Rais Samia: Mimi ni Mzanzibari

Rais Samia: Mimi ni Mzanzibari

Mama plz usianzishe vita na wasukuma wale watu wametubeba sana CCM 2015 na 2020.
Kama ukumpenda mtangulizi wako usichukie na jamii yako yote. Lile kundi likisimama na wapinzani tutapata shida.
Acha uongo wewe.

Hakuna msukuma ana time na hayo mambo zenu wala raisi Samia hana ugomvi na wasukuma,wewe ndie unautengeneza huo ugomvi.
 
Tumeona mama akiwaondoa wazalendo wenye Phd na kuweka watu wenye kutiliwa mashaka na umma kama wajuzi wa kupiga hela ya umma. Tanesco wamewekwa wafanya biashara wakubwa kwenye bodi na waziri mpya kwa kazi gani? Huko nyuma tumeona wafanyabiashara binafsi wakifilisi mashirika ya umma kwa maslahi yao.

Sekta ya umma tangu lini imeonyesha mafanikio kwa kuwekwa wafanyabiashara kwenye management na body ya wakurugenzi? Kama inafanyika kwingine uzoefu kwa tanzania ni kwamba unawapa ulaji na kulifilisi shirika.

Kuhusu wizara ya nishati wengi tumeona ni upendeleo umetumika kwa lengo hasi kwa maslahi ya nchi. Aliyewekwa wala hana uwezo kama aliyeondolewa.
Acha uongo.
 
Kwani wale waliopendekeza uwepo mfumo wa vyama vingi walikuwa wangapi ukilingganisha na wale waliokataa?
Hiyo ina husu vipi? Si yalikua maamuzi ya mwalimu? Ngoja nikuambie huku mitandaona kuna hata ghost people na wengi wana post hata hawa maanishi wanacho andika na wengine wetu ni walevi tu
 
..sukuma gang wanamtuhumu kuwachomoa ktk nafasi mbalimbali.
Hahaha, hilo linajulikana, Ila sukuma gang wengi walibebwa bebwa, sasa Mama afanyaje? Na ameshasema yeye anaangalia weledi wa mtu!! Sukuma gang pekee naweza sema JPM katuachia kama legacy yake ya kuteua ni Mabeyo, jamaa ni the best of the best
 
Ingekuwa hivyo kama kura zingekuwa zinapigwa chini ya tume huru. System ndio inaamua nani akae wapi.
Mama plz usianzishe vita na wasukuma wale watu wametubeba sana CCM 2015 na 2020.
Kama ukumpenda mtangulizi wako usichukie na jamii yako yote. Lile kundi likisimama na wapinzani tutapata shida.
 
Mzanzibar mwenye asili ya chato. 😜😜😜

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mapema leo amesema yeye hapendi Ukanda ila yeye ni "Mzanzibar!"

Kiukweli Rais kakosea sana kukemea ukabila huku yeye akitamka bayana ni wa mahali fulani.

Samia umekosea sana!

====


Samia Suluhu ninapotoka hatuna makabila. Kwetu kule Zanzibar tunajuana kwa maeneo...

Kwenye system ya makuzi – shule na siasa – tunamshukuru sana Baba wa Taifa Mwl. Nyerere. Kwahiyo, tunapofanya kazi hapa, na mimi binafsi, ninafanya kazi bila kuangalia kabila fulani.

Sasa watu wakifanya makosa, “nimewajibishwa kwakuwa ni kabila Fulani”. Sina kabila. Mimi hapa ukiniuliza kabila lako nani nitakwambia ni Mzanzibari.
 
Naona mumeamua ku PICK bahadhi ya sentence sio all context

Watanzania wasas kweli vituko!
 
Kama yeye ni Mzanzibari,kuna wengine ni wazazi baa na wadanga nyika
 
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mapema leo amesema yeye hapendi Ukanda ila yeye ni "Mzanzibar!"

Kiukweli Rais kakosea sana kukemea ukabila huku yeye akitamka bayana ni wa mahali fulani.

Samia umekosea sana!

