Rais Samia mteue Dkt. Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa Fedha na Mipango

Hapana, kwenye u smart Dkt Ashatu ni genius! Ana kipaji cha akili! Fuatilia historia yake enzi anasoma IDM Mzumbe au wakati anasoma
PhD yake nchini Norway.
Kumbe unamjua na ulisema humjui. Anyway mie pia nampenda Dr. Ashatu ila wewe ni CHAWA
 
Kama ni usomi anaweza mzidi Mwigulu kweli?

Ni msomi ndio ila hawezi na hajui kujieleza kwa hiyo hata changamoto kama hizi za Uchumi hajui kuongea.

Nimemuona mara nyingi kwenye mikutano ya Ziara za Rais ameahindwa kutolea maelezo ya mambo ya kupanda Kwa bei za vitu na yeye ndio mhusika kwenye hiyo wizara ya viwanda na Biashara..

Pamoja na Chuki zenu sijamuona Waziri wa Fedha wa kumzidi Mwigulu kwa sasa hata yule Mchaga ndio kabisaa ataishia kupaniki na kujing'ata ulimi bure..

Hizo nafasi nyeti zinahaitaji uwe na uwezo wa kujieleza ambao Mwigulu anao na mara nyingi ametoka kutetea sera zake..

Mwisho uchumi unapimwa Kwa matokeo sio blaa blaa blaa zenu.
Dkt Ashatu uwezo wa kujieleza anao, tena she is an inspirational person. Sema humjui vizuri tu. Dkt Ashatu ana uwezo mkubwa sana wa kuchambua mambo.
 
Huko tuu kwenye biashara naona kafeli,ujue kuna watu Bora wawe walimu tuu sio kazi kama hizo..

Mara elfu Mwigulu kuliko huyo mmama hajui kabisa kujieleza.

Exaclty, Ashatu ni zero result oriented naweza sema hivyo..

Wako Mawaziri wanapiga kazi hadi basi mfano, Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Fedha, Dr. Mwigulu, au waziri wa Maji, Aweso, ila Ashatu mm katika Mawaziri nampa nafasi ya mwishooo kabisa, wizara yake tu imemlemea sana
 
Kumbe unamjua na ulisema humjui. Anyway mie pia nampenda Dr. Ashatu ila wewe ni CHAWA
Mbona kwenye CV yake hivyo vitu vipo tu jamani na uki google unapata kila kitu
 
Dkt Ashatu uwezo wa kujieleza anao, tena she is an inspirational person. Sema humjui vizuri tu. Dkt Ashatu ana uwezo mkubwa sana wa kuchambua mambo.
Nimekuelewa hapo kwamba mara nyingi tuu nimemuona kwenye mikutano ya Rais akijiuma uma..

Kuwa intelligent ni kitu kingine na isitoshe amewahi kuwa Waziri Naibu Waziri wa Fedha..

Hana huo uwezo wa kujieleza kudefend mazingira ya siasa na weledi kwa pamoja kumzidi Mwigulu..

Unadhani wanaomteua Mwigulu toka zama za Kikwete ni Wajinga?
 
Exaclty, Ashatu ni zero result oriented naweza sema hivyo..

Wako Mawaziri wanapiga kazi hadi basi mfano, Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Fedha, Dr. Mwigulu, au waziri wa Maji, Aweso, ila Ashatu mm katika Mawaziri nampa nafasi ya mwishooo kabisa, wizara yake tu imemlemea sana
😬😬 Bila kusahau Mwamba Bashe na Naibu wake 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220724-092729.png
    Screenshot_20220724-092729.png
    117.6 KB · Views: 5
Kiufupi Wizara ya Viwanda na Biashara Rais amteue Yule Mwarabu wa Gairo sio Hawa wasomi..

Huyu Dr.Kijaji arudi darasani kufundisha ndio kunamfaa..
 
Nimekuelewa hapo kwamba mara nyingi tuu nimemuona kwenye mikutano ya Rais akijiuma uma..

Kuwa intelligent ni kitu kingine na isitoshe amewahi kuwa Waziri Naibu Waziri wa Fedha..

Hana huo uwezo wa kujieleza kudefend mazingira ya siasa na weledi kwa pamoja kumzidi Mwigulu..

Unadhani wanaomteua Mwigulu toka zama za Kikwete ni Wajinga?
Nadhani Rais Samia anahitaji mtu sahihi kwa wakati sahihi ili amsaidie kuiongoza vema wizara ya fedha. Dkt Ashatu ni muadilifu na mchapa kazi, ni mzalendo na ni uhakika Mama atapa ushauri sahihi. Ktk kipindi alichokaa wizara ya Fedha na Mipango kama naibu waziri, tuliona kabisa alivyofanya kazi vizuri na Makamu wa rais Dkt Mpango, tunaamini hata sasa hii mifumuko ya bei isingekuwepo kama Dkt Ashatu angekuwa waziri wa Fedha na Mipango. Ndiyo Maana tunaomba Rais Samia amteue ili kubalance mambo na kurudisha imani kwa wapiga kura.
 
Kiufupi Wizara ya Viwanda na Biashara Rais amteue Yule Mwarabu wa Gairo sio Hawa wasomi..

Huyu Dr.Kijaji arudi darasani kufundisha ndio kunamfaa..
Bila wizara ya Fedha na Mipango kufanya vema basi wizara zote hamna kitu. Dkt Ashatu anafaa kuwa waziri wa Fedha na Mipango ili kuimarisha uchumi
 
Hata angeteuliwa mchumi aliyeshinda tuzo ya Nobel asingeweza kwa sababu nchi bado ina mfumo mbovu wa Ujamaa. Ujamaa ndiyo unatukwamisha.
Siyo kweli.china ni nchi ya ujamaa.haifanyi vizuri kuwa among G7?
 
Nadhani Rais Samia anahitaji mtu sahihi kwa wakati sahihi ili amsaidie kuiongoza vema wizara ya fedha. Dkt Ashatu ni muadilifu na mchapa kazi, ni mzalendo na ni uhakika Mama atapa ushauri sahihi. Ktk kipindi alichokaa wizara ya Fedha na Mipango kama naibu waziri, tuliona kabisa alivyofanya kazi vizuri na Makamu wa rais Dkt Mpango, tunaamini hata sasa hii mifumuko ya bei isingekuwepo kama Dkt Ashatu angekuwa waziri wa Fedha na Mipango. Ndiyo Maana tunaomba Rais Samia amteue ili kubalance mambo na kurudisha imani kwa wapiga kura.
Acha utoto Mzee ,VP ni mshauri namba moja wa Uchumi wa Rais pamoja na Mwigulu na huyo huyo Dr.Kijaji sasa unaposema mifumuko isingekuwepo kwani hawapo sasa hivi?

Unaweza zuia mfumuko wa Bei ikiwa bidhaa ni chache?
 
Jamal, Malima, na Kibona walikuwepo in the past 20 years? Mgimwa naye ndio hivyo bahati mbaya.
Nakupa historia ya wizara

Hiyo 20 years kuna Mramba, Mkullo,, Sada Mkuya na Dr Mpango!

Chagua mwenyewe hapo!
 
Bila wizara ya Fedha na Mipango kufanya vema basi wizara zote hamna kitu. Dkt Ashatu anafaa kuwa waziri wa Fedha na Mipango ili kuimarisha uchumi
Hamna kitu kivipi ikiwa Kazi ya Wizara ya fedha ni kufikosha pesa na kuweka sera za Uchumi..

Huyo Kijaji amefanya nini cha maana huko Wizara ya Viwanda na Biashara?
 
Back
Top Bottom