Rais Samia: Majirani zetu wanazo The so called 'Tume Huru', hawana migogoro? Auliza nini kinafatwa kwenye tume huru

Rais Samia: Majirani zetu wanazo The so called 'Tume Huru', hawana migogoro? Auliza nini kinafatwa kwenye tume huru

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Rais Samia akiwa anapokea ripoti ya kikosi kazi alichounda ameongelea Tume huru ya uchaguzi na kuhoji uwepo wa kuendelea migogoro kwenye nchi za jirani zinazotajwa kuwa na tume huru.

Rais Samia ametaka kujua 'Definition' ya tume huru na ipi kiu itakayopatikana kwenye tume huru.

======

Samia Suluhu: Tume huru hizo na nini mtatulete mapendekezo, tume huru maana yake nini!

Iweje? Lakini angalieni na mifano ya waliokuwa na tume huru, Je hawana migogoro ya kisiasa? The so called 'Tume Huru'.

Kwa mfano majirani zetu wanazo The so called 'Tume Huru' lakini zinaendeshwaje? Hawana migogoro? Hawatangazi matokeo wakakimbia nchi kabisa?

Si hutangaza matokeo kisha wakakimbia! Nendeni nchi mbalimbali zenye hizo zinazoitwa tume huru, angalieni yanaendaje lakini tunaposema tume huru tunafata nini hasa huko kwenye tume huru.

Kitu gani kinatupa kiu tunahisi tutakipata kwenye tume huru huko na definition hasa ya tume huru ni nini?

===

Kuhusu maboresho ya sheria na kanuni za Uchaguzi, Rais Samia amesema watasema vipengele gani vinavyouma kwani inawezekana maboresho yakifanyika, kelele ya katiba inaweza ikaishia kwasababu zile kiu za watu zinapotaka katiba ibadilishwe ilishafanyiwa kazi.

PIA, Soma=> Ikulu, Dar es Salaam: Rais Samia apokea taarifa ya Kikosi Kazi cha Kuratibu Maoni ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa
 
Sahihi kabisa Mh.Rais

Kuna Wanasiasa wakubwa tu hawajui hata tofauti ya Tume huru na Tume yenye wawakilishi wa Vyama

Kabla ya kuundwa kinachoitwa Tume huru kwanza watu wapewe elimu ya kujua Tume huru ipoje ipoje lakin pia waelezwe Tume huru sio muarobaini wa kila changamoto ya Uchaguzi na ndio sababu kwa majirani zetu nyakati za Uchaguzi huwa kinanuka vya kutosha japo kuna Tume huru na hiyo Katiba Mpya
 
Nashangaa mbona yeye ndie anakuwa kikwazo cha upatikanaji wa hiyo Tume Huru? anyway wengine hatutaki Tume Huru tunataka Katiba Mpya.

Halafu kama hajui maana ya Tume Huru kwanini asiulize akajibiwa kuliko kujitokeza hadharani na kuanza kutoa kauli zitakazoleta sintofahamu?

Vipi Zitto hawezi kumuelewesha rafiki yake kwenye hili?

Huyu Rais kama walivyo CCM wenzake hawana nia ya dhati ya kutupa Katiba Mpya wala Tume Huru ya uchaguzi, yote yanayoendelea kuunda timu zao za vikosi kazi vya uongo ni maigizo matupu, wananchi tusipoamua tutasubiri sana.
 
Suala la kutangaza matokeo na kukimbia, ni kwasababu ya ubora wa tume huru.

Hapa kwetu wakisha mnyonga mtu hawakimbilii nje kwasababu walie mpendelea ndo yupo madarakani atawalinda na walionyongwa hawana la kumfanya.

Eti huko kwenye time guru kunamigigoro.

Kuna migogoro kwasababu katiba zinawapa meno ya kuhoji, hapa kwetu ni vifatu tu utakutana navyo badala ya nguvu ya hoja.

Hatuna migogoro inayoonekana kwasababu ya kukaliwa kimabavu.

Fanya yote, tupe katiba mpya, hayo mengine tutayashughulikia kwani hatusemi baada ya katiba kutakuwa hakuna mambo yatakayo hitaji maboresho tena.

Kwa sasa tupe katiba usituzuge
 
The so called Tume huru - alisikika Mhe Rais Samia Suluhu hassan

Wet shit, gone stone
 
Huenda hao wana So called Tume Huru ila hawana Tume Huru

In short hata iliyopo duniani ni so called demokrasia lakini sio demokrasia ya kweli...

