Rais Samia: Mimi ni Mzanzibari

Rais Samia: Mimi ni Mzanzibari

..sikumbuki Nyerere kupanda jukwaani na kuzungumza Kizanaki na kutoa ujumbe mahsusi kwa Wazanaki wenzake.

..alichokuwa akifanya Nyerere ni kutolea mifano na vichekesho vya Kizanaki ktk mazungumzo yake. Na alikuwa akitafsiri kwa Kiswahili hapo hapo, on the spot.

..Nyerere alipozungumza Kizanaki aliwalenga watu wote, na alitoa tafsiri kwa Kiswahili.
Uko sahihi mkuu. Na ndicho alichofanya Samia . Hajautukuza u Zanzibari wake
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mapema leo amesema yeye hapendi Ukanda ila yeye ni "Mzanzibar!"

Kiukweli Rais kakosea sana kukemea ukabila huku yeye akitamka bayana ni wa mahali fulani.

Samia umekosea sana!
Hata Nyerere alikuwa anasema yeye ni Mzanaki na Magufuli alikuwa anaongea mpaka Kisukuma kwwnye majukwaa. Sasa tatizo liko wapi yeye akisema ni Mzanzibar. Wewe lengo lako ni kumfitinisha rais na Watanzania bara tu.
 
JF ongezeni moderators, inaweza kuwa ni ngumu kuwalipa ila pambaneni mpate wadhamini mpate fedha, Jukwaa lenu linashuka hadhi sana, sababu kubwa ni aina ya Mada zinazoanzishwa

Siku hizi Mlevi yeyote anaweza kuamka na kuja kumwaga pumba zake zinazomjia kichwani jukwaani.

Alichoongea Samia ni tofauti na alichoandika huyu jamaa, yeye kadokoa sentensi moja tu kaimwaga hapa, na wanaokomenti nao ni walewale tu
Acha kiherehere
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mapema leo amesema yeye hapendi Ukanda ila yeye ni "Mzanzibar!"

Kiukweli Rais kakosea sana kukemea ukabila huku yeye akitamka bayana ni wa mahali fulani.

Samia umekosea sana!

====

Samia Suluhu ninapotoka hatuna makabila. Kwetu kule Zanzibar tunajuana kwa maeneo...

Kwenye system ya makuzi – shule na siasa – tunamshukuru sana Baba wa Taifa Mwl. Nyerere. Kwahiyo, tunapofanya kazi hapa, na mimi binafsi, ninafanya kazi bila kuangalia kabila fulani. Sasa watu wakifanya makosa, “nimewajibishwa kwakuwa ni kabila Fulani”. Sina kabila. Mimi hapa ukiniuliza kabila lako nani nitakwambia ni Mzanzibari.
Threads zingine hazina hadhi ila unakuta umefungua tu, haina namna inabidi uisome.

Ila huu ni upuuzi haufai kuwa jukwaa hili
 
Haaa,kwa hiyo una record kwamba watu hawakuhoji,yaani kwa nini mnamtumia Magufuli kama standard,kwa hiyo kama Magu alikuwa anakosea basi na Samia naye akosee
Unapata wapi ujasiri wa kumkosoa ikiwa Maghufuli alikuwa yeye na Chato na kisukuma chake. Na hamkuhoji !!

Mwacheni Samia afanye yake. Na kwa katiba mbovu hii huna cha kumfanya, zaidi ya kunung'unika. Wapinzani wanapowaambia tushughulikieni katiba , eleweni
 
Mama alipaswa kusema yeye ni Mtanzania anayetokea Zanzibar.Lakini kujitanabaisha kuwa yeye ni Mzanzibari inaleta ukakasi fulani
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mapema leo amesema yeye hapendi Ukanda ila yeye ni "Mzanzibar!"

Kiukweli Rais kakosea sana kukemea ukabila huku yeye akitamka bayana ni wa mahali fulani.

Samia umekosea sana!

====

Samia Suluhu ninapotoka hatuna makabila. Kwetu kule Zanzibar tunajuana kwa maeneo...

Kwenye system ya makuzi – shule na siasa – tunamshukuru sana Baba wa Taifa Mwl. Nyerere. Kwahiyo, tunapofanya kazi hapa, na mimi binafsi, ninafanya kazi bila kuangalia kabila fulani. Sasa watu wakifanya makosa, “nimewajibishwa kwakuwa ni kabila Fulani”. Sina kabila. Mimi hapa ukiniuliza kabila lako nani nitakwambia ni Mzanzibari.
 
Anajichanganya Sana huyu maza
Anakuwa Kama bashite ambaye aliwakusanya waandishi wa habari kuwataarifu kwamba wawaelimishe wananchi waepuke mikusanyiko ili kujikinga na uviko

Bashite alikua na vituko sana yule jamaa
 
Na sisi Wenyeji wa Tanga tulio sababisha kuzaliwa kwa jina la nchi yetu ya Tanganyika, tunaruhusiwa kutembea vifua mbele kama kuku walio nyonyolewa?
Waliosababisha nchi yetu kuitwa Tanganyika ni Wafipa kutokana na Ziwa Tanganyika. Na huko Katavi kuna wilaya inaitwa Tanganyika.
 
Watatambuana vipi kwa makabila hali ya kua wengi wao wahamiaji? Mabaki ya utumwa na arab
 
Mataga na CHADEMA mwacheni Rais Samia mbona aliyetangulia alikuwa anazungumza Kisukuma, Ikulu ikahamia Usukumani, Madc Wasukuma, Wakurugenzi Wasukuma, Mawaziri Wasukuma,Ma-Ras na Das na wateule Wasukuma, mlikaa kimya?
 
Back
Top Bottom