Pre GE2025 Rais Samia kwa Mabalozi: Hatupo hapa kuelekezwa nini cha kufanya kwenye nchi yetu

Pre GE2025 Rais Samia kwa Mabalozi: Hatupo hapa kuelekezwa nini cha kufanya kwenye nchi yetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
nchi amedokeza kuwa hayuko tayari kuelekezwa nini cha kufanya.

Balozi namba moja rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo anatekeleza sera yake ya mahusiano ya kimataifa, kwa kukataa kuna tatizo Tanzania na kuwa hahitaji msaada wa kiufundi na kiuzoefu kupambana na genge la kihalifu liloishinda jeshi la polisi la Tanzania pia Idara ya Usalama wa Taifa TISS.

Kwa tamko hili la balozi namba moja ambaye ni Rais amiri jeshi mkuu na mfariji , wahuni hawa wanaoitwa watu wasiojulikana wakiamua kufanya matukio makubwa zaidi kwa kuwa sasa Tanzania imejitutumua haitaki kushirikiana na vyombo vingine mahiri vya nchi zingine kitachotokea ina maana lawama zipo katika mabega ya rais.

Hawa wahuni wasiojulikana kiaina watakuwa hofu ya kushughulikiwa kimataifa haipo na kwa vyombo vya ndani vinawaogopa ni kwamba kuna mawili yataibuka.

Vitendo hivi vya kuteka, kupoteza na kuua vitakoma kwa sababu zisizojulikana au vitashamiri ikiwa kweli serikali haihusiki kabisa na wahuni hawa.

Muda utatupa majibu ya scenario (mazingira) hizi mbili matukio kuisha kabisa au matukio kupamba moto mkali zaidi. Kwa akili na ufahamu wa kawaida jibu litapatikana upande gani unahusika dola (state) au wahuni wanaojitegemea bila nguvu ya dola waliopachikwa jina genge la watu wasiojulikana.

View: https://m.youtube.com/watch?v=0igGRu63Hgk
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hivi karibuni amejibu kuhusu matamko yaliyotolewa na balozi mbalimbali hapa nchini Tanzania kufuatia kifo cha Kada wa CHADEMA, Ali Kibao.

Mara baada ya Ali Kibao kupatikana akiwa amefariki huko Ununio, Dar Es Salaam balozi za nchi mbalimbali kama Marekani, Ufaransa na Umoja Wa Ulaya yaani EU walijitokeza kukemea kitendo hicho na kuitaka serikali ya Tanzania kufanya uchunguzi wa haraka.

Soma Pia: Rais Samia: Mauaji ya Kibao hayakubaliki. Uchunguzi umeanzishwa

Leo akiwa anatoa hotuba kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi La Polisi, mkuu huyo wa nchi amedokeza kuwa hayuko tayari kuelekezwa nini cha kufanya na kwamba Tanzania ina katiba na miongozo yake na kwamba sisi tunajua nini cha kufanya.

View attachment 3098778

Source: Mwananchi
Hivi hapo kati ya askari wa jw na tis nani anaonekana kaiva japo kidogo
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hivi karibuni amejibu kuhusu matamko yaliyotolewa na balozi mbalimbali hapa nchini Tanzania kufuatia kifo cha Kada wa CHADEMA, Ali Kibao.

Mara baada ya Ali Kibao kupatikana akiwa amefariki huko Ununio, Dar Es Salaam balozi za nchi mbalimbali kama Marekani, Ufaransa na Umoja Wa Ulaya yaani EU walijitokeza kukemea kitendo hicho na kuitaka serikali ya Tanzania kufanya uchunguzi wa haraka.

Leo akiwa anatoa hotuba kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi La Polisi, mkuu huyo wa nchi amedokeza kuwa hayuko tayari kuelekezwa nini cha kufanya.

Source: Mwananchi
Yes hicho ndicho,
Lazima waheshimu mila, utamaduni , desturi, katiba na sheria za nchi yetu huru,
vinginevyo wasipobadilika mabalozi hao wote watarudishwa makwao bila mbambambba yoyote 🐒
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hivi karibuni amejibu kuhusu matamko yaliyotolewa na balozi mbalimbali hapa nchini Tanzania kufuatia kifo cha Kada wa CHADEMA, Ali Kibao.

Mara baada ya Ali Kibao kupatikana akiwa amefariki huko Ununio, Dar Es Salaam balozi za nchi mbalimbali kama Marekani, Ufaransa na Umoja Wa Ulaya yaani EU walijitokeza kukemea kitendo hicho na kuitaka serikali ya Tanzania kufanya uchunguzi wa haraka.

Leo akiwa anatoa hotuba kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi La Polisi, mkuu huyo wa nchi amedokeza kuwa hayuko tayari kuelekezwa nini cha kufanya.

Source: Mwananchi
Mna Katiba, sheria , miongozo, mila na desturi ambavyo hamviheshimu wala kuvifuata. Hamjuincha kufanya ndiyo maana mpaka sasa hamjawahi kufanya kitu matokeo yake mnazalisha watafuta hifadhi huku na ninyi mkiwa ni vichwani maboga pamoja na rasilimali lakini kila kukicha viguu na njia kwenda kuombomba kwao.
Nina uhakika baada ya kauli hiyo utafanya safari nyingine ndefu kwenda kusafisha hali ya hewa na ukirudi tu rasilimali nyingine zinaondoka
 
kama rais amesema vile, mjue kuwa haya yoooooooooooooooote yana baraka zake. Anajua fika nini kinaendelea na anaagiza yeye
Kwani kuna mtu hajui hilo jambo kweli?

Mtu atekwe auawe halafu Polisi wasijue aliyefanya utekaji, eti na Rais naye asijue!

Hizo ni dana dana za mazingaombwe ya kijinga sana kutuona sisi waTz wote blood fuckin!
 
Shujaa Magufuli kama binadamu Wengine alikuwa na madhaifu yake lakini katika kuwashikisha adabu Mabeberu Africa nzima walimpigia salute

Katika hilo Kazi Iendelee

Kwani Wao Wazungu ni nani? 🐼
 
Anamaanisha yeye kama yeye hayupo kuelekezwa ? Nadhani Sheria na Katiba za nchi zinamuelekeza cha kufanya na kama so called waliomuelekeza wamesema afanye nje ya Katiba hapo sawa ila kama ni mambo yaliyomo kwenye Katiba inapaswa ajishangae kwanini hayafuatwi...

In short statement kama hizi wakati kama huu ambazo zinaweza kuwa misquoted hazifai...
 
Shujaa Magufuli kama binadamu Wengine alikuwa na madhaifu yake lakini katika kuwashikisha adabu Mabeberu Africa nzima walimpigia salute

Katika hilo Kazi Iendelee

Kwani Wao Wazungu ni nani? 🐼
Huna akili, muuaji mbona anapepea kila leo kwenda kwa mabeberu na mabakuli
 
Back
Top Bottom