====


Samia Suluhu ninapotoka hatuna makabila. Kwetu kule Zanzibar tunajuana kwa maeneo...

Kwenye system ya makuzi – shule na siasa – tunamshukuru sana Baba wa Taifa Mwl. Nyerere. Kwahiyo, tunapofanya kazi hapa, na mimi binafsi, ninafanya kazi bila kuangalia kabila fulani.

Sasa watu wakifanya makosa, “nimewajibishwa kwakuwa ni kabila Fulani”. Sina kabila. Mimi hapa ukiniuliza kabila lako nani nitakwambia ni Mzanzibari.
Kusema yeye ni Mzanzibari tayari ni ukabila au ukanda ni bora angesema mimi ni Mtanzania Visiwani/Zanzibari.

Kila Mtanzania ana kabila la asili ambalo linasaidia kufahamu na kutambulisha mila na desturi pamoja kwa yakini uraia wa mtu hata huko Zanzibari kuna Wakoja, Wangazija, Wamakunduchi, Wamvita, Watangana, Wakilindini, Wabarawa, Wakiamu, Wapokomo, Wapemba, Wakivanga, Wakiriama, Wakiduruma, Wakijibana nk.

Kuna makabila zamani nchini Tanzania yalikuwa yakwepwa kupewa nafasi za uongozi ngazi za juu kwenye utumishi wa umma na serikali kwa hofu ya uwiano wao kuhitaji wawe wengi ili kuridhika kwamba ni sehemu ya ujenzi wa taifa. Kuna baadhi ya makabila tangu yalisikika yenyewe tu ikidaiwa kwamba wamesome sana ndio maana walipewa nafasi za uongozi wakati sio kweli.

Ukichukuwa kwa mfano Wanyakyusa walioko wilaya za Rungwe na Kyela mkoani Mbeya, Wasukuma walioko mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Geita, Tabora na Simiyu kwa kipindi kirefu hawakuwa washirika wakubwa wa kiuongozi wa juu sio kwamba hakuna aliyesoma au uwezo ila ni hofu ya uwingi wao kumeza nafasi za wengine kitu ambacho pia sio kweli.

Taifa linatakiwa likwepe sana dhana ya kutoa uongozi kwa mtu kwa taswira ya UDINI, UKABILA, UKANDA na ITIKADI za chama cha SIASA kudhibiti mawazo mbadala yenye kuleta tija kwa Taifa la Tanzania (Bara & Visiwani).

Zamani kabla na wakati wa ukoloni kulikuwa na tawala zenye nguvu sana zikijulikana kama
1. Meruland
2. Chaggaland
3. Pwaniland iliyoanzia Somalia, Kenya, Tanganyika, Zanzibar, Comoro hadi Sofala Msumbiji,
4. Sukumaland
5. Songealand
6. Nk

Enzi za Mwalimu Nyerere wilaya ya Mwanga huko Kilimanjaro chini ya waziri wa fedha na baadae akawa waziri mkuu ndio iliyoonekana kuwa na maendeleo makubwa ya miundo mbinu za barabara za lami, maji na umeme huku wila jirani yake ya Same ikiwa baki kuwa hoi katika nyanja zote; leo hii wilaya hiyo rasilimali zote zimechakaa hakuna wakuziendeleza huku wilaya iliyokuwa nyuma kimaendeleo ya Same iking'ara kwa miundo mbinu ya aina zote mpaka wazekezaji wanavutiwa kuwekeza huko (suala ni mipango inatakiwa iwe ni endelevu hata aliyekuwa ameanzisha akiondoka anayekuja anatakiwa kuendeleza kwa faida ya wananchi sio kuendekeza ukomoaji kwa visingizio vyovyote vile.

