nchi amedokeza kuwa hayuko tayari kuelekezwa nini cha kufanya.
Balozi namba moja rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo anatekeleza sera yake ya mahusiano ya kimataifa, kwa kukataa kuna tatizo Tanzania na kuwa hahitaji msaada wa kiufundi na kiuzoefu kupambana na genge la kihalifu liloishinda jeshi la polisi la Tanzania pia Idara ya Usalama wa Taifa TISS.
Kwa tamko hili la balozi namba moja ambaye ni Rais amiri jeshi mkuu na mfariji , wahuni hawa wanaoitwa watu wasiojulikana wakiamua kufanya matukio makubwa zaidi kwa kuwa sasa Tanzania imejitutumua haitaki kushirikiana na vyombo vingine mahiri vya nchi zingine kitachotokea ina maana lawama zipo katika mabega ya rais.
Hawa wahuni wasiojulikana kiaina watakuwa hofu ya kushughulikiwa kimataifa haipo na kwa vyombo vya ndani vinawaogopa ni kwamba kuna mawili yataibuka.
Vitendo hivi vya kuteka, kupoteza na kuua vitakoma kwa sababu zisizojulikana au vitashamiri ikiwa kweli serikali haihusiki kabisa na wahuni hawa.
Muda utatupa majibu ya scenario (mazingira) hizi mbili matukio kuisha kabisa au matukio kupamba moto mkali zaidi. Kwa akili na ufahamu wa kawaida jibu litapatikana upande gani unahusika dola (state) au wahuni wanaojitegemea bila nguvu ya dola waliopachikwa jina genge la watu wasiojulikana.
View: https://m.youtube.com/watch?v=0igGRu63Hgk