Pre GE2025 Rais Samia kwa Mabalozi: Hatupo hapa kuelekezwa nini cha kufanya kwenye nchi yetu

Pre GE2025 Rais Samia kwa Mabalozi: Hatupo hapa kuelekezwa nini cha kufanya kwenye nchi yetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Chura kumbe anackia!! Omba omba hana chake kila mara kiguu na njia kwenda kwao.
All the best
 
Kilichofuata kilikuwa ni bendera nusu mlingoti.
Mzee alikuwa akiishi kwa kutumia kijenereta cha moyo kilichotengenezwa na kuendeshwa kwa akili za beberu, na kila kikisumbua beberu aliitwa kukiweka sawa, kijenereta sijui kilizimwa vile watu wakarudi kati.
 
Mkuu Unaelewa maana ya neno m?a ,utamaduni na desturi!? Kuua watu mayo ni Mila ,desturi au utamaduni!?

Haya uliyoyaandika ulipaswa kujua maana yake ikiwa angalau ulikomea form two ,
halipo taifa lolote lililostaarabika na linalozingatia mila, desturi, utamaduni na sheria za kimataifa ulimwenguni, eti kupitia balozi wake lielekeze taifa husika namna ya kudeal na mambo yake ya ndani,

take it from me,
huo ni ukiukwaji wa Sheria na ustaarabu wa kimataifa na yeyote anaekwenda kinyume anastahili kufurushwa kwao mara moja...

hayo mengine nadhani nimeshayaelezea sana maeneo mengine 🐒
 
Chura kiziwi amesahau mwaka kesho anakwenda kuwapigia magoti,kuwaomba fedha za uchaguzi mkuu?
Umeingia hofu,subiri watakujibu
Kuwa na adabu,yule ni Raisi wa Jamhuri, vilevile yule ni mama.
Asiyefundwa na wazazi wake atafunzwa na singeli.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hivi karibuni amejibu kuhusu matamko yaliyotolewa na balozi mbalimbali hapa nchini Tanzania kufuatia kifo cha Kada wa CHADEMA, Ali Kibao.

Mara baada ya Ali Kibao kupatikana akiwa amefariki huko Ununio, Dar Es Salaam balozi za nchi mbalimbali kama Marekani, Ufaransa na Umoja Wa Ulaya yaani EU walijitokeza kukemea kitendo hicho na kuitaka serikali ya Tanzania kufanya uchunguzi wa haraka.

Soma Pia: Rais Samia: Mauaji ya Kibao hayakubaliki. Uchunguzi umeanzishwa

Leo akiwa anatoa hotuba kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi La Polisi, mkuu huyo wa nchi amedokeza kuwa hayuko tayari kuelekezwa nini cha kufanya na kwamba Tanzania ina katiba na miongozo yake na kwamba sisi tunajua nini cha kufanya.

View attachment 3098778

Source: Mwananchi
Tofauti ni chombo cha Sirikali kutuhumiwa na sio suala la mtoto. Je suala la Floyd na mengine kama hayo yalifichwa au yalishughulikiwa ipasavyo. Na US
 
Mtawala aliyeitangazia dunia kuwa kuzurula kwake huko na huko duniani ni kwa ajili ya kuomba omba visenti na kuwalamba viatu wakubwa wale ili wampe chochote (kwa masharti yoyote yale) cha kuja kuendeshea nchi yake inayodidimia vibaya, sasa leo hii amesikika akisema wakubwa wale anaowategemea wampe chochote wasimpangie cha kufanya!

Mtawala amesahau ule msemo unaosema 'anayemlipa mpiga ngoma ndiye anayechagua midundo ipi ya ngoma ipigwe'.
Mswahili ameanza kutukuna mamba kabla ya kuvuka mto.

Muda utatufundisha kitu.
Hoja yake ni kwamba ni kweli walichokisema ni maagizo kutoka kwa marais wa nchi zao au wanaleta siasa? Binafsi sijaona alipokosea
 
Kilichofuata kilikuwa ni bendera nusu mlingoti.
Mzee alikuwa akiishi kwa kutumia kijenereta cha moyo kilichotengenezwa na kuendeshwa kwa akili za beberu, na kila kikisumbua beberu aliitwa kukiweka sawa, kijenereta sijui kilizimwa vile watu wakarudi kati.
Wewe utafia Guest house 😂
 
Chura kiziwi amesahau mwaka kesho anakwenda kuwapigia magoti,kuwaomba fedha za uchaguzi mkuu?
Umeingia hofu,subiri

Chura kiziwi amesahau mwaka kesho anakwenda kuwapigia magoti,kuwaomba fedha za uchaguzi mkuu?
Umeingia hofu,subiri watakujibu
Nilitegemea anakuja kukemea mauaji kumbe hapana basi hawezi kukwepa hizi lawama
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hivi karibuni amejibu kuhusu matamko yaliyotolewa na balozi mbalimbali hapa nchini Tanzania kufuatia kifo cha Kada wa CHADEMA, Ali Kibao.

Mara baada ya Ali Kibao kupatikana akiwa amefariki huko Ununio, Dar Es Salaam balozi za nchi mbalimbali kama Marekani, Ufaransa na Umoja Wa Ulaya yaani EU walijitokeza kukemea kitendo hicho na kuitaka serikali ya Tanzania kufanya uchunguzi wa haraka.

Soma Pia: Rais Samia: Mauaji ya Kibao hayakubaliki. Uchunguzi umeanzishwa

Leo akiwa anatoa hotuba kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi La Polisi, mkuu huyo wa nchi amedokeza kuwa hayuko tayari kuelekezwa nini cha kufanya na kwamba Tanzania ina katiba na miongozo yake na kwamba sisi tunajua nini cha kufanya.

View attachment 3098778

Source: Mwananchi
Chura kiziwi katika ubora wake. Kesho anaendelea kwao kutembeza bakuli.
 
Back
Top Bottom