Rais Samia, nani kakushauri kununua Treni zenye muundo mbovu namna hii?

Rais Samia, nani kakushauri kununua Treni zenye muundo mbovu namna hii?

[emoji38][emoji38][emoji38]
Hapana. Sikubaliani na hoja yako. Najua jinsi Hayati alivyokuwa na taste nzuri ya vitu. Kama treni tuliyo nunua ni hii, haitakuwa imenunuliwa kwenye awamu ya tano.
Angalia vitu ambavyo Hayati Magufuli amevifanya kama Dreamliner, Design ya Meli mpya Victoria, Madaraja na kadhalika. Magufuli alikuwa na Taste nzuri na alipenda vitu vizuri. Asingependa sisi tuwe na vitu vibaya hiyo nina uhakika.
Punguza ushamba, umejuaje kama hiyo treni ni mbaya!?? Nipe specifications zake. Tatizo lenu mnapinga kila kitu hata msiyofahamu! Ovyo kabisa.
 
Baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusu ile mitungi ya chang'aa sasa naweza kuja kuchangia zaidi.
Nadhani kwenye hiyo picha unaoneka.

Kwanza nataka kusema hii kampuni ya kikorea iko vizuri, wanauzoefu wa kutosha kwenye haya mambo. Kazi walizofanya nyingi zinaonekana kwenye tovuti yao.

Sasa kwenye ile mitungi ya chang'aa nahisi kuna iwezekano mkubwa sana ikaja huku kwetu. Kwe sababu zifuatazo
1: ile mitungi Korail walidesign mahususi kwa ajili ya Turkish Railways na watu wanotujemgea hii reli ni hao hao waturuki.

2: wakorea waliwapa leseni waturuki wakitengeneze kwao. Inamaanisha kwamba ni treni za kikorea ila zinatengenizwa uturuki. Na kutokana na hali ya sasa kwa mturuki ndo mpango mzima kwenye huu mradi kuna uwezekano mkubwa wakatubambika huu uchafu.

Kwa tamati, naona kama kuna kila dalili kwamba hizo ndo zitakuwa treni zetu za "kisasa" na jinsi nchi yetu ilivyo, hakuna la kufanya kabisa.

Ila tusife moyo. Tuendelee kupiga kelele humu ndani labda mama atatusikia au haya makelele yakamgusa kadogosa na akajikamua tukapata treni zingine. Maana kitreni nzuri hao wakorea wanazo kibao. Nisisi tu wenyewe kukomaa. View attachment 1849824
Samahani mkuu inabidi nisikubaliane na wewe kwa maelezo yako ya kwenye paragraph yako ya mwisho kuwa South Korea wana treni nyingi nzuri. Treni nzuri ambayo nimeiona ni hiyo KTX kidogo. Lakini hizo nyingingine huwezi kuzitumia kama treni za kusafirisha abilia wano safiri masafa marefu.
Hizo ni treni za kupiga masafa ya Bagamoyo na Kibaha, lakini sio masafa ya Mwanza au Dodoma.

Hivyo vichwa vinafaa kuvuta mabehewa ya.mizigo labda,.lakini sio kusafirisha abiria.
 
Safi Sana. Nimeona mchango wako Kwa huo Uzi.
Ulichoelezea kwamba flyover iwe ni more or less the same na original plan ya Ile flyover ya hapo ubungo. So big up for your opinion.
However Mimi nimesema kua plan ilikuja kubadilishwa wakati wa ujenzi na hakuna aliemhoji mwendazake. Lakini sasa hivi SASA mama wa watu mnamsumbuaaaaa Kwa vitu trivial.
Kwa hilo sita msamehe Hayati Rais wetu Magufuli kwa kumwamini mjenga madaraja Marehemu Engineer Mfugale. Marehemu Engineer Mfugale toka lini akajua kujenga Flyover? Sidhani kama hata hizo Flyover aliziona huko Ulaya. Yeye alikuwa mtu wa madaraja tu. Flyover kwake aliunderstand daraja la juu.
 