LAKINI..., faida ya hivi vitu ni kama wenzetu wanasheria wanavyosema -
Justice should not only be done but should manifestly and undoubtedly be seen to be done”.

Kwahio watu wakiona kwamba TUME ni huru hata malalamiko / sababu / excuses zitapungua hence huenda tukahamia kwenye malalamiko na Kero nyingine..., ila sababu ya kwamba fulani ingawa anacho hiki ila analalamika sio mtaji wa kutokufanya hilo jambo...

KAMA Tume sio Huru kwanini tuendelee kuwanayo ? Si bora isiwepo kabisa hili hivyo vijisenti vikafanye mengine ?
 
Tume huru yenye mamlaka na mipaka haiwezi kutokana na katiba hii ya 1977 ambayo base yake ilikuwa ni ya chama kimoja cha siasa.

Ni sawa na kujenga ghorofa kwenye msingi wa matope.
 
Namkubali Mama lakini naona kuna maeneo kama ana U-mbogamboga badala ya kukaa nyutro akaishepu nchi,dawa ya kuondoa malalamiko ni kutia kinachodaiwa,mambo mawili huwa mbogamboga hawayakubali na huenda hawatayakubali kitahisi ni TUME HURU NA KATIBA MOYA KABISA,siyo iliyokarabatiwa.

Haoa Mama atupatie vyote viwili,awe na legacy yake.
 
Mama anaweweseka. Anajua hawezi kushinda urais wa Tanzania kwa haki...

Kura za kwenye vikapu lazima zitumike na hakuna kupinga matokeo mahakamani!!

Jibi swali na ikiwezekana jenga hoja...

Hoja ya mama ipo hapa, nini maana ya tume huru na je tufanyaje ili tume huru yetu kweli itatue matatizo maana zipo nchi zilitumia muda mwingi kuunda na kutafuta tume huru na katiba pia, lakini hizo nchi mpaka leo bado zina matatizo kwenye chaguzi na hiyo Katiba...

Nimekusaidia kudadavua, tujaribu kuwa positive ili kupata tiba ya matatizo yetu...
 
Suala la kutangaza matokeo na kukimbia, ni kwasababu ya ubora wa tume huru.

Hapa kwetu wakisha mnyonga mtu hawakimbilii nje kwasababu walie mpendelea ndo yupo madarakani atawalinda na walionyongwa hawana la kumfanya.

Eti huko kwenye time guru kunamigigoro.

Kuna migogoro kwasababu katiba zinawapa meno ya kuhoji, hapa kwetu ni vifatu tu utakutana navyo badala ya nguvu ya hoja.

Hatuna migogoro inayoonekana kwasababu ya kukaliwa kimabavu.

Fanya yote, tupe katiba mpya, hayo mengine tutayashughulikia kwani hatusemi baada ya katiba kutakuwa hakuna mambo yatakayo hitaji maboresho tena.

Kwa sasa tupe katiba usituzuge

Sasa maana yakuvitafuta hivyo vitu ni nini? kama hata vikiwepo migogoro bado inaendelea ...
 
Sahihi kabisa Mh.Rais

Kuna Wanasiasa wakubwa tu hawajui hata tofauti ya Tume huru na Tume yenye wawakilishi wa Vyama

Kabla ya kuundwa kinachoitwa Tume huru kwanza watu wapewe elimu ya kujua Tume huru ipoje ipoje lakin pia waelezwe Tume huru sio muarobaini wa kila changamoto ya Uchaguzi na ndio sababu kwa majirani zetu nyakati za Uchaguzi huwa kinanuka vya kutosha japo kuna Tume huru na hiyo Katiba Mpya
Ndiyo Mnayoongea na Zungu Mchikichini hayo, Tume huru ni huru kwa muundo wowote ule.
 
Jibi swali na ikiwezekana jenga hoja...

hoja ya mama ipo hapa, nini maana ya tume huru na je tufanyaje ili tume huru yetu kweli itatue matatizo maana zipo nchi zilitumia muda mwingi kuunda na kutafuta tume huru na katiba pia, lakini hizo nchi mpaka leo bado zina matatizo kwenye chaguzi na hiyo Katiba...

Nimekusaidia kudadavua, tujaribu kuwa positive ili kupata tiba ya matatizo yetu...
Yeye alete tume huru, maana take adiyo weza kuiinhilia kwa njia yoyote ile, halafu hayo mengine yatajitengeneza yenyewe, asitutishe juu ya migogoro.

Hoja yetu sio kuondoa migogoro, hoja ni kumzuia raisi kulazimisha ushindi wake na chama chake kama 2020.
 
Back
Top Bottom