Mheshimiwa Rais, suala la Mkataba wa Bandari limefichua nyufa kubwa za Taifa letu hasa katika suala la Dini, Muungano, Ukabila, Ukanda, Jinsia na Itikadi za Siasa. Sasa naomba nikushauri kwa unyenyekevu mkubwa epuka mtego wa wasaidizi wako hasa huu wa kukamata watu na kuwaambia ni wahaini.
Huu ni mtego Mkubwa kwako ili 2025 ubaki mkiwa na watakutoa sadaka. Usicheze na Hawa Jamaa wana mbinu balaa. Hivi unadhani unaweza mfunga Dr. Slaa halafu watu wa dini za mlengo wake wakakaa kimya, watakuandama balaa na watataka kuthibitisha madai ambayo mimi sitaki kuamini ya udini na mambo kama hayo. Vilevile waliokamatwa kwa uhaini wote ni watanzania bara, hili nalo litaongeza ufa uliopo katika Muungano.
Ushauri Wangu, kuwa makini kubali sauti za kila upande, amua kwa busara, jikabidhi kwa Mungui akupe busara, hekima na uthabiti.