Lakini hakuishia hapo pa hutazikwa nazo, alisema watuupishee, au hukumsikia. Kupisha kuna maana nyingi sana. Tundu Lissu aliambiwa atupishe akakiona cha mtema kuni. Shida yetu tumezoea kutawaliwa na wanaume wanaofoka tu lakini hakuna vitendo. Mfano, wakati wa wizi wa EPA, Escrow, Richmond, Melemeta, mikataba mibovu ya madini, ununuzi wa ndege kwa cash, uuzwaji wa nyumba za serikali na viwanda kwa bei ya kutupwa na wizi wa mabasi ya UDA tulikuwa na Marais wanaume, niambie waliwafanya nini wezi hao? Tusiwe na chuki binafsi na Rais huyu, subirini mtaona moto wake wa kimyakimya bila kufokafoka na kupayuka kama mlivyozoea huko nyuma. Huyu mama haoni shida CCM kupisha kama akiona ndio kikwazo cha maendeleo ya wananchi. Ana orodha ya wakwamishaji wote wote aliowaita wahavidhina wanaotukwamisha kwa maslahi yao na ndugu zao. Utamkuta mtu yeye, mkewe, mtoto wake, dada yake, mpwa wake na mjukuu wote ni viongozi ama serikalini ama kwenye chama au wako bungeni kwa njia za mchongo kama vile hii nchi ni mali yao binafsi.