Pre GE2025 Rais Samia kwa Mabalozi: Hatupo hapa kuelekezwa nini cha kufanya kwenye nchi yetu

Pre GE2025 Rais Samia kwa Mabalozi: Hatupo hapa kuelekezwa nini cha kufanya kwenye nchi yetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Yes hicho ndicho,
Lazima waheshimu mila, utamaduni , desturi, katiba na sheria za nchi yetu huru,
vinginevyo wasipobadilika mabalozi hao wote watarudishwa makwao bila mbambambba yoyote 🐒
Huo ujeuri hana. Ajaribu kuwafukuza hao mabalozi, kama ana jeuri hiyo. Wewe Serikali yako iteke na kuua watu halafu useme unajua la kufanya!!

Ameota mapembe kiasi cha kuona ana mamlaka ya kuamua nani aishi, na nani afe muda anaoutaka yeye!!
 
Haha,
Siyo makasiriko dogo, ni angalizo tu
angalizo lielekeze kwa mabalozi wasio zingatia mila,desturi na utamaduni wa host country,

vinginevyo hawatavumiliwa hata kidogo wasipozingatia sheria za kimataifa na ustaarabu wa kidiplomasia. watarejeshwa makwao mara moja 🐒
 
The Commander-In-Chief, and the President of the United Republic of Tanzania has spoken loud and clear!
 
Inaonekana hata historia ya ukombozi wa kusoni mwa Afrika hakuisoma. Mauaji na utekaji hayana tofauti na waliyofanyiwa wananchi wa Afrika ya kusini na makaburu. Lazima uovu huo upingwe kama Nyerere alivyopinga ukaburu.

Kwa sheria za kimataifa, baada ya tukio lile la kimbali la Rwanda, kwa sasa mataifa yana mamlaka ya kuingia nchi yoyote kama lengo ni kwenda kuzuia mauaji ya jamii au kundi fulani.

Sovereignity ya nchi haipo katika kuwafanyia uovu watu unaowaongoza.
 
Huo ujeuri hana. Ajaribu kuwafukuza hao mabalozi, kama ana jeuri hiyo. Wewe Serikali yako iteke na kuua watu halafu useme unajua la kufanya!!

Ameota mapembe kiasi cha kuona ana mamlaka ya kuamua nani aishi, na nani afe muda anaoutaka yeye!!
hakuna ujeuri wala ubabe kwenye masuala ya kimataifa na diplomasia gentleman,

ni ustaarabu unaozingatia mila, desturi na sheria za kimataifa na kila taifa lililotuma muwakilishi wake kwenye nchi yeyote lazima azingatie, vinginevyo atafurushwa nyumbani mara moja...

hayo mengine hayahusiani 🐒
 
Mabalozi wamesema sana juu ya hali ya usalama na haki za binadamu Zanzibar. Mara zote wamepuuzwa na hawakuchukuwa hatua zozote. Kauli zao ni danganya toto.
 
Aliyesema hivo ni kichaa.kwa hiyo anaunga mkono utekaji na uuaji wa watu?Kwa hiyo mabalozi wasiseme maovu wanayoyasema?
hata huko kwao kuna mauaji na unyama mwingi unafanyika. Pia amewataka watambue kuwa uhai wa kila Mtanzania ni muhimu....wakemee na vibaka, watekaji maalbino na watoto, siyo kubagua wanaowataka wao tu!
 
sasa mtu anasaga na kukoboa atakuaje na akili timamu?
Mimi hayo yote siyaamini
Lakini pia siamini kama huyu mama anaweza fanya huu unyama,,
Hawezi kuwa na roho mbaya kiasi hicho Cha kumwaga damu

Lakini anatuangusha Kwa kulegeza kamba ,hawa wauaji walitakiwa wawe wameshapatikana siku zilezile Kwa usalama wa taifa letu...hadi sasa ni blah blah tu.
Inaumiza sana.
 
Yes hicho ndicho,
Lazima waheshimu mila, utamaduni , desturi, katiba na sheria za nchi yetu huru,
vinginevyo wasipobadilika mabalozi hao wote watarudishwa makwao bila mbambambba yoyote 🐒
Mkuu Unaelewa maana ya neno m?a ,utamaduni na desturi!? Kuua watu mayo ni Mila ,desturi au utamaduni!?

Haya uliyoyaandika ulipaswa kujua maana yake ikiwa angalau ulikomea form two ,
 
Back
Top Bottom