Rais Samia ni kama bado yupo kwenye umakamu wa raisi.
Kuna vitu wala havihitaji kamati ila yeye anaunda kamati. Hadi sasa sijaona umuhimu wa kamati kuhusu tozo. Tozo mmeziweka wenyewe bila kushirikisha wananchi, halafu nyie tena haohao mnaunda kamati kuhusu hizo tozo.
Hapa Rais Samia unajichanganya sana, kwa nini hizo kamati usingeziweka kabla ya kuja hizo tozo? Mama Samia ukweli ni kuwa hii kazi ya uraisi inaenda kukupa wakati mgumu sana.
Kamati kamati kamati halafu kamati hizohizo zinaleta majibu ambayo wewe tayari ulikuwa ukiyataka, umuhimu wa kamati upo wapi?
Mama Samia ushasema tozo zipo palepale, Sasa Kama zipo palepale hiyo kamati unategemea itakupinga?
Watu walimshambulia mwigulu kuwa yeye ndio kaleta tozo Ila leo nadhani jibu wamelipata. Mama Samia unasema tozo ni kwa ajili ya kujenga barabara vijijini, kwani mbona watangulizi wako walijenga barabara nchi nzima bila hizo tozo? Uzuri watangulizi wako wengine wapo nenda kawaulize walipata wapi pesa za kujenga barabara na hospitali.
Hadi hapa umuhimu wa katiba mpya unaonekana wazi tu.
Ni muda ipo siku isiyo na jina mtatoka madarakani