Ukisoma comment za watu wengi humu ni kwamba nchi hii watu tushazoea uvunjivu wa sheria kiasi kwamba as long as una cheo basi ni haki yako kufanya chochote. Halafu watu hawa hawa baadaye utasikia wanasifia kuheshimu sheria katika nchi za wenzetu. Afrika bwana.
Mimi narudia kusema, shida ya nchi hii sio katiba bali ni utayari wa kuheshimu hata hiyo katiba. Kama mawazo na fikra za wananchi wenyewe ndio kwamba mtoto wa raisi anaweza fanya chochote, au anaweza kupewa exclusive right ya kuagiza hata matairi, hata ije katiba mpya hakuna kitakachobadilika. TRA yenyewe ina mamlaka ya kukusanya kodi kutoka kwa wafanyabiashara ila simu moja tu inawazuia kufanya hivyo.