Ni kauli fupi sana lakini nzito kwelikweli. Akionyesha kukerwa na majizi Rais Samia aliitoa kauli hii. Majizi yote hakuna linalolala kwenye vitanda viwili, vyumba viwili wala kula sahani mbili za ugali kwa wakati mmoja, wanaiba na kurundika pesa ambazo wataziacha wakati wakifa.
Pesa hizo mara nyingi ndio zinageuka chanzo cha vifo vyao kwanjia ya kisukari, shinikizo kubwa la damu, uzito mkubwa, ugonjwa wa ini na figo, kansa, ajali za magari, ukimwi na msongo wa mawazo. Na mara nyingi fedha hizo huwa ama zinapotea au kugeuka pia kuwa chanzo cha laana na vifo kwa watoto, ndugu na wajukuu atakaowaacha. Ni heri ya mtu aliacha mti mmoja wa kivuli kwenye uwanja wake wa nyumba kuliko yule aliyeacha mabilioni ya fedha kwenye vihenge na bank.
Nimuombe tu mama yetu atengeneze katiba nzuri yenye meno kabla hajaondoka madarakani. katiba "nzuri" kwangu ni katiba ambayo:
1. Inaondoa kinga ya kushitakiwa kwa wezi wote wa mali ya umma
2. Unatoa njia rahisi ya kumuondoa kiongozi wa ngazi yoyote ambae ni mwizi au mbadhilifu.
3. Inatoa adhabu kubwa sana ya kunyonga au inayokaribia na kunyonga
4. Inatoa dira na mwelekeo wa taifa kwenye uchumi, afya, elimu, chakula na ulinzi.
Mali za Nchi haziwezi kulindwa kwa ukali wa mtu mmoja, bali kwa katiba na taasisi zenye nguvu na meno ya kuzilinda.