econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Huyu Rais kaanza kampeni mapema kabla ya muda. Sijui anaogopa Nini? Tume ya Uchaguzi ni ya kwake, Polisi wa kwake, JWTZ wa kwake nk ila kaanza kampeni kabla ya muda.
Naomba nimpe Rais ushauri ufuatao;
1. Achana na kampeni kabla ya muda.
Wewe kama Rais wa Nchi unatakiwa kuwa namba moja Kwa kutii Sheria. Sheria ya uchaguzi inahitaji kampeni zifanyike kwenye muda wa kampeni na si vinginevyo. Rais unapopita huku na kule na kuwaambia wananchi wasiwachague wapinzani bado ni wachanga bali wachague CCM hiyo ni kampeni ya wazi.
Ni aibu Kwa Rais mzima aliyeapa kuilinda Katiba na Sheria za nchi, kuanza ujinga wa kampeni mapema. Je wenzako wafanye nini? Je na wao wafanye kampeni ya kuomba kuchaguliwa mwaka mmoja kabla ya uchaguzi?.
2. Inabidi utofautishe Ziara za kampeni na Ziara za kiserikali.
Wewe ni Rais wa Nchi, inabidi utofautishe kati ya Ziara ya kampeni na Ziara ya kiserikali. Hizi Ziara zako unazofanya huko Katavi na Rukwa ni Ziara za kiserikali, Kwa maana nyingine ni Ziara zinazo gharamiwa na Kodi za wananchi. Ni ujinga kutumia Kodi za wananchi kujipigia debe na kukipigia debe chama chako.
Nilishangaa sana ulipomlazimsha mbunge wa Nkasi kupitia CHADEMA mwanamama Aida Kenani kuanza na salamu ya CCM oye. Nikajiuliza hii ni Ziara ya Rais au Ziara ya chama Cha mapinduzi. Unamwambiaje mbunge aanze na salamu ya chama wakati ni Ziara ya kiserikali?. Ulipotoka sana.
Nikushauri tu, Kama unataka kujipigia debe basi anzisha Ziara za kichama na sio kutumia raslimali za Serikali na Kodi za wananchi kufanya makampeni yako ya kijinga. Yani utumie Magari ya Serikali na walinzi wa Serikali kujipigia kampeni? No please.
Pia soma: Kampeni za Uchaguzi 2025 zimeanza?
Nikushauri tu, hizi ni Ziara za kikazi zitumie kufanya kazi za Serikali , achana na huu ujinga unaoufanya wa kampeni, acha mara moja.
3. Tumia Ziara hizi kujibu maswali magumu ya watanzania.
Nikushauri ya kwamba kwa sababu upo kwenye Ziara ya kiserikali jaribu kutoa ufumbuzi kwa mambo yanayoendelea Tanzania. Jikite kwenye mambo ya msingi kama masuala ya utekaji, sukari, maji, mmonyoko wa maadili, malalamiko ya wafanyabiashara, ajira nk. Jikite huko na uongee na Raia na kusikiliza shida zao achana na vijembe havisaidii kwa Sasa watu Wana shida nyingi sana na hawaitaji vijembe vyako.
4. Mwisho punguza kauli za dharau na kiburi.
Unadai upinzani ni wachanga hawawezi kuongoza nchi. Nikuulize swali, mwaka 2015 CCM ilipata asilimia 57 ya Kura za Urais, Kwa maana nyingine wapinzani walipata asilimia 42, tofauti ya asilimia 15. Je hiyo tofauti ya asilimia 15% ni ya wachanga au wakubwa? Tena kwenye mfumo wa uchaguzi ambao unaifavour CCM.
Nijuzi tu hapa 2019, wagombea wa viti vya seriakali za mtaa wa upinzani waliondolewa kugombea kwa asilimia 80% mpaka wakaamua kususia uchaguzi wote na CCM kupata ushindi wa asilimia 95%.
Kama hiyo haitoshi, 2020 wagombea wa Ubunge wa vyama vya upinzani wakaondolewa tena kwenye kugombea Ubunge. Cha kusikitisha wengine wakiwa ni wabunge waliomaliza muda wao Kama mbunge Susan Kiwanga, aliondolewa kwenye kinyang'anyiro Cha Ubunge wakati alikuwa amehudumu kwa muda wa miaka mitano. Cha kusikitisha zaidi siku ya kupiga kura mtandao ukazimwa kwa wiki nzima, na ujinga mwingi kufanyika.
Nikuulize swali, je Kama upinzani ni wachanga kwanini mnatumia nguvu na mabavu kupambana nao. Yani wewe baba mzima wa miaka 60 unapigana na mtoto mchanga kwa kutumia rungu, huo sio utaahira?. Hivyo basi hakuna Cha mchanga Wala Mzee, kila kiongozi akiingia madarakani ataongozwa na Katiba iliyopo na sio umri wa miaka yake.
Niishie hapo
By Econonist.