Ukisema siwezi kuonesha uthibitisho wala hauta kufa na si dhambi.
Kuhusu biblia, nakuonesha uhusiano uliopo kati ya vitabu vya kabla ya injili (agano la kale) na injili (agano jipya). Aya hizo hapo chini zinaoneshwa kutabiriwa kuzaliwa kwa Yesu na Manabii waliomtangulia. Hiyo inaonyesha uhusiano wenye nguvu sana wa agano la kale na agano jipya
| Angezaliwa na bikira, angeitwa Imanueli Isaya 7 : 14 | |
| Angezaliwa Bethlehemu Mika 5 : 2 | |
| Angeingia Yerusalemu kwa punda Zekaria 9 : 9 | |
| Utabiri wa Kuzaliwa kwake na sifa zake Isaya 9 : 6 - 7 | |
| Mesiya atakuwa Kiongozi na Mtawala Danieli 9 : 25 | |
| Angeteseka kwa ajili ya dhambi zetu Isaya 53 : 5 - 6 | |