Kumekuwapo maonyo mengi tangia ugonjwa huu ulipoingia. Ni wazi kuwa kutokana na kauli mkanganyiko zilizokuwapo katika nyakati mbali mbali hali halisi ndiyo hii inayoonekana leo.
Ugonjwa uliopaswa kushughulikiwa na wataalamu wa afya ukawa wa kushughulikiwa na wanasiasa. Matokeo yake miongoni mwetu wangalipo wasioamini hata uwepo tu wa ugonjwa huu duniani.
Hivi sasa dunia inakabiliwa na wimbi la tatu ambalo ni baya zaidi:
www.mwananchi.co.tz
Hawatakuja manabii kutoka mbinguni kutuletea jumbe maalumu za kutuasa kutoka kwake mola. Tunaposikia wenzetu wakinyolewa kama hivyo, ndiyo jumbe zetu hizo.
Awamu ya tano walionywa sana hadi kufikia huku:
www.jamiiforums.com
Kumbuka kikulacho ki nguoni mwako. Waliokuwa wakipinga naye uwepo wa Corona, leo hii kimya kimya barakoa haziwabanduki nyusoni.
Kauli yako italiokoa taifa hili. Wakati chelewa yako (nasikitika kusema) hali ikija kuwa mbaya utawala wako utakuwa njia panda.
Walio mstari wa mbele leo na vi propaganda uchwara vya kukushinikiiza kutokuuzingatia ushauri uliopewa na watalaamu uliowateua, watakuwa vinara wa kukunanga mambo yatakapo haribika.
Kinga ni bora zaidi kuliko tiba. Ni heri ukosee ukichukua tahadhari kuliko kubweteka.
Hili sasa ni lako wewe kama mkuu wa nchi.
Ninawasilisha.
Ugonjwa uliopaswa kushughulikiwa na wataalamu wa afya ukawa wa kushughulikiwa na wanasiasa. Matokeo yake miongoni mwetu wangalipo wasioamini hata uwepo tu wa ugonjwa huu duniani.
Hivi sasa dunia inakabiliwa na wimbi la tatu ambalo ni baya zaidi:
Watu 126 wafariki dunia kwa corona nchini Uganda ndani ya siku nne
Wizara ya Afya nchini Uganda imesema watu 126 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona katika kipindi cha siku nne.
Hawatakuja manabii kutoka mbinguni kutuletea jumbe maalumu za kutuasa kutoka kwake mola. Tunaposikia wenzetu wakinyolewa kama hivyo, ndiyo jumbe zetu hizo.
Awamu ya tano walionywa sana hadi kufikia huku:
Rais Magufuli kuhusiana na Corona bora ukachukua hatua bila kuchelewa zaidi unauweka uongozi wako njia panda
MODs natumaini mtaunusuru uzi huu kumwangazia mheshimiwa rais hali ilivyo, ili naye, aweze: 1. Kujinusuru mwenyewe kuweza kuendelea kuongoza kama kazi hiyo anaipenda. 2. Kuyanusuru maisha ya watu wake wasio na hatia kwa maana ndiyo kazi kuu tuliyompa kama rais wetu. 3. Kulinusuru taifa ili...