Rais Samia: Nani atazikwa na hela?

Rais Samia: Nani atazikwa na hela?

Mifumo ni mibovu ndio maana mnataka rais achunge hela. Kwenye mifumo yenye nguvu, CAG angejiridhisha na wezi amgewapeleka mahakamani kwa kesi. Sio mambo ya kusubiri rais wakati hakuna uhakika kama rais ni muadilifu. Kuna mwingine hivi majuzi alikuwa anajifanya mzalendo, matokeo yake imekutwa account huko China.
Mifumo tena?!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mhusika au wahusika mpaka sasa walipaswa kuwa wameshazikwa, mali zao zote mufilisi.... short and clear, kuendelea kupoteza muda na wajingawajinga matokeo yake ndio haya.

Wajinga wakiwa wengi wanachagua Rais na kuiweka serikali madarakani, wajinga wakiwa wengi wanatunga katiba yao yakuwalinda, Wajinga wakiwa wengi hata uwe na katiba bora kiasi gani watateka kila njia ili wawe salama.

Dawa ya mpumbavu na mjinga ni risasi au jela na mateso makali.
Hayo uliyopendekeza yatafanywa na nani kama wajinga ndio watakua wameunda serikali?
 
Huyu mama ni dhaifu hilo halina ubishi.

Hilo la china ni propaganda tu.

Rais anahubiria wala rushwa na waiba mali za umma, amekua mtume mwamposa?

Kwa nchi yenye watu wanaojielewa Samia hana sifa ya kua hata balozi wa nyumba kumi.

Ajabu ndio rais, ndio maana haya yanatokea, sasa acha ahubirie wezi kwa miaka 7 ijayo kama hii nchi itakuwepo.

Taasisi za kukamata hao wezi ziko wapi?
 
hii kauli haiwezi zuia mwizi kamwe kama mtu hana hofu ya Mungu hii ni kauli ya kichekesho😀
Kama unataka kuwa kama Marekani au China au Japan au Uingereza kiuchumi lazima ujue wanafanye kwenye kukusanya Kodi na namna wanavyoshughulika na wasiolipa Kodi na wezi wa kodi, vinginevyo itakuwa unajidanganya mwenyewe. Watanzania wote hata viongozi wetu hawana woga na Mali ya umma kwakuwa wanajua Sheria zetu na hulka ya watanzania ilivyo,
 
Alitakiwa awaambie hakuna atakae zila hizo hela.
Kamata majizi peleka mahakamani yakanyongwe. Stupid
 
Afadhali hayo majizi yanayokwapua huko juu kwenye kodi.

Huku chini nako watumishi wa umma wameanza upya dhulumati kwa wananchi bila ya huruma ni unyanyasaji wa hali ya juu.

Mambo yamerudi upya enzi za J.K cha mtoto, watumishi wa umma wenye vinafasi vyao huko kwa wananchi ni balaa; haya mambo uwezi elewa mpaka yakukute.

Binafsi sina shida na ‘Bi Tozo’ inawezekana on personal level ni mtu mwenye huruma na mkarimu sana; lakini hizo sio sifa za raisi

Muungu ampe busara Bi Tozo asigombee 2025 anaumiza watu wengi sana huko chini bila ya yeye kufahamu na hao watu wa JK wengi sio wazuri hawana utu kabisa katika taasisi anazowaweka.

Mtaani hali inaanza kuwa mbaya sana, watumshi wa mashirika ya umma wamerudi na hasira kwenye kupora raia haki zao. Hayo mambo walishasahau zama za Magufuli; mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.

Nchi imerudi kuwa ya ovyo mno ndani ya muda mfupi; kwa diaspora mpaka yakukute ndio utaelewa. Mambo ya kuuziana kiwanja kimoja watu watatu yameanza tena, yaani vitu vingi vya ovyo ambavyo Magufuli alifuta miezi yake mwanzo tu wa uraisi vimerudi upya kwa kasi zaidi!.

Tuna raisi wa ovyo kweli
 
Rais amekiri Kuna WAPUMBAVU wamejipenyeza Hadi nafasi nyeti kabisa za kufanya maamuzi,

Wamefikaje hapo? Kwann anavumilia kufanya KAZI na wapumbavu?

Anaenda kukopa akileta zinaibwa.

Bado safari ni ndefu.
Kama hatutaondokana na kizazi Cha waramba asali hata Rais attashindwa kufanya maamuzi. Rais amezunguukwa na watoto na wapwa wa wapigania Uhuru na machawa wa CCM.
 
Bibi tozo achia madaraka jmn.

unapitaga JF, plz imetosha umeshafanya uharibifu mkubwa kuliko kujenga.

Ukitaka Tanzania ikuheshimu achia madaraka vinginevyo wewe ndo utakuwa raisi wa hovyoo kuwahi kutokea achilia mbali yule kiwete wa pwani
 
Kombora hilo ..limepiga hokooo...4eyes!!!
Kombora gani hilo urojo mtupu, yaani mwizi unamtisha na kauli za kuchomwa moto mbinguni...si kichekesho hicho.
Ye ameshachagua hayo mambo ya moto huko mbinguni sasa hapa duniani wewe mwenye mamlaka unampa adhabu gani ikiwa utamkamata na kuthibitika kweli katupiga pesa?!.
 
"NI LAZIMA WEZI WACHACHE WATOLEWE KAFARA NA IWE MFANO KWA WENGINE TENA WAWE WATU WA HADHI YA JUU KABISA SEREKALINI "
:ADHABU,
-WAREJESHE KILICHOIBWA
-KIFUNGO KIFUATE.
 