"Sura nzuri ya treni" ni moja ya 'specs' muhimu, kati ya hizo nyingine unazozitafuta.

Unaelewa nini ninapoulizia specs? Maana tusichanganye mmbo mambo. Muonekano ni kitu tofauti na specs.
Mfano engines zake zikoje...zinatumia nini kama nishati? Matengenezo yake yanafuata taratibu gani? Etc
 
Vijana wa tender tuitendee haki nchi yetu mstakee kutuletea madude ya aina hii ndg zetu,tupate vyombo vyenye hadhi kidogo hata Mimi babu yenu nimeumia sana kwa kweli, LAWAMA KWA WATU WA TENDER KUWENI WAZALENDO JAPO KIDOGO MSIFANYE ALI MRADI TU
 
Punguza ushamba, umejuaje kama hiyo treni ni mbaya!?? Nipe specifications zake. Tatizo lenu mnapinga kila kitu hata msiyofahamu! Ovyo kabisa.
Niache ushamba mimi au wewe? Mimi nazungumza hayo kama mtu mwenye uelewa wa mambo haya ya treni. Nimefanya kazi ya kutengeneza treni za Deutsche Bahn huko Ujerumani, ndiyo maana nayafahaamu hayo. Na ndiyo maana nakueleza kuwa hili dubwasha sio treni ya kusafirisha abiria kwenye karne hii yetu. Nisikilze ninacho kuambia. Na kama TRC ina wataalam, basi hao wataalam nina uhakika hawakuhusika kwenye kutoa maamuzi.

Hilo Container ni kichwa tu cha kuvuta wagons za mizigo na wanyama, lakini sio Lok kwa ajili ya kutumika kwenye treni ya kusafirisha abiria. Utasafirishaje abiria kwenye karne hii 21 kwenye dude kama hilo hata halina mvuto na wala halina streemlined shape ili ku-meet conditions za aerodynamic kulingana na speed iliyokusudiwa?

Dude liko liko tu utafikiri "The Rocket" treni ya George Stephenson ya karne ya 18. Mbona ni haibu kubwa sana.
 
Baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusu ile mitungi ya chang'aa sasa naweza kuja kuchangia zaidi.
Nadhani kwenye hiyo picha unaoneka.

Kwanza nataka kusema hii kampuni ya kikorea iko vizuri, wanauzoefu wa kutosha kwenye haya mambo. Kazi walizofanya nyingi zinaonekana kwenye tovuti yao.

Sasa kwenye ile mitungi ya chang'aa nahisi kuna iwezekano mkubwa sana ikaja huku kwetu. Kwe sababu zifuatazo
1: ile mitungi Korail walidesign mahususi kwa ajili ya Turkish Railways na watu wanotujemgea hii reli ni hao hao waturuki.

2: wakorea waliwapa leseni waturuki wakitengeneze kwao. Inamaanisha kwamba ni treni za kikorea ila zinatengenizwa uturuki. Na kutokana na hali ya sasa kwa mturuki ndo mpango mzima kwenye huu mradi kuna uwezekano mkubwa wakatubambika huu uchafu.

Kwa tamati, naona kama kuna kila dalili kwamba hizo ndo zitakuwa treni zetu za "kisasa" na jinsi nchi yetu ilivyo, hakuna la kufanya kabisa.

Ila tusife moyo. Tuendelee kupiga kelele humu ndani labda mama atatusikia au haya makelele yakamgusa kadogosa na akajikamua tukapata treni zingine. Maana kitreni nzuri hao wakorea wanazo kibao. Nisisi tu wenyewe kukomaa. View attachment 1849824
Inawezekana.

Enjoy Safari ya kutoka Frankfurt Germany kwenda Paris Ufaransa na IEC 3 ya Deutsche Bahn (DB) second class. By the way wajerumani wana classes mbili tu. 1st na 2nd class. Tofaut ni kwamba 1st class abiria ana uhuru mkubwa wa nafasi ya seat kuliko 2nd class.




