Rais Samia: Msikubali wanaotaka kuanzisha chokochoko, pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani

Rais Samia: Msikubali wanaotaka kuanzisha chokochoko, pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani

NB: Possibly Rais anawaasa wanaotaka katiba mpya.
Inakuwaje achanganye ya "Katiba Mpya", na huko "Kujiandaa kujitibia"?

Ina maana yeye Rais sasa, anakwenda kuwatia uoga wananchi wasidai katiba mpya (kufanya chokochoko) kwa vile hawajajiandaa watakavyotibu (majeraha)? watakayopata wakati wakidai haki hiyo?

Mbona haileti mantiki?
 
Rais Samia amewataka wananchi wa Morogoro wasikubali chokochoko zinazoanzishwa na baadhi ya watu.

Amesema hao wanaotaka kuanzisha vurugu wameshaandaa na wanajua watakavyojitibia ikitokea wamepata madhara.

Amewataka wananchi kutokubali na kutunza amani iliyopo. Amesema hayo akiwa Morogoro kwa ziara ya siku mbili.

NB: Possibly Rais anawaasa wanaotaka katiba mpya.


Yule aliepanga kumnyoa mama na wembe ajiandae yeye sasa kunyolewa na chupa. Najua mwenyekiti wake aliemtuma muda huo atakuwa Dubai au South Africa kwa kisingizio cha kuchek afya yake.
 
Tutafuatilia mapema kabisa, tangu muunda wazo tu la kuvuruga hii amani, tutakula naye sahani moja, mbona ni jambo dooogo kabisa!! hatutaki ujinga sisi

Demokrasia ni starehe ya Ulaya na American huko
 
Wimbi la KATIBA Halizuiliki

Kuzulumatism wanachama NSSF ni matokeo ya katiba tuliyonayo

Kwa hisani ya Mutu ya MAREKANI

eti Mabeberu ....
 
Back
Top Bottom