Ni kauli fupi sana lakini nzito kwelikweli. Akionyesha kukerwa na majizi Rais Samia aliitoa kauli hii. Majizi yote hakuna linalolala kwenye vitanda viwili, vyumba viwili wala kula sahani mbili za ugali kwa wakati mmoja, wanaiba na kurundika pesa ambazo wataziacha wakati wakifa.

Pesa hizo mara nyingi ndio zinageuka chanzo cha vifo vyao kwanjia ya kisukari, shinikizo kubwa la damu, uzito mkubwa, ugonjwa wa ini na figo, kansa, ajali za magari, ukimwi na msongo wa mawazo. Na mara nyingi fedha hizo huwa ama zinapotea au kugeuka pia kuwa chanzo cha laana na vifo kwa watoto, ndugu na wajukuu atakaowaacha. Ni heri ya mtu aliacha mti mmoja wa kivuli kwenye uwanja wake wa nyumba kuliko yule aliyeacha mabilioni ya fedha kwenye vihenge na bank.

Nimuombe tu mama yetu atengeneze katiba nzuri yenye meno kabla hajaondoka madarakani. katiba "nzuri" kwangu ni katiba ambayo:
1. Inaondoa kinga ya kushitakiwa kwa wezi wote wa mali ya umma
2. Unatoa njia rahisi ya kumuondoa kiongozi wa ngazi yoyote ambae ni mwizi au mbadhilifu.
3. Inatoa adhabu kubwa sana ya kunyonga au inayokaribia na kunyonga
4. Inatoa dira na mwelekeo wa taifa kwenye uchumi, afya, elimu, chakula na ulinzi.

Mali za Nchi haziwezi kulindwa kwa ukali wa mtu mmoja, bali kwa katiba na taasisi zenye nguvu na meno ya kuzilinda.
Mama kwa style hiyo nchi itamshinda kabla ya 2025,unaongea na wezii kwa kuwaomba wasiibe kweli hilo uliona wapi...baraza lake tu la mawaziri la hovyo,njoo wizara ya ndani napo matukio ya mauaji,utekaji,watu kupotezwa,ufisadi,unamchagua igp n dci ambao hawana uweledi ni wahuni tu
 
Viatu vimepwaya? Chuma kimelala!
hata Mimi ningekuwemo humo ndani kwao ningeiba tu shamba la bibi huibi unachukua!
Watu wamparura ye awapepea!!

Mama weka roho ya chui fukuza majizi yote si ripoti ya CAG unayo na majizi unayajua usikubali majizi na mawaziri mazembe yanakushusha hadhi na thamani yako kwa raia . Itakuwa Mama ukija mitaani raia hawana vibe lolote nawewe wanakung'ong'a tu maana maisha magumu sana kwasasa.
 
Yaan hizi kauli haziwez mfanya mwizi aache kuiba .

Mama kama anataka kua Mtume, aanzishe Msikiti awe Mtume huko !!.

Mwanadamu ameumbwa kupewa Adhabu ili abadilike..

Hivi kama Yesu mwenyewe alipigwa misumali na wanazengo licha ya kwamba aliponya viwete, alifufua, na waliona kabisa Kwa macho, ila bado wakamuua,

Sembuse Hela ?? Hela ??? .
Kama kauli haziwezi, unadhani afanye nini?

By the way, umeisoma hoja ya jamaa (kavulata) mpaka mwisho kweli?

Mwenzako katoa hoja. Akapendekeza na njia sahihi ya kukomesha au kupunguza wizi..

Kasema, wizi haumalizwi na ukali wa mtu mmoja bali kutengeneza mfumo imara wa kikatiba na kisheria kumbana kila kiongozi mwenye mamlaka na maamuzi ktk nchi...

Akaendelea kusema kuwa, katiba mpya na sheria zinazotungwa zifute na kuondoa kinga ya kushitakiwa kwa kiongozi yoyote mwenye madaraka au mamlaka fulani ya umma anapofanya makosa ya ubadhirifu au wizi wa mali ya umma..!

Sasa mpaka hapo wewe unasemaje? Bado unapendekeza Rais Samia aende akawe Mtume au imamu na kuanzisha msikiti na kusema aliyosema huko?

Really??
 
Kama kauli haziwezi, unadhani afanye nini?

By the way, umeisoma hoja ya jamaa (kavulata) mpaka mwisho kweli?

Mwenzako katoa hoja. Akapendekeza na njia sahihi ya kukomesha au kupunguza wizi..

Kasema, wizi haumalizwi na ukali wa mtu mmoja bali kutengeneza mfumo imara wa kikatiba na kisheria kumbana kila kiongozi mwenye mamlaka na maamuzi ktk nchi...

Akaendelea kusema kuwa, katiba mpya na sheria zinazotungwa zifute na kuondoa kinga ya kushitakiwa kwa kiongozi yoyote mwenye madaraka au mamlaka fulani ya umma anapofanya makosa ya ubadhirifu au wizi wa mali ya umma..!

Sasa mpaka hapo wewe unasemaje? Bado unapendekeza Rais Samia aende akawe Mtume au imamu na kuanzisha msikiti na kusema aliyosema huko?

Really??
Unaona ni sawa kiongozi mkuu kulalamika?

Ridhaa ya kununua Treni chakavu, mitumba Kwa Bei ya treni mpya aliitoa wapi?

Na nani aliwajibishwa Hadi sasa?
 
Sema aliwachamba sana
Jana nilikuwa nasikilizia speech yake aisee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Alichafukwa mama wa watu,hadi anawaita majitu[emoji1787]
 
Back
Top Bottom