Rais Samia muondoe ofisini haraka huyu jamaa wa EWURA

Polisi kwenye uchaguzi ujao,wawaambie chama tawala kuwa wao hawajihusishi na siasa.Ngoma ibaki kwao na upinzani,tuone itakuaje.
Na hawa ndio wanaotuangusha siku zote
 
Ishu ya mafuta juu ni Dili la Ewura na waagiza mafuta.
Ishu ya uhaba wa dollar ni kichaka tu.
Mrusi hataki kuuza mafuta kwa dollar.
Dhahabu ndio strong currency apewe dhahabu atupe mafuta.
 
Ni haki yako kuamini hivyo mkuu. Mimi sikubaliani na wazo hilo kamwe.
Makamba hana umaarufu wowote, na hata baba yake hana 'influence' popote, achia huko kwenye chama chenyewe, kiasi kwamba rais wa nchi ashindwe kufanya jambo analotaka kufanya kwa kuwagwaya hawa watu.

Hii fikra sijui mnaiokota wapi?
Mi nadhani ni namna yenu ya kummwondolea lawama mhusika mwenyewe, ambaye ni Samia, kwa sababu mnazozijua wenyewe.
 
Huyu si shemeji kwa kipaza sauti pale Idodomia
 
Get to know this, Samia kama Samia anapangiwa ya kufanya. Ila Rais Samia hapangiwi .


Labda utaelewa hapo.
 
Mtu na mkewe wote wana uwezo mdogo wakufikiri na nashangangaa wamepewa madaraka makubwa? Sasa je kama hawa ndio viongozi wanaoongoza wananchi ikiwa uwezo wao ndio huu je wananchi wenyewe uwezo wao ukoje??

"Mzungu"
Ukiwa na uwezo mkubwa na akili na kuongoza nchi kwa maslahi ya umma, hufiki kule juu..
 
Get to know this, Samia kama Samia anapangiwa ya kufanya. Ila Rais Samia hapangiwi .


Labda utaelewa hapo.
Dah!

Hii fasihi, tunaweza kutumia muda kuidadavua uhalisia wake ulivyo; lakini hilo haliniondoi kwenya nadharia ya msingi mkuu 'CWR'.

Labda niseme tu kifupi kwamba kinachoweza kumtisha Samia juu ya Makamba ni vikundi anavyomiliki Makamba ambavyo ni vya kihalifu, hasa nyakati za chaguzi. Hiyo inaweza kuwa sababu ya kumgwaya January. Timu za akina Maharage na wengineo.
 
Parallel government.

Ndio iliyopo Tz.
 
Nchi wahuni wengi, wakisikia bei ya mafuta inapanda basi siku hiyo wiki nzima mafuta yanapatikana kwa tabu.Ewura wa kitangaza bei mpya saa sita siku ya siku inayo fuata mafuta ya naanza kupatika kwa wingi sana.

Bi mkubwa anacheka na ndezi,waziri nae mmmmhhhhhh.......... anabebwa na jina la mzee wake, yaaani tabu tubu. Tujiandae na mfumuko mwengine wa bei ya vyakula,kwani wafanyabiashara wa chakula lazima hili biti la uhaba wa dola na ongezeko la mafuta lazima wapite nalo,japo kipindi hiki chakula kipo kingi.
 
Parallel government.

Ndio iliyopo Tz.
Kwa hiyo tuseme Samia karuhusu hili, ili iweje?

Hiyo 'serikali ya pembeni' ikiharibu, akubali kubeba makosa yote?

Si angetumia mwanya huo sasa kujinanua na hiyo serikali nyingine inayokwenda sambamba na hii ya kwake?
 
Kwa hiyo tuseme Samia karuhusu hili, ili iweje?

Hiyo 'serikali ya pembeni' ikiharibu, akubali kubeba makosa yote?

Si angetumia mwanya huo sasa kujinanua na hiyo serikali nyingine inayokwenda sambamba na hii ya kwake?
Kazi ni kujinasua.

Huenda mwanzo aliona itamsaidia.

Lakini yanapoanza kuharibika, hata yeye anawaza sana.
 
Kazi ni kujinasua.

Huenda mwanzo aliona itamsaidia.

Lakini yanapoanza kuharibika, hata yeye anawaza sana.
Huo ndio udhaifu wa uongozi wenyewe. Maana yake ni kwamba huyu siyo kiongozi, ni pambo tu lililowekwa hapo na kutumiwa na wengine.
 
Huo ndio udhaifu wa uongozi wenyewe. Maana yake ni kwamba huyu siyo kiongozi, ni pambo tu lililowekwa hapo na kutumiwa na wengine.
Anatamani kujinasua.
Mfano wewe unamsaidiaje?!

Je, aanze moja? Kwa muda huu ataweza?!

Si atajiongezea maadui na wapinzani?!
 
Haya yote yalitarajiwa baada ya bi tozo kukirudisha serikalini kikosi cha vijana wapigaji.
Tukae kwakutulia. Wameambiwa "WALE KWA UREFU WA KAMBA"
 
Anatamani kujinasua.
Mfano wewe unamsaidiaje?!

Je, aanze moja? Kwa muda huu ataweza?!

Si atajiongezea maadui na wapinzani?!
Mimi nimsaidie Bi Tozo kujinasua, kwa sababu zipi hasa?
Sioni chochote katika uongozi wake kwa nchi hii kinachoweza kunisukuma nimsaidie huyu kiongozi, kwa maana amejipambanua wazi kabisa kuwa hana uchungu wowote na maslahi mpana ya nchi hii na wananchi wake..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…