Pre GE2025 Rais Samia kwa Mabalozi: Hatupo hapa kuelekezwa nini cha kufanya kwenye nchi yetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Balozi namba moja rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo anatekeleza sera yake ya mahusiano ya kimataifa, kwa kukataa kuna tatizo Tanzania na kuwa hahitaji msaada wa kiufundi na kiuzoefu kupambana na genge la kihalifu liloishinda jeshi la polisi la Tanzania pia Idara ya Usalama wa Taifa TISS.

Kwa tamko hili la balozi namba moja ambaye ni Rais amiri jeshi mkuu na mfariji , wahuni hawa wanaoitwa watu wasiojulikana wakiamua kufanya matukio makubwa zaidi kwa kuwa sasa Tanzania imejitutumua haitaki kushirikiana na vyombo vingine mahiri vya nchi zingine kitachotokea ina maana lawama zipo katika mabega ya rais.

Hawa wahuni wasiojulikana kiaina watakuwa hofu ya kushughulikiwa kimataifa haipo na kwa vyombo vya ndani vinawaogopa ni kwamba kuna mawili yataibuka.

Vitendo hivi vya kuteka, kupoteza na kuua vitakoma kwa sababu zisizojulikana au vitashamiri ikiwa kweli serikali haihusiki kabisa na wahuni hawa.

Muda utatupa majibu ya scenario (mazingira) hizi mbili matukio kuisha kabisa au matukio kupamba moto mkali zaidi. Kwa akili na ufahamu wa kawaida jibu litapatikana upande gani unahusika dola (state) au wahuni wanaojitegemea bila nguvu ya dola waliopachikwa jina genge la watu wasiojulikana.
Acheni utumwa wa kujiona hamuwezi na mpaka mtegemee kila kitu kutoka kwa hao wageni.

Punguzeni huu unyonge, sio kila kitokacho huko nje basi tukione ni cha kweli na chenye haki ya kusikilizwa.
 
Kiburi cha madaraka live kwa tv😱😳,hofu ya kutekwa ya watanzania haimhusu.
Dunia nzima unafanyika unyama wa kuteka na kutekwa, punguzeni hizi nongwa za kitoto.

Huko USA kila siku wanaokota maiti na polisi wanaanza uchunguzi na kuna mwingine unachukua mpaka miaka 20 kupata uhakika wa wahusika wa vifo.

Hali ngumu ya maisha huja na mengi, kwa wengine ni changamoto nzuri na kwa wengine ni balaa la vifo.
 
Mtu aliye karibu na Rais wetu anisaidie kumuuliza kama kuna siku Tanzania imewahi kutoa msaada wa kifedha kwa Marekani.

Kama unaenda kutembeza bakuli kuombaomba pesa za kuendesha nchi yako utapangiwa tu na watakuelekeza hata jinsi ya kuongoza na hakuna kitu utawafanya.

Kuhusu utekaji na mauaji, Katibu Mkuu wa Chama aliongea vizuri kwa utulivu na umakini mkubwa, yeye kaja kuongea ndio ameharibu mwanzo mwisho.
Halafu Kesho kiguu na njia kwenda kuomba MKOPO wa kununuua ma V8

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hivi karibuni amejibu kuhusu matamko yaliyotolewa na balozi mbalimbali hapa nchini Tanzania kufuatia kifo cha Kada wa CHADEMA, Ali Kibao.

Mara baada ya Ali Kibao kupatikana akiwa amefariki huko Ununio, Dar Es Salaam balozi za nchi mbalimbali kama Marekani, Ufaransa na Umoja Wa Ulaya yaani EU walijitokeza kukemea kitendo hicho na kuitaka serikali ya Tanzania kufanya uchunguzi wa haraka.

Soma Pia: Rais Samia: Mauaji ya Kibao hayakubaliki. Uchunguzi umeanzishwa

Leo akiwa anatoa hotuba kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi La Polisi, mkuu huyo wa nchi amedokeza kuwa hayuko tayari kuelekezwa nini cha kufanya na kwamba Tanzania ina katiba na miongozo yake na kwamba sisi tunajua nini cha kufanya.

View attachment 3098778

Source: Mwananchi
Safi sana wafanye yaliyowaleta!
 
kama rais amesema vile, mjue kuwa haya yoooooooooooooooote yana baraka zake. Anajua fika nini kinaendelea na anaagiza yeye
Nope

Kajieleza vizuri sana kwamba sisi hatupendi yanayotokea lakini pia wenzetu waheshimu rights na sovereignty ya nchi yetu
 
Balozi namba moja rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo anatekeleza sera yake ya mahusiano ya kimataifa, kwa kukataa kuna tatizo Tanzania na kuwa hahitaji msaada wa kiufundi na kiuzoefu kupambana na genge la kihalifu liloishinda jeshi la polisi la Tanzania pia Idara ya Usalama wa Taifa TISS.

Kwa tamko hili la balozi namba moja ambaye ni Rais amiri jeshi mkuu na mfariji , wahuni hawa wanaoitwa watu wasiojulikana wakiamua kufanya matukio makubwa zaidi kwa kuwa sasa Tanzania imejitutumua haitaki kushirikiana na vyombo vingine mahiri vya nchi zingine kitachotokea ina maana lawama zipo katika mabega ya rais.

Hawa wahuni wasiojulikana kiaina watakuwa hofu ya kushughulikiwa kimataifa haipo na kwa vyombo vya ndani vinawaogopa ni kwamba kuna mawili yataibuka.

Vitendo hivi vya kuteka, kupoteza na kuua vitakoma kwa sababu zisizojulikana au vitashamiri ikiwa kweli serikali haihusiki kabisa na wahuni hawa.

Muda utatupa majibu ya scenario (mazingira) hizi mbili matukio kuisha kabisa au matukio kupamba moto mkali zaidi. Kwa akili na ufahamu wa kawaida jibu litapatikana upande gani unahusika dola (state) au wahuni wanaojitegemea bila nguvu ya dola waliopachikwa jina genge la watu wasiojulikana.
aicc kuna wakati wanataka watu waende kutembea kule uholanzi
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hivi karibuni amejibu kuhusu matamko yaliyotolewa na balozi mbalimbali hapa nchini Tanzania kufuatia kifo cha Kada wa CHADEMA, Ali Kibao.

Mara baada ya Ali Kibao kupatikana akiwa amefariki huko Ununio, Dar Es Salaam balozi za nchi mbalimbali kama Marekani, Ufaransa na Umoja Wa Ulaya yaani EU walijitokeza kukemea kitendo hicho na kuitaka serikali ya Tanzania kufanya uchunguzi wa haraka.

Soma Pia: Rais Samia: Mauaji ya Kibao hayakubaliki. Uchunguzi umeanzishwa

Leo akiwa anatoa hotuba kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi La Polisi, mkuu huyo wa nchi amedokeza kuwa hayuko tayari kuelekezwa nini cha kufanya na kwamba Tanzania ina katiba na miongozo yake na kwamba sisi tunajua nini cha kufanya.

View attachment 3098778

Source: Mwananchi
no longer at ease
 
Back
Top Bottom