Ni kweli Mama au serikali katika mambo haya ya ufundi inadanganywa sana na hawa wanao jiita consultants kama Hayati Engineer Mfugale.

Nilimsikitikia Marehemu Engineer Mfugale siku ile aliyokwenda kukagua daraja la Tanzanite au New Surrender jinsi Marehemu huyo alivyo udanganya umma kuhusu kucheleweshwa kwa daraja hilo na hivyo kusababisha ongezeko la $32 milioni ya gharama yote.

Marehemu aliendelea kutuambia kuwa kwenye mradi huo umechelewa kidogo kama miezi miwili kwa sababu ya janga la Corona na pili walikutana na tofauti ya Design ndani ya daraja. Walivyoweka faundation walikuta kuna maeneo yenye mwanya chini ya bahari ambayo yalisababisha ongezeko la urefu wa piles kwenda chini zaidi.

Baada ya kufanya evaluation ikaonekana kuwa kazi imeongezeka kwa mda wa miezi miwili na gharama wasilisha. Kama gharama yote ni $91milion, $30 milion itakuwa ni ongezeko la 33%. Waziri wa ujenzi unaweza kutuambia inakuwaje wewe unakaa kimya bila kuhoji mkakati huu? Au na wewe ndiyo umo kwenye hiyo 10%? Hayo ni mahesbu ya aina gani mradi wa miezi 36 uongezewe gharama ya 33% kwa mda wa miezi miwili? Mama Samia Suluhu Hassani, Rais wetu na Waziri wetu mkuu mpendwa Majaliwa Majaliwa mpo au ndiyo mnaufumbia macho huu wizi kwasabau ya kukosa knowledge ya technolojia?




Huu ni uongo wa hali ya juu. Karne hii ya leo yenye dhana kem kem za ku-detect kila kitu kilicho meta kadhaa chini ya ardhi, wakati wa survey na mchakato wa physibility studies, anakuja kutueleza sisi mambo ya uongo na yasiyo na tija, ili tu serikali itoe hela nyingi zaidi kwa ajili ya 10% yao, wakati wataalam wetu wengi wanauvumilia tu upuzi huo?

Maelezo kama haya nilitegemea vyombo vya habari kuhoji kwanini hawakutambua mapema na watoe uthibitisho wa maelezo hayo na siyo kwa maneno tu. Hii ni absurd story, sorry!

Nilisononeka sana moyoni, kwani niliona jinsi gani hapo Marehemu Engineer Mfugale alivyo kuwa akituchapa wazi wazi.

Ningemshauri Mama yetu na viongozi wetu wengine kuweka chombo cha wataalam wa kisanyansi na technolojia waliobobea kwenye maswala mazima ya ujenzi na uundaji wa vitu tofauti ili maelezo kama haya ambayo, watu wanao jiita consultants na makadarasi wanayatoa kama kisingizio, waya-verify na wakibaini kuwa ni uongo serikali ichukue mkondo wake wa kuwachukulia hatua watu wa namna hiyo. Vinginevyo tutakuwa tuna chapwa kila wakati na hatimaye hatufiki kokote katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.

Kujua Science nako kuna faida zake!
 
Treni ilinunuliwa awamu ya Magufuli. Usimsingizie mama bure.
Hii vipi

Screenshot_20210712_143150.jpg
 
Nyoka tena! Kikubwa ziwe imara na zenye mwendo mzuri, mambo ya show waachieni wazungu au Mamiss.
Acha kujidharau mwenyewe, kwani wewe na mzungu mnatofautiana nini? Rangi yako ndiyo inakufanya ujishushe kwenye level ya mnyama? Kakae porini basi tujue moja.
 