Maumbile ya kijiografia ya uliokuwa mkoa wa Shinyanga yafanana na jinsi ulivyo mkoa wa Morogoro kwa sasa ambapo unakuta wilaya moja iko mbali karibia kilomita 300. Shinyanga iligawanywa kutokana na ongezeko la watu hivyo mahitaji ya kiutawala kuongeza kuwa karibu zaidi wakati Morogoro kwa wilaya za Mahenge na Malinyi umbali unawatesa sana wananchi kupata huduma stahiki kwa wakati. Laiti kama kungekuwa na uwezekano wa wilaya hizo kuhamishiwa Iringa ambapo ni kati ya kilomita 140-150km wangehama zamani maana ni karibu kwao.

Kuiita Uzanzibari, Uunguja, Upemba au Utanganyika ni ubaguzi ambao mwisho wake wengi wakikasirika wachache wanaweza kuja kupata shida sana huko mbeleni.

Kwa mfano Watanzania Zanzibar wa Pemba ya kasikazini wanamanung'uniko ya kutothaminiwa na kubaguliwa kwamba wana nasaba na waaarabu wa kishirazi; siku wakipata madaraka ya kuongoza nchi taifa litagawika vipande kadhaa hatarishi kwa umoja wa kitaifa.

Kwa sasa kuna chuki inayoenezwa na baadhi ya Watanzania wenye chuki binafsi dhidi ya JPM kwamba alipendelea wasukuma, alikuwa hashauriki, alikuwa dikteta (kila mmoja ni dikteta kwa nafasi ya dhamana aliyokabidhiwa kuisimamia ili atekeleze kile alichoagizwa na wananchi afanye) hoja ambayo haina ushahidi thabiti ukilinganisha na wingi wao nchini. Watu wanathubutu kumtupia lawama zote bila mamlaka ya nchi kukemea kitu kinachotengeza chuki nyingine dhidi ya nyingine ndani ya chumba kile kile. Siku wakiacha kusemeshana wenyewe ndani wananchi watakipata cha mtema kuni.

Kwa muda mrefu utamaduni wa kila mtumishi kuwajibika kutumikia wananchi kwa ufanisi uliachwa kusimamiwa kwa kisingizio cha demokrasia hivyo kupelekea kila mmoja hasa wasio na maadili mema kutumia nafasi hizo kujinufaisha wenyewe huku wakiwadharau raia waliowapa kazi na kuwalipia mishahara yao kupitia tozo, kodi na michango lukuki bila manung'uniko yoyote.

Viongozi wa nchi acheni kuongoza au kutawala kwa kuelemea UDINI, UKABILA, UKANDA, RANGI ya mtu na ITIKADI Kinzani yenye tija.

Viongozi msitumie vitisho mnapokosolewa kwa kuwa ndio kioo chenu kujirekebisha ili kufanya vema zaidi (dhana ya KUKOSOA na KUKOSOLEWA) ifanye kazi kwa vitendo bila kuangalia nafasi ya mtu mkubwa akubali kukosolewa kama yeye anavyokosowa kwa wanaofanya kinyume na matarajio yake kwa niaba ya wananchi.

Wananchi ndio waajiri wa watumishi wa umma na serikali hivyo kujirekebisha kutokana na kukosolewa huongeza imani, heshima na kutahaminiwa nao.
 
Hata Nyerere alikuwa anasema yeye ni Mzanaki na Magufuli alikuwa anaongea mpaka Kisukuma kwwnye majukwaa. Sasa tatizo liko wapi yeye akisema ni Mzanzibar. Wewe lengo lako ni kumfitinisha rais na Watanzania bara tu.
Angejitambulisha kwamba yeye ni Mkojani au Mnungwi isingekuwa na tatizo lolote. Ni sawa na ilivyokuwa haina tatizo kwa JPM alivyokuwa akijitambulisha kwamba alikuwa Msukuma. Pamoja na kwamba tulikuwa tunafahamu kwamba JPM alikuwa Mtanganyika, lakini ingeleta kero sana kama kwa siku yoyote angejitambulisha kwamba alikuwa Mtanganyika. Hata Samia kwa kujitambulisha kwamba yeye ni Mzanzibar kakosea na nadhani haina afya kwa taifa. Kujitambulisha kwa kutumia utaifa wetu wa zamani ambao kimsingi ulishakufa siyo vyema sana.
 
Back
Top Bottom