Tupambane na umasikini, ujinga na maradhi, bado vinatukwamisha na kuleta husuda na lawama nyingi, huko vijijini elimu ipelekwe Ili tuendane na mjini, hata hiyo miaka 60 tunayoilamu CCM kusema la kweli ni sisi wenyewe tujilaumu kwasababu ya ujinga wetu, imagine wafugaji na wakulima walikuwa hawapeleki watoto shule Ili wakatumike kulima na kuchunga mpaka serikali ndiyo ilazimishe watoto waende shule na bado hao wananchi wanagoma hata kujijengea shule Ili watoto wao wapate elimu na kijiji kina watumishi waliopangiwa huko wanaona wachukue uwanja wanaweka watoto juani na Mvua wanapiga picha serikali haijaleta shule bila wao kuchukua hatua zozote za kujikwamua, sasa hivi kuna umeme vijijini lakini bado watu wanataka serikali ndo iingize umeme ndani kwao, hiyo mifugo na kilimo mpaka wakauze mjini maana wao hawana hata sehemu ya kuweka soko watu wakanunue, sasa kwanini tusijilaimu sisi kwa ujinga wetu? Ujinga umetuletea umasikini na ndo maana watu wanalilia maisha ya kuitwa wanyonge Ili lawama watupie serikali wakati serikali ishawaambia familia iwe ya watoto wasiozidi 4 na Sheria za kuunda familia zimewekwa lakini bado huko vijijini hakuna kitu hicho ni mwendo wa kuishi Kama wanyama bila vitu vya kuwapa raha na maisha Bora wakitaka raha wanalazimisha kuja mjini bila kuwaza kujenga raha zao huko vijijini na serikali ingewaheshimu Kama watu wa mjini wanavyoheshimiwa.