu, Ndugai, Mkumbo, Molel, Tulia, Bashiru, Kabudi, Lukuvi, nk kwamba siyo lazima uwe na roho ya kikatili Ndipo ukubalike au uongoze....Duniani tunapita ccm au CDM tutaviacha......Sisi NI ndugu.
Hivi Mkumbo, Kabudi na Lukuvi waliwahi kufanya nini ukilinganisha na orodha ya watu kama kina Makonda na Sabaya???

Ila kuna wakati binadamu anamchukia binadamu mwenziye bila sababu ya msingi. Nashangaa sana kuona orodha ya wenzetu hawa wanalinganishwa na watu kama kina Makonda. Kuna wakati tuache unafiiki bhana

Ni ushamba!
 
Ni watu wenye mawazo mgando tu wanaoweza kupinga ushirikiano na mshikamano kati ya wanasiasa na vyama vya kisiasa. Mara nyingi tumeona wanasiasa wa vyama wakialikana kwenye matukio ya vyama na haijawahi kuwa dhambi. Sasa inakuwaje hili tukio la mama Samia kuhudhuria mkutano wa BAWACHA uchukuliwe kwa hisia hasi?

Watanzania punguzeni chuki. Muombe Mungu awaepushe na dhambi ya chuki. Sisi sote ni ndugu hatupaswi kuchukiana kama ilivyokuwa ktk utawala wa Magufuli.

Lengo la Magufuli lilikuwa kuigawa nchi kwa misingi ya kisiasa na kikabila lakini Rais Samia anataka kutuunganisha pamoja. Asiyependa umoja miongoni mwa watanzania, ahamie Burundi.
 
Missile, do not speculate untill you spectate. Sikudhanii kama unaweza kuwa na such reasoning
Kubali chadema imekufa kabisa hakuna Chama pale hata mtetee vipi
 
Ni watu wenye mawazo mgando tu wanaoweza kupinga ushirikiano na mshikamano kati ya wanasiasa na vyama vya kisiasa. Mara nyingi tumeona wanasiasa wa vyama wakialikana kwenye matukio ya vyama na haijawahi kuwa dhambi. Sasa inakuwaje hili tukio la mama Samia kuhudhuria mkutano wa BAWACHA uchukuliwe kwa hisia hasi?

Watanzania punguzeni chuki. Muombe Mungu awaepushe na dhambi ya chuki. Sisi sote ni ndugu hatupaswi kuchukiana kama ilivyokuwa ktk utawala wa Magufuli.

Lengo la Magufuli lilikuwa kuigawa nchi kwa misingi ya kisiasa na kikabila lakini Rais Samia anataka kutuunganisha pamoja. Asiyependa umoja miongoni mwa watanzania, ahamie Burundi.
Sukuma gang wote hawafurahii huu muelekeo mzuri wa mshikamano wa nchi yetu.

Hata baadhi ya wabunge wa ccm hawataki kabisa hii hatua tuliyofikia
 
Hivi Mkumbo, Kabudi na Lukuvi waliwahi kufanya nini ukilinganisha na orodha ya watu kama kina Makonda na Sabaya???

Ila kuna wakati binadamu anamchukia binadamu mwenziye bila sababu ya msingi. Nashangaa sana kuona orodha ya wenzetu hawa wanalinganishwa na watu kama kina Makonda. Kuna wakati tuache unafiiki bhana

Ni ushamba!
Mkumbo ni mnafiki na anaongoza kuwachukia wapinzani.

Mkumbo kuchukia hatua hii ya muafaka na maridhiano ni sawa maana hana uhakika na kurudi jimboni alilopewa na Jiwe.
 
Eti Eeeh! Bhwanaaah?

"... Kuirudisha amani na upendo kwa waTanzania..."!

Haya mambo mazuri hayawezi kurudi bila CHADEMA kujisalimisha kwa Samia na tawi lake la CCM?

Kwa hiyo ajenda pekee iliyokuwa ikipiganiwa na CHADEMA miaka yote hii ni hayo mawili tu basi?
Mkuu Kalamu wewe unepaniki huko Ccm leo watu watalala na viatu.

Tusubiri Rais aweke mambo sawa kisheria na kikatiba.
 
Sukuma gang wote hawafurahii huu muelekeo mzuri wa mshikamano wa nchi yetu.

Hata baadhi ya wabunge wa ccm hawataki kabisa hii hatua tuliyofikia
Dr Slaa amesema leo kama haya anayofanya Rais hawakukubaliama kwenye Kamati Kuu ya CCM basi leo kuna watu watalala na viatu na wengine watalazwa hospitalini.
 
Back
Top Bottom