Rais Samia: Majirani zetu wanazo The so called 'Tume Huru', hawana migogoro? Auliza nini kinafatwa kwenye tume huru

Rais Samia: Majirani zetu wanazo The so called 'Tume Huru', hawana migogoro? Auliza nini kinafatwa kwenye tume huru

Tatizo kuu la Mama ni hofu ya kupoteza hapo 2025! Hataki chama kimfie mikononi!!hataki kuwa mbuzi wa kafara!!anajitutumua Sana !!
 
Mambo mengi uliyoyaelezea hapa baadhi yake sio ya kweli kabisa, mengine ni controversial au pseudo truths. Hakuna facts.
Hata bila kuwaza sana President Bush kwa kuwa na urafiki na Kampuni ya Enron alipush kubadilisha Sera za Energy (kufanya Energy iweze kuuzwa kama vile stock nyingine) na kuwapa financial leeway Kampuni ya Enron...
 
Tume Huru ni kitu cha kufikirika zaidi kuliko uhalisia.

Angalia chaguzi za Ghana pamoja na kuitwa za mfano Africa lakini walioko ndani wanagomea matokeo na kuilaumu tume.
 
Ikiwa default setting ya mifumo ya tawala za kibinadamu ni uimla(autocraticism), kivipi demokrasia in it's purest form inaweza kuleta shida kama hizo za tyranny of majority?
Hivi umenisoma tangia mwanzo ? Sababu nadhani ni kama kuna wawili majibu ninayotoa na wewe majibu unayojibu sio majibu niliyotoa...

Katika moja ya Matatizo ya Demokrasia ni Tyranny of the majority na hio inaweza ikawa countered sio kuwa na mfumo mbadala bali kuzingatia individual rights zinakuwa taken care of.

Hapo jibu langu kwako lilikuwa naongelea decisions making na sio mahitaji ya watu (hapo tukija kwenye mahitaji ni another chapter) Kwahio naongelea ile decision making (theoretically ni kwamba kila mtu anaamua, ila realistically sio hivyo) Ingawa kuna forms of direct democracy na sio representative ambazo kila mtu anaweza kuamua (ingawa its practicability is not easy).

Kwamba kwenye autocraticism minority rights zina uhakika wa kuheshimiwa sana AU ulimaanisha demokrasia bado inaweza isiziondoe hizo shida?
Neither democracy nor autocratism inaweza kuziondoa hizo bali lazima democracy iwe countered / checked na individual rights bila hivyo kuna watu watapata shida sababu tu ni wachache kwahio ndio nikakwambia what majority always says / wants is not always right (argumentum ad populum)

Lakini hapo tunatoka nje ya topic na Debate sio kwamba Demokrasia ni nzuri au mbaya bali uwepo wa Demokrasia ya kweli Duniani
Madhara ya Lobbying za interest groups na blah blah nyingine ulizozitaja hapo chini ni malalamiko yako tu(ambayo ni petty) dhidi ya mifumo ya demokrasia , sio kila mtu anaona Lobbying za makampuni/wafanyabiashara (kwenye kodi, udhibit , mazingira wezeshi n.k), Lobbying za vyama vya wafanyakazi n.k ni mbaya.
Kwahio sababu kuna lobbying nzuri basi na lobbying mbaya ni nzuri ? Umeniambia nitoe mifano ya lobbying USA na Ulaya nimekupa michache hapo mingine ambayo ilifika hadi kwenye meza za White House President.

Kwahio hapa tatizo hilo linaweza kuwa solved sio wachache kupewa nguvu ya policy making na wakamaliza wenyewe (hapo decision makers sio watu per se bali baadhi ya watu ambao wanajifanya ku-represent watu ila mwisho wa siku wanarepresent corporations ambazo zina pesa zaidi) Na hili limekuwa likijitokeza time and time and time again kila corporation lazima iwe na lobbyist wa kutosha na kutenga funga la pesa za kutosha ili mambo yake yaende sawa....

