kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
Leo, Rais Samia Suluhu Hassan ameshiriki kilele cha matembezi maalum ya UVCCM ya kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi Zanzibar ambapo katika sehemu ya hotuba yake amewasisitiza vijana wa UVCCM kuachana na siasa za kuchokozana na ugomvi na hata ikitokea watakosolewa basi wajibu kwa hoja.
"Zama za ugomvi, kupigana na kutukanana katika siasa sasa ziishe, twendeni na hoja za maana, twendeni na hoja za kujenga. Tuvumiliane tulete maendeleo ya kweli na yenye tija, ili tujenge Tanzania yenye maendeleo endelevu."- Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan
Aidha alisema kwa kuwa ameruhusu mikutano ya hadhara vyama vingine vitakaposimama na kuikosoa serikali basi wawe wasikivu wa nini kinasemwa ili kirekebishwe kwa maslahi ya Taifa.
"Tunapokosolewa tuyaangalie, yale ya kweli tuyachukue tuyafanyie kazi makosa yawe yameondoka. Yale ambayo sio ya kweli twendeni tukajibu kwa hoja lakini kubwa ni ustahamilivu."- Rais Samia Suluhu