Rais Samia kwa hili la kuruhusu Mashirika ya Umma kuajiri nakupa pongezi sana

Dola ya Tanzania isiruhusu hili jambo. Huyu mama aache haraka haraka. Haraka haraka haina baraka. Atapotea. Apewe ile ripoti ilipropose kuanzishwa kwa utaratibu wa ajira unaotumika sasa.
sawa tumesikia
 
imekua na urasimu wa kishenzi.imeanza kuingilia hata taratibu za watumishi kwenye mashirika na kuwaita watumishi wa umma hadi maslahi yao.
tena ndumbaro wamle tu kichwa
 
Dola ya Tanzania isiruhusu hili jambo. Huyu mama aache haraka haraka. Haraka haraka haina baraka. Atapotea. Apewe ile ripoti ilipropose kuanzishwa kwa utaratibu wa ajira unaotumika sasa.
Syo kitu kigeni.
wakati wa mkapa alibadilisha sheriia kuruhusu mashirika kuajiri na kujilipa kwa jinsi wanavyozalisha.
sheitwan alipoingia kaanza ujinga bila hata,sheria kubadilishwa.
anachotaka mama ni ile sheria kufatwa
 
Kuna watu wanapayuka ila hawajui wanacho kiongea,ila Utumishi wanafanya kazi kubwa sana, nina wanangu wametoka life la chini kabisa tena wengine walikata tamaa leo wapo kwenye taasisi kubwa sababu ya Utumishi.Hii siku ya leo nina mwanangu mwengine katoboa TRA sababu ya Utumishi nae katokea life bovu kinyama.

Hii kuhusu Tasisi au shirika liajiri wenyewe wataja wakina KAMLETE.

Daaah bi mkubwa hapa kachemka.
 
Kumbe.
 
Barua yangu imepotea hapo Utumishi zaidi ya mara nne...inaonekana imepokelewa ila hauonekani iko wapi?
 
Watoto wa walalahoi ndio msahau kupata kazi katika hizo taasisi. Utumishi sifahamu makando kando yao mengine ila kwenye suala la ajira wako fair sana. Ni kupitia mfumo wao wa ajira nimeona vijana waliotokea familia za kawaida (akina sie watoto wa mama ntilie) wakipata kazi mashirika/vitengo nyeti Serikalini.

Rais Mama Samia Usijaribu kuua mende kwa nyundo, fikiria tena kuhusu kauli/maamuzi yako, elewa tatizo lilipo kisha tatua ila sio kwa kuondoa mfumo rasmi uliopo. Kati ya Mashirika yaliyoongoza kwa vi Memo kabla ya mfumo wa ajira kuwepo ilikua ni TTCL na hapo TRA, ofisi nzima ilikua inaongozwa na familia.
 
Ila mmemlisha maneno amesema kwa zile za muda mfupi ambazo pesa hazitoki hazina wanazitoa mashirika yenyewe utumishi iwape go ahead mashirika yaendelee lakini zile permanent hajazizungumzia.

Ila utumishi nao waangalie kama ni kanuni ndizo zinachelewesha basi wazirekebishe.
 
Secretariat ya ajira nao wanachukua muda mrefu sana mpaka mtu apate ajira.

Huko kwenye taasisi nako ni majipu tu.

Kujuana kwingi.

Kifupi hakuna mahali kuna unafuu.

usemalo ni Kweli!
Taasisi wanapenda Hire&Fire wawe na Huo Uwezo!
Yaani Wakikuajiri Ukizingua Tuu au Ikitokea hitilafu Flani Kesho asubuhi hauna Chako[emoji12]
 
Maagizo yametoka kishkaji sana, hizo taasisi mfano TANESCO ilivyo na Miungu watu. Wao wanawazia kupunguza watu kisha kazi wabinafsishe Mh Raisi anataka waajiriwe watu kwa projects husika ajira za mikataba au za kudumu ikibidi, Watampuuzia bila shaka kwakuwa hapawezi pale , yetu macho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…