Rais Samia na Lissu, mwanzo mzuri kwa Watanzania, ndicho tulichokifanya hapa Kenya

We utampigia kura Baba?

Halafu kwa nini mnamuita Baba?

Ila nawapenda wanawake wenu waliopo kwenye siasa…Sabina Chege….Cate Waiguru….nk.

Kwa sasa sijafanya maamuzi ya yupi anastahili kura yangu, kina mmoja aendelee kunadi sera zake, sio autmatic kiihivyo...
Kwa kweli ningependa raundi hii tumpe mwanamke, mama Samia ameonyesha wanaweza, sio huu ubabe wetu wa kiume.
 
Hamna aliye mwema ndani ya CCM. Je unafuatilia kesi ya kubumba ya ugaidi inayomkabili MBOWE? Ni kichekesho cha karne

Hehehe!! Huwa napitia majukwaa yenu ya siasa na kusoma kuihusu, aisei kama imebuma vile, hawakuisuka vizuri na itamtokea mtu puani, tafuteni suluhu la kisiasa kuimaliza, sio kila kitu lazima kifuate taratibu zote za mahakamani, kuna mengine yanazungumzwa na kuwekana sawa.
 
Ah wapi! Kukomoana kupo sana tu.

Juzi tu hapa Abab Namwamba wamemuondolea walinzi wake kisa kumuunga mkono Ruto.

Na hata huyo Ruto naye anahujumiwa tu sasa hivi.

Sabina Chege ana kesi ya kujibu huko IEBC kwa sababu alisema hata sasa hivi wataiba kura kama walivyoiba 2017!

Safari hii RAO ‘atashinda’ kwa sababu state machinery iko nyuma yake.
 

Nachokisema ni kwamba, huyo Ruto hajakubali kubamizwa au kuburuzwa kwa pua na rais, enzi hizo hazipo kwetu tena, kwamba rais akikohoa nyote chali, anakataliwa tu, rais Uhuru huwa namkubali ila kuna kitu imemchukua muda kuelewa tupo chini ya katiba tofauti.

Wacha waendelee na siasa zao ila Agosti ikifika tutajitokeza na kumchagua kila mmoja kwa amtakaye, kimsingi asiruhusiwe yeyote kufoka hate speech kama huyo Sabina, nampenda pia lakini hapo alivuka mpaka na alipaswa kunyea debe.

Kwa kweli napenda namna Raila na Ruto wanapelekeshana, hamna automatic, yeyote kati yao ataibuka na kutuongoza na tutampokea, japo kutakua na makasiriko ila ndivyo ilivyo kisiasa, sio lazima achaguliwe umtakaye.
 
CCM
Chanzo
Cha
Matatizo
 
Ndio maana nikamshangaa mwenzangu pale juu eti yuafananisha Miguna na Lissu. Eti official opposition leader anacharazwa viboko. Hainiingii kichwani. Hapa hata governor huwezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…