Rais Samia: Mbowe alijificha Nairobi aliporudi akaanza harakati za madai ya Katiba, nadhani ni Calculation akijua kwamba ana kesi

Hapo mama kachemka kweli hao alioshitakiwa nao mbowe ambak wameshahukumiwa ni akina nani?
 

Mama anaelekea kukwama. Sasa kama hiz taarifa ameamu kuziweka ktk muktadha huu maelekezo hayo ni hakika

Kwa hiyo walio nnje kwasababu wao hawatafuti cover ya chochote je waendelee na madai ya katiba mpya?
 
Wewe toka povu kwa kuingia ktk mtego wa mbowe ila rais kaongea kama mtu ambaye ameshapewa intels zote na kaamua utawala wake usiwe chaka la mbowe...
 
Mama ogopa Mungu wako aliyekuumba .... tunaweza kukusahau kama vile yule mtemi - mtangulizi wako..aliyefikiri dunia yote ni yake...ogopa sana maombi ya watanzania...yana nguvu za ajabu.

Mbowe huyu mmemvunjia bilicanas - akakaa kimya
Mbowe huyu mkalima saba lake la mbogamboga kumkomoa - akakaa kimya
Mbowe huyu mkambambikizia kodi ya ajabu kwenye hotel yake - akakaa kimya
Mbowe huyu mkampa kesi ya kumuua Akwilina - akashinda kesi na akabakia kimya
Mbowe huyu mkamvunja mguu ili kumtisha aachane na siasa za upinzani - akakaa kimya
Mbowe huyu huyu mkamfungia account zake zote kwa miaka 3 na ushee - akakaà kimya
.
Sasa kama haitoshi leo wewe na wenzako mmeamua kumpa kabisa UGAIDI ili kunyamazisha...hamtaweza.

CCM muogopeni Mungu wako..kudai katiba ndiyo ugaidi...
Mungu atashughulika na ninyi wote na familia zenu..wala si muda mrefu atatoa majibu ya maombi yetu..cha msingi tusije kulaumiana.

Mungu wa mbinguni huwa hadhihakiawi kamwe
 

Kuna anaekataa kuwa Mbowe hakukimbilia Kenya?
Yaani mtu kwenda kupumzika wewe jinga unasema kakimbia?
Kwani Mbowe ni mara ya kwanza kwenda Kenya au nje ya nchi na mara zote hizo huwa anakimbia kesi?? Kwa ushirikiano uliopo kati ya Tz na Kenya mbona ni rahisi sana kumkamata gaidi au mtuhumiwa yeyote anayehitajika pindi awapo Kenya.
Ni akili za ajabu sana hizi.Tumieni ubongo kufiki na sio kiungo kingine.!!
 
Wakati baba yake Mbowe anadai uhuru wa nchi yetu hii baba za wengine walikuwa wanawapikia chai wakoloni.. ( chawa)

Leo wanageuka na kumwita ati Mbowe Gaidi ...
 
Kuna vitu ambavyo sisi tulioko huku chini hatuvijui na kamwe hatuwezi kuvijua,sema tu kuna mahala inahitajika busara kwa mamlaka zinazohusika kuamua the way forward ili maisha yaendelee kwa commitment ya muhusika /taasisi kutorudia tena.
 
Kuna vitu ambavyo sisi tulioko huku chini hatuvijui na kamwe hatuwezi kuvijua,sema tu kuna mahala inahitajika busara kwa mamlaka zinazohusika kuamua the way forward ili maisha yaendelee kwa commitment ya muhusika /taasisi kutorudia tena.
Maza kashachemka...be straight.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…