Rais Samia mteue Dkt. Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa Fedha na Mipango

Tunasema mnapotosha kwa sababu kipindi Dkt Magufuli yupo alizuia mfumuko wa bei. Na angekuwepo pasingekuwepo mfumuko wa bei.
 
Sema wewe unamtaka sio watanzania
 
Nilikuwa nafikiri kateuliwa kumbe ni porojo za mwandishi.
 
Tunasema mnapotosha kwa sababu kipindi Dkt Magufuli yupo alizuia mfumuko wa bei. Na angekuwepo pasingekuwepo mfumuko wa bei.
Sijui kwanini watu ni degree holder lakini mnakuwa wajinga. Magufuli angezuia vita na kufanya normal supply ya bidhaa duniani? Magufuli kafungua mashamba mangapi ya ngano? Magufuli angechimba mafuta kule Chato? Hebu google neno moja tu fuel crisis uone dunia inaongea kitu gani kwa sasa. Na bahati mbaya, hii crisis ni zaidi ya ile ya 1973-74 ambapo crisis ilikuwa kwenye petrol tu lakini hii ya sasa ni energy kwa ujumla wake plus food. So, wacheni malalamiko.
 
Amekutuma??? maana naona siku hz imeshakuwa style kila mtu akitaka uteuzi lazima amtume chawa wake aje kumuwekea andiko la kumpigia debe hapa.
Umeona eeh,wameshajua mama huwa anapitapita humu kuchungulia comments...
 
Kwa hiyo na mapinduzi ya ufaransa na marekani ni ujamaa Ila we jamaa jua kutofautisha Kati ya mapinduzi na ujamaa mapinduzi yana weza kufanywa na watu wa aina yoyote ile wabepari au hata wajamaa . Mapinduzi hayana mahusiano na falsafa za kijamaa. Nimekwisha kuambia CCM sio chama Cha kijamaa wewe endelea kung'ang'aniza vitu . Ili tu matatizo ya CCM uutupie lawama ujamaa . Ujamaa katika ardhi ya Tanzania ulizikwa 1985 toka hapo mpaka Sasa ujamaa unao uzungumzia wewe haupo hapa .
 
Tunasema mnapotosha kwa sababu kipindi Dkt Magufuli yupo alizuia mfumuko wa bei. Na angekuwepo pasingekuwepo mfumuko wa bei.
December 2015 Sukari Kilo moja ilikuwa Tsh 1,800/= then ika shoot hadi Tsh 5,000 na hadi anakufa nadhani haijawahi kuteremka chini ya Tsh 3,000.

Ila mnamsifia yule DIKTETA wa Chato sijui huwa mnapeleka wapi akili zenu.
 
Unamfahamu vizuri au unabwabwaja tu, wizara aliyopo yenyewe imemshinda hajui hata anafanya nini, eti wizara ya Fedha? ur not serious! Kinachombeba ni dni yake km hujui.
 
Huyo Dr. ameanzisha biashara gani na amefanikiwa kwa kiasi gani katika biashara zake?
Kama hajawahi kuanzisha biashara yoyote au kuendesha biashara yoyote anawezaje kutoa mwongozo sahihi wa jambo ambalo hajawahi kulifanya?, Hasa kutoa ushauri sahihi wa kuendesha biashara na uchumi?
NB
Mtu mwenye utaalamu wa uchumi kupitia vitabu tu, huenda akawa hajui lolote kuhusiana na changamoto za kibiashara katika mazingira halisi( zaidi ya nadharia za vitabuni tu).
 
Uzi mzuri sana ila unazijua.. Tunguri za madelu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…