Rais Samia: Msikubali wanaotaka kuanzisha chokochoko, pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani

Rais Samia: Msikubali wanaotaka kuanzisha chokochoko, pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais Samia amewataka wananchi wa Morogoro wasikubali chokochoko zinazoanzishwa na baadhi ya watu.

Amesema hao wanaotaka kuanzisha vurugu wameshaandaa na wanajua watakavyojitibia ikitokea wamepata madhara.

Amewataka wananchi kutokubali na kutunza amani iliyopo. Amesema hayo akiwa Morogoro kwa ziara ya siku mbili.

NB: Possibly Rais anawaasa wanaotaka katiba mpya.

===

Rais Samia: Niwaombe sana tulinde amani, vijichokochoko vimeanza naomba msivipokee, wanaokuja na vijichokochoko walishajua matumbo yao yanajaaje, chakula chao wanatoa wapi, pesa za matibabu watatoa wapi, nawaomba wasije wakawaingiza kwenye huo mkenge”

Rais Samia:
“Pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani na Watoto wako na Mama Watoto na msijue chakula mnatoa wapi, msijue Mtoto akiumwa mtakwenda kumtibu na pesa gani, niwaombe sana tulinde amani yetu, Nchi yetu itulie tuendelee na maendeleo yetu
 
Dawa ni kufuata sheria ili kuepuka hizo chokochoko, ila mkiwaumiza wanaoleta chokochoko wanaofuata sheria ili kudai haki zao mnawaonea, tumieni madaraka yenu vizuri kwa kuheshimu haki za wengine.
 
Dawa ni kufuata sheria ili kuepuka hizo chokochoko, ila mkiwaumiza wanaoleta chokochoko wanaofuata sheria ili kudai haki zao mnawaonea, tumieni madaraka yenu vizuri kwa kuheshimu haki za wengine.
Chokochoko ziwe za kisheria au za kihuni zote zinaleta taharuki na kama mnavyojua huyu mnyama “taharuki” ambavyo hakubaliki na serikali ya JMTz!
 
Back
Top Bottom