Again hapa debate sio uzuri au ubaya wa lobbist bali uwezekano wa a few to get their agendas through lobbyists (and this goes against democracy sababu decisions are being made by the powerful with deep pockets and not common mwananchi without a dime)

Which takes me back to my original point.., The Real Power to the People remains to be un-achieved na sio kwamba haiwezekani bali the powers that be would not like it....
 
Hadi kichefuchefu, utafikiri mtoto wa Darasa la pili ndo anaongea.
 
Rais Samia akiwa anapokea ripoti ya kikosi kazi alichounda ameongelea Tume huru ya uchaguzi na kuhoji uwepo wa kuendelea migogoro kwenye nchi za jirani zinazotajwa kuwa na tume huru...
Majibu mazuri sana kwa akina Zitto & co. wanaofikiri kuwa Tume Huru ya Uchaguzi nje ya Katiba Bora itakuwa na tija.

Kwa mujibu wa Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa ccm, Tume huru ishafeli kabla haijaanza kazi

Sitaki kuwaharibia ulaji wao!
 
Mambo mengi uliyoyaelezea hapa baadhi yake sio ya kweli kabisa, mengine ni controversial au pseudo truths. Hakuna facts.
Chagua moja nikupe facts au hilo la Bush na Enron ndio limekushitua ?

Au Deregulation kwenye Banks haikuanza kipindi cha Bush na Bankers ku-lobby ili kupunguza sheria ?

Au hakukuwa na Scandal ya Lordship for Hire huko UK...

Mbona its a well know fact bila kulainisha hawa decision makers jambo lako haliendi ? (Ila tatizo wanaolainishwa sio wananchi for their benefit bali wachache wanaojifanya kufanya maamuzi waliyotumwa na mwananchi)
 
Nashangaa mbona yeye ndie anakuwa kikwazo cha upatikanaji wa hiyo Tume Huru? anyway wengine hatutaki Tume Huru tunataka Katiba Mpya...
Rais anayo hofu kubwa sana; anaonekana kujiamulia kuwa yeye ndiye mwenye kujua nchi hii inataka nini. Baada ya kilichotokea kwenye uchaguzi Zanzibar 2015 na nchi nzima 2020 usingetegemea kiongozi yeyote anayejiheshimu kuonyesha kuwa na mashaka na kukejeli dhana ya tume huru.
 
Ni Watanzania kuwa na mamlaka ya kuchagua viongozi wao kwa kura zao. Siyo wale wa kura za kwenye mabegi. Uchaguzi huru na wa haki ni aspect moja tu ya Katiba.

Kuna tunu za Taifa zilizopendekezwa na Watanzania watoa maoni yao kwa Tume ya Waryoba. Na kushinda uchaguzi siyo kwa TLP ama CHADEMA tu. Hata CCM nayo itapongezwa kama itashinda bila kutegemea kura za kupigia kwenye mahoteli.

Kwahiyo kumbe lengo kubwa la Tume huru ya uchaguzi na Katiba Mpya Ni kushinda uchaguzi🤣🤣🤣
 
Unajichekesha kama wenyeji wa nchi ya Malaysia (Malaya kwa Kiswahili). Kuna lipi la kukuchekesha hapo?
Kwahiyo kumbe lengo kubwa la Tume huru ya uchaguzi na Katiba Mpya Ni kushinda uchaguzi🤣🤣🤣
 
Rais Samia akiwa anapokea ripoti ya kikosi kazi alichounda ameongelea Tume huru ya uchaguzi na kuhoji uwepo wa kuendelea migogoro kwenye nchi za jirani zinazotajwa kuwa na tume huru...
Aendelee kujilisha upepo
 
Rais Samia akiwa anapokea ripoti ya kikosi kazi alichounda ameongelea Tume huru ya uchaguzi na kuhoji uwepo wa kuendelea migogoro kwenye nchi za jirani zinazotajwa kuwa na tume huru...
Na ameongea hayo mbele ya mwanae Zitto ?😀
 
Mimi sitaki tume huru wala katiba mpya.

