Rais Samia: Muda wa siasa za uhasama umekwisha

Kwa dhamira yake hii njema, Rais Samia, atabarikiwa na bila shaka atafanikiwa. Jamabo jema ni kwamba kama uongozi wake utafanikiwa, yatakuwa mafanikio ya Taifa.

Kama kuna nchi, siasa za ushindani humaanisha uhasama, siyo lazima sisi kuziiga hizo. Twende na kile tumachokiona ni chema, ili na wengine siku moja waje wajifunze kwetu.
 
Upinzani au ushindani ubaki kuwa utani wa jadi kama simba na yanga bila kupigana,hata yanga na simba enzi za kale tulishuhudia ugomvi mkubwa wa kutoana ngeo, ustaarabu umeingia umebaki kuwa utani wa jadi, pia CDM na CCM ibaki kuwa hivyo upendo, utani na kukosoana kwa minajili ya maendeleo. Fullstop. Mama kaelewa. Falsafa safi.
 
CCM ya Mwendazake hawataki siasa za amani, wamesikitishwa saana na hatua ya Mwenyekiti wetu Taifa kusema sasa yatosha - hawana uhakika kama watatoboa majukwaani maana wengi walisaidiwa kupita majimboni bila kupingwa, kuiba kura nk.
 
Atwambie muda upi ulikuwa wa siasa uhasama
 
Kumbe kulikuwa na siasa kipindi Cha J.P.M Mbona mlitwambia haliwazuia
Hizo ndiyo siasa za uhasama ndugu yangu,Mkurugenzi nimekuajiri,gari nmekupa mimi,mshahara nakulipa mimi halafu Mpinzani ashinde utakuwa huna kazi,"Mkichagua mpinzani jueni kwenu sileti maendeleo","Wapinzani walichewesha sana Maendeleo" hizo ni kauli za mwendazake kwa vipindi tofauti.
 
Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako.
 
Rais Samia Suluhu namuelewa sana hata ushauri wake anaotoa anaongea kama mama pia kama Rais wale waliozoea mambo ya kutumia nguvu bila kuelimishana hawatamuelewa
 
Hao uvccm hoja watolee wapi mana wote wana akili za kushikiwa
Haya ni mabadiliko na usikalili mzee huu ni utawala wa Rais Samia Suluhu na siasa zitakazofanywa kipindi hiki ni siasa za kistaarabu sio mlizozizoea
 
Exactly Rais Samia Suluhu lazima afanikiwe na ameshafanikiwa kutuweka pamoja na sasa kwa pamoja tunaelekea kwenye ujenzi wa Tanzania mpya
 
SAWA MAMA Mtangulizi wako ALIZIPENDA SANA HIZO SIASA MUNGU akupe Afya njema na Busara ili UTUPATIE KATIBA MPYA
Siasa za uhasama mlizianzisha nyie chadema sema hamkujua uvumilivu wa kiongozi mmoja mmoja, kikwete alikuwa mvumilivu lkn ikawa tofauti Kwa magufuli, so revenge ya magufuli ilikuwa doubled ndo mana mkamuona yeye kama mshari Ila wachokozi mlikuwa nyinyi.
 
Dah!
Wewe ni bonge ya chawa.
Nafikiri unayo PhD kwenye uchawa🤔
 
Safi sana mama umesema vitu makini mnooo
 
Matusi ndio silaha yao ! Ngoja tuone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…