Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais Samia Suluhu ametaja changamoto tatu ambazo amekutana nazo tangu awe Rais wa Tanzania lakini ameonyesha nguvu ya Mwanamke kwa kuongoza Nchi vizuri na katika hali fulani amezidi hata kile kilichofanywa na Wanaume ndani ya mwaka mmoja.
Akizungumza wakati akishiriki Mdahalo wa Wakuu wa Nchi unaofanyika Accra, Ghana, leo Mei 24, 2022 amesema: “Changamoto kubwa ya kwanza ilikuwa kuaminiwa, Mwanamke wa kwanza kushika nafasi kubwa, kuwafanya watu wa Tanzania waniamini.
“Niliongoza Nchi vizuri kama Wanaume wanavyofanya inawezekana zaidi ya kile walichokuwa wanafanya wao.”
Anasema: “Changamoto nyingine ni kuhusu maambukizi ya Ugonjwa wa Covid-19 ambayo yalikuwa yakiisumbua Dunia, uchumi haukuwa mzuri. Nilikabiliwa na kibarua cha kukuza uchumi wa Tanzania.
“Changamoto ya tatu, uchumi ulipokuwa ukishuka nilijiuliza wapi pa kuanzia, nashukuru washirika, ikiwemo African Development Bank, wametusaidia katika ujenzi wa miundombinu, kilimo. Hivyo, kwa msaada wao na washirika wengine tulifanya vitu vizuri kadhaa.
“Kutokana na maambukizi ya Covid-19, tulipata fedha kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) kama ilivyotoa kwa mataifa mengine, wengi walitumia kwa matumizi ya kupambana na maambukizi.
“Tulichoamua ni kutumia sehemu ya fedha hizo kwa ajili ya kuboresha madarasa, kusambaza maji katika maeneo mengi ya nchi ambayo upatikanaji wake ulikuwa kama 72% lakini tukasogea hadi 80% na tunatarajia hadi kufikia 2025 maeneo ya mijini inaweza kuwa 92% na 85% kwa Vijijini, pia tumetumia kwa ajili ya masuala ya kuboresha huduma za afya.