Hii no kuanzia jamani. Ni sawa kuwa na gari kwa mara ya kwanza. Toyota mkonga. Baadaye ni Toyota XV baada ya kupata pesa za mafuta ya Uganda na nikkia toka bukoba. Na chuma ya liganga
 
Unaelewa nini ninapoulizia specs? Maana tusichanganye mmbo mambo. Muonekano ni kitu tofauti na specs.
Mfano engines zake zikoje...zinatumia nini kama nishati? Matengenezo yake yanafuata taratibu gani? Etc
Pamoja na muonekano nayo ni specifications mfano magari ya surv, hatchback, saloon hizi ni specification tosha
 

Kusema kweli leo nimesikitika sana kuona aina ya muundo wa treni ambayo serikali yetu imeweka mkataba na kampuni ya Hyundai-Rotem ni treni zenye mwonekano wa ki-Hitler!

Mimi nilifikiri tunaondokana na treni zenye muundo wa kutisha za enzi za George and Robert Stephenson na kuingia kwenye era ya treni za umeme zenye kuburudisha macho kwa design kama za wenzetu wajerumani.

Mama samia Suluhu Hassan Rais wetu nani kakupa ushauri wa kutua saini ya makubaliano ya kununua treni za aina hiyo? Mimi sitaki kuamini na sikutegema kama aina ya treni ambazo zitatereza kwenye reli yetu zingekuwa na mwonekano huo kwenye hiyo picha ya taarifa tuliyoipata kwenye Website ya hiyo kampuni iliyo shinda zabuni ya Hyndai-Rotem. Mbona inatisha?

Nitashangaa sana kama upande mmoja tumejitahidi kutengeneza Stations nzuri, za kisasa na zenye mwonekano mzuri na wa kupendeza na kupata system yenye technology mpya, alafu leo tunaambiwa kuwa tunapata treni zenye vichwa na mabehewa ya enzi za Hitler? Ama kweli Tanzania tunawatu ambao kweli hawajui kwenda na na wakati. Watu wasiokuwa na test ya biashara. Mnategemea nani mtampata kwenye kwenye hayo ma-wreck yenu?

Mkurugenzi Kadogosa hii sio treni ambazo models zake mtangazaji wako Beni Mwanantala amekuwa akituonyesha kwenye maonyesho uwanja wa sabasaba kurasini.

That's awful! Are you really serious with this mkurugenzi?

Sasa naomba niambie kuna tofauti gani na SGR ya kenya kimwonekano? Inamaana mnatufanya sisi ni masokwe mpaka mnatuletea matakataka kama haya ambayo hakuna mtu anaye yataka?

Waziri wa Ujenzi na uchukuzi hivi ni sahihi kweli sisi watanzania mtusweke kwenye ma-wagon yanayo onekana kama treni za kusafirisha mizigo na wanyama kama haya ambayo hata hayavutii? Mmepewa bure nini? Ama ndiyo tuseme mmedhamiria nini kutuletea? Tuambieni?

Nilipokuwa kwenye jengo lenu la maonyesho ya sabasaba mwaka jana na kujionea mwenyewe models za treni na mabehewa ambayo Mr. Mwanantala alitupa maelezo yake, aisee, nilifarijika sana sana moyoni na niliwaombea baraka nyingi kwa muumba wetu za kuwaongoza vizuri katika shughuli zenu za kuwatumikia Watanzania.

Sikutegemea kabisa kuwa leo ingekuwa siku ya majonzi makubwa kwa kuona au kusikia mashine zitakazo tereza kwenye reli yetu ya kisasa ya SGR kumbe ni madudu ambayo yamepitwa na wakati na yasiyo na mvuto hata lidogo. ES IST SCHRECKLICH!

inafanana na ya TAZARA
 
Pamoja na muonekano nayo ni specifications mfano magari ya surv, hatchback, saloon hizi ni specification tosha
Lets have a look at the most expensive cars...ili tuone kama zina mvuto huu
Halafu hii sio gari binafsi . Haitapandwa sababu ya hizo engine?
 
Back
Top Bottom