Mifumo tena?!Mifumo ni mibovu ndio maana mnataka rais achunge hela. Kwenye mifumo yenye nguvu, CAG angejiridhisha na wezi amgewapeleka mahakamani kwa kesi. Sio mambo ya kusubiri rais wakati hakuna uhakika kama rais ni muadilifu. Kuna mwingine hivi majuzi alikuwa anajifanya mzalendo, matokeo yake imekutwa account huko China.
Hayo uliyopendekeza yatafanywa na nani kama wajinga ndio watakua wameunda serikali?Mhusika au wahusika mpaka sasa walipaswa kuwa wameshazikwa, mali zao zote mufilisi.... short and clear, kuendelea kupoteza muda na wajingawajinga matokeo yake ndio haya.
Wajinga wakiwa wengi wanachagua Rais na kuiweka serikali madarakani, wajinga wakiwa wengi wanatunga katiba yao yakuwalinda, Wajinga wakiwa wengi hata uwe na katiba bora kiasi gani watateka kila njia ili wawe salama.
Dawa ya mpumbavu na mjinga ni risasi au jela na mateso makali.
Nia ya dhati utaipata kwa nani?.Katiba Mpya peke yake haitakuwa suluhisho, kama hapatakuwepo na nia ya dhati kufuata sheria kati ya mtawala na watawaliwa..
Huyu mama ni dhaifu hilo halina ubishi.
Hilo la china ni propaganda tu.
Rais anahubiria wala rushwa na waiba mali za umma, amekua mtume mwamposa?
Kwa nchi yenye watu wanaojielewa Samia hana sifa ya kua hata balozi wa nyumba kumi.
Ajabu ndio rais, ndio maana haya yanatokea, sasa acha ahubirie wezi kwa miaka 7 ijayo kama hii nchi itakuwepo.
Kama unataka kuwa kama Marekani au China au Japan au Uingereza kiuchumi lazima ujue wanafanye kwenye kukusanya Kodi na namna wanavyoshughulika na wasiolipa Kodi na wezi wa kodi, vinginevyo itakuwa unajidanganya mwenyewe. Watanzania wote hata viongozi wetu hawana woga na Mali ya umma kwakuwa wanajua Sheria zetu na hulka ya watanzania ilivyo,hii kauli haiwezi zuia mwizi kamwe kama mtu hana hofu ya Mungu hii ni kauli ya kichekesho😀
Nasema mafisadi wanyongwetuNi kweli. Kwanza hiyo ni kauli ya kuonyesha kushindwa. Mwizi hatishiwi bali anakamatwa na kuadhibiwa.
Kama hatutaondokana na kizazi Cha waramba asali hata Rais attashindwa kufanya maamuzi. Rais amezunguukwa na watoto na wapwa wa wapigania Uhuru na machawa wa CCM.Rais amekiri Kuna WAPUMBAVU wamejipenyeza Hadi nafasi nyeti kabisa za kufanya maamuzi,
Wamefikaje hapo? Kwann anavumilia kufanya KAZI na wapumbavu?
Anaenda kukopa akileta zinaibwa.
Bado safari ni ndefu.
Kombora gani hilo urojo mtupu, yaani mwizi unamtisha na kauli za kuchomwa moto mbinguni...si kichekesho hicho.Kombora hilo ..limepiga hokooo...4eyes!!!
Mama kwa style hiyo nchi itamshinda kabla ya 2025,unaongea na wezii kwa kuwaomba wasiibe kweli hilo uliona wapi...baraza lake tu la mawaziri la hovyo,njoo wizara ya ndani napo matukio ya mauaji,utekaji,watu kupotezwa,ufisadi,unamchagua igp n dci ambao hawana uweledi ni wahuni tuNi kauli fupi sana lakini nzito kwelikweli. Akionyesha kukerwa na majizi Rais Samia aliitoa kauli hii. Majizi yote hakuna linalolala kwenye vitanda viwili, vyumba viwili wala kula sahani mbili za ugali kwa wakati mmoja, wanaiba na kurundika pesa ambazo wataziacha wakati wakifa.
Pesa hizo mara nyingi ndio zinageuka chanzo cha vifo vyao kwanjia ya kisukari, shinikizo kubwa la damu, uzito mkubwa, ugonjwa wa ini na figo, kansa, ajali za magari, ukimwi na msongo wa mawazo. Na mara nyingi fedha hizo huwa ama zinapotea au kugeuka pia kuwa chanzo cha laana na vifo kwa watoto, ndugu na wajukuu atakaowaacha. Ni heri ya mtu aliacha mti mmoja wa kivuli kwenye uwanja wake wa nyumba kuliko yule aliyeacha mabilioni ya fedha kwenye vihenge na bank.
Nimuombe tu mama yetu atengeneze katiba nzuri yenye meno kabla hajaondoka madarakani. katiba "nzuri" kwangu ni katiba ambayo:
1. Inaondoa kinga ya kushitakiwa kwa wezi wote wa mali ya umma
2. Unatoa njia rahisi ya kumuondoa kiongozi wa ngazi yoyote ambae ni mwizi au mbadhilifu.
3. Inatoa adhabu kubwa sana ya kunyonga au inayokaribia na kunyonga
4. Inatoa dira na mwelekeo wa taifa kwenye uchumi, afya, elimu, chakula na ulinzi.
Mali za Nchi haziwezi kulindwa kwa ukali wa mtu mmoja, bali kwa katiba na taasisi zenye nguvu na meno ya kuzilinda.
Mafisadi kamwe hawanyongwi. Wezi wa kuku ndiyo huuawa bila hata kwenda mahakamani.Nasema mafisadi wanyongwetu
Inasikitisha sanaMafisadi kamwe hawanyongwi. Wezi wa kuku ndiyo huuawa bila hata kwenda mahakamani.
Kama kauli haziwezi, unadhani afanye nini?Yaan hizi kauli haziwez mfanya mwizi aache kuiba .
Mama kama anataka kua Mtume, aanzishe Msikiti awe Mtume huko !!.
Mwanadamu ameumbwa kupewa Adhabu ili abadilike..
Hivi kama Yesu mwenyewe alipigwa misumali na wanazengo licha ya kwamba aliponya viwete, alifufua, na waliona kabisa Kwa macho, ila bado wakamuua,
Sembuse Hela ?? Hela ??? .
Unaona ni sawa kiongozi mkuu kulalamika?Kama kauli haziwezi, unadhani afanye nini?
By the way, umeisoma hoja ya jamaa (kavulata) mpaka mwisho kweli?
Mwenzako katoa hoja. Akapendekeza na njia sahihi ya kukomesha au kupunguza wizi..
Kasema, wizi haumalizwi na ukali wa mtu mmoja bali kutengeneza mfumo imara wa kikatiba na kisheria kumbana kila kiongozi mwenye mamlaka na maamuzi ktk nchi...
Akaendelea kusema kuwa, katiba mpya na sheria zinazotungwa zifute na kuondoa kinga ya kushitakiwa kwa kiongozi yoyote mwenye madaraka au mamlaka fulani ya umma anapofanya makosa ya ubadhirifu au wizi wa mali ya umma..!
Sasa mpaka hapo wewe unasemaje? Bado unapendekeza Rais Samia aende akawe Mtume au imamu na kuanzisha msikiti na kusema aliyosema huko?
Really??