Nataka watu waelimishwe kwanza wajitambue kabla ya kuvipata vyote hivyo...
Ukweli ni kwamba tangu chaguzi za vyama vingi zirudi tena 1995 kumekuwa na malalamiko ya uchakachuaji wa matokeo na wizi wa kura na kwamba tume siyo huru. Binafsi sikuyapa uzito mkubwa sana tuhuma hizo kwani kwa macho ya raia wa kawaida demokrasia iliendelea kukua. Hali hii ilikuja tu kubadilika ghafla tuliposhuhudia matokeo ya urais wa Zanzibar 2015.

Kabla ya hapo nchi yetu ilikuwa na ustaarabu wa kutosha katika siasa. Ustaarabu huu uliwafanya wenye madaraka kuona haya. Kilichofuata kwenye chaguzi ndogo baada ya 2015 kiliendelea kuelimisha zaidi umma kuwa siasa zetu sasa zimeingiliwa na wahuni!. Hakuna ustaarabu tena. Elimu hii ilihitimishwa 2019 na 2020 kwamba tatizo sasa siyo uhuni tu bali kuna uharamia pia.

Akapatikana na mtaalam wa siasa aliyetamka hadharani kuwa dola itatumika kuhodhi madaraka! Wanaohitaji elimu sasa siyo raia bali wanasiasa walioshikilia madaraka. Mama Samia sasa anao wakati mgumu sana kulinda huo uhuni na uharamia kiasi cha kulazimika kukejeli dhana ya tume huru! Mungu amsaidie sana.

Lakini kama raia kamili wa nchi hii tunao wajibu wa kutambua kuwa kubwa linalowasumbua wanasiasa wetu sasa ni hofu ya kupoteza madaraka huku kukiwa na tuhuma za uhalifu mkubwa uliofanyika chini yao miaka ya hivi karibuni.

Pengine tunahitaji kwanza kuweka utaratibu wa ukweli, usuluhishi na upatanisho kitaifa. Kinyume chake tutaangamiza hii nchi kwa sababu ya watu wachache wenye shida zao binafsi wanaotamani kuwatumia raia maskini kama human shield kujilinda wao wenyewe.
 
Mimi sitaki tume huru wala katiba mpya.

Nataka watu waelimishwe kwanza wajitambue kabla ya kuvipata vyote hivyo.

Hakuna tija ya kuwa na vifaa vipya kabla ya kujifunza kwanza kuvitumia.

Tuondoane ujinga kwanza ndio twende huko.
Katiba mpya siyo rocket science kiasi cha kuwalazimisha watanzania kupewa elimu kwanza juu ya umuhimu wa Katiba mpya ambayo imekuwa hitaji lao la mda mrefu.
 
Jibi swali na ikiwezekana jenga hoja...

Hoja ya mama ipo hapa, nini maana ya tume huru na je tufanyaje ili tume huru yetu kweli itatue matatizo maana zipo nchi zilitumia muda mwingi kuunda na kutafuta tume huru na katiba pia, lakini hizo nchi mpaka leo bado zina matatizo kwenye chaguzi na hiyo Katiba...

Nimekusaidia kudadavua, tujaribu kuwa positive ili kupata tiba ya matatizo yetu...

..Mama angeeleza, kwa uelewa wake, tume huru ni kitu gani.

..vinginevyo ataonekana anapinga kitu asichokielewa.
 
Rais Samia akiwa anapokea ripoti ya kikosi kazi alichounda ameongelea Tume huru ya uchaguzi na kuhoji uwepo wa kuendelea migogoro kwenye nchi za jirani zinazotajwa kuwa na tume huru...
Mh.Rais yuko sahihi.....

TUME HURU za uchaguzi ndio mwanzo wa migogoro.

Afrika haihitaji SIASA ZA KINAFIKI zenye mwelekeo wa maelekezo ya IMPERIAL FORCES.....imperialism is the highest form of capitalism.

Siasa ya CCM ndio siasa bora ya kuigwa barani Afrika.

Watanzania tuamke na tuache kufanywa mazuzu na wanaotaka siasa za BIASHARA NA ZA KUENDESHWA NA "rimoti" kutoka nje ya bara letu.

#Siempre SSH🙏
 
Back
Top Bottom