Rais Samia, nani kakushauri kununua Treni zenye muundo mbovu namna hii?

Rais Samia, nani kakushauri kununua Treni zenye muundo mbovu namna hii?

Mkuu nami nashangaa malalamiko haswa ni ya nini?
Tuondoe hofu kwa muonekano. Hili linaonekana kama kondoo lakini ni double deck na hebu angalia ndani uone

Screenshot_20210712_184650.jpg


Screenshot_20210712_184629.jpg


Screenshot_20210712_184559.jpg
 
Mbona hazina ubaya wowote...

Unataka kama za Tokyo zile bullet train... Zile ni gharama sana...
Sikiliza mkuu. Kwenye Website ya Hyundai Rotem imeandikwa kama ifutavyo; South Korean-based company Hyundai Rotem has won a $ 295.65 million (335.4 billion won) contract from the Tanzania Railways Limited (TRC) to deliver eco-friendly rail vehicles.

Under the contract, TRC will receive $ 190.12 million worth of 80 trains and $ 155.3 million worth of 17 electric locomotives from Hyundai Rotem.

Hayati Magufuli yeye katika uzinduzi wa safari za treni Arusha alisema kuwa serikali imepanga kununua vichwa vipya 39 vya treni kwa njia kuu, vichwa 18 vya treni sogeza sogeza, mabehewa 800 ya mizigo na mabehewa 37 ya abiria. Kwa hali hii inaonyesha dhahiri kuwa hapa hakuna dalili za kupata treni ya nyoka. Hebu tumsikiliza Hayati mwenyewe anavyosema;




Chakujiuliza ni kwamba kama serikali inatumia $295.65milioni ambazo sawa na TSH 700 bilioni kununua vichwa 17 vya treni na mabehewa 80, kuna shida gani ya kutumia TSH 2 trilioni kununua hata treni nne tu kwanza za kuanzia kwa masafa ya DAR-MORO?

Kwa nchi yenye rasilimali kem kem kama hii yetu sioni haja ya kuwa na reserve ya $4.5 bilioni. Za nini, wakati nchi hivi sasa inahitaji hizo hela kwa maedeleo yake ya uchumi? For me it doesn´t make any sense. Does it? Tungekuwa hatuna kitu cha kuuza hapo sawa. Hizi hela zingetosha kabisa kwenye kuwekeza katika miundo mbinu hiyo ya kimkakati ili ije kuwavutia watalii wa nchi jirani.
 
Tuondoe hofu kwa muonekano. Hili linaonekana kama kondoo lakini ni double deck na hebu angalia ndani uone

View attachment 1850770

View attachment 1850771

View attachment 1850772
😁😁😁😁😁 Nafurahi sana unavyo jitahidi. Hii kwa nchi kama Ujerumani ni treni ambayo wanaiita RB (Regional Bahn), yaani ni treni ambayo ina kwenda masafa mafupi within a region labda na majimbo jirani, wenyewe wanasema (Nahverkehr). Huwezi ukasafiri na treni ya muundo huu kutoka Duesseldor (Nordrhein Westfallia) mpaka Berlin, kwa mfano. Hii treni haiko katika category ya High-Speed train. Kwa speed yake ya jongoo ukifika Berlini utakuwa hoi kwa kuchoka.
au zile za kisasa zaidi Intercity 2
 
Hivi ni ufyatu au ni ile kawaida ya watu kupenda kulalamika? Mtoa hoja amejuaje kuwa treni iliyoko kwenye picha ya habari ndio model ya treni Tanzania inatengenezewa?
Msikilize hayati Magufuli kwenye hotuba yake Arusha.

 
Mimi kwa maoni yangu nadhani wasi wasi wa mtoa mada unatokana na historia ya Tz katika maswala ya miundo mbinu. Baada ya kuona picha ya treni iliyochapishwa na jinsi ambavyo hali ya manunuzi huko nyuma kwa kweli mtu yeyote mwenye kujali bila ya kufikiri zaidi atadhani ndicho kinachokuja of which inawezekana pia kuwa ni kweli ndivyo vinavyoletwa. Sasa kama umeamua kujitutumua kuvaa suti kipindi hiki basi hakikisha unavaa suti iliyokamilika siyo suti nzuri kisha chini unamalizia na yeboyebo yani ujenge reli nzuri kama inavyojengwa vituo vizuri sana uimarishe upatikanaji wa nguvu ya uendeshaji kisha umalizie na train kuu kuu. Hata mimi nina wasiwasi sana na waliopewa wajibu wa kusimamia manunuzi kama ni kamati zile za kipigaji na hivi mwanzilishi wa mradi wenyewe hayupo aiseee wanaweza kuingia mkataba wakatuletea vitu vya ajabu sana badala ya kuendelea tukajikuta tunaharibu hata rail yenyewe
🙏 👏 Ume-state vizuri sana!
 
Mkuu nami nashangaa malalamiko haswa ni ya nini?
Kama hujui watu wanalalamikia nini, basi inawezekana hata maana ya maendeleo hujui. Kama ungejua maana yake nafikiri ungejiuliza kwanza kwanini unatumia smart phones badala ya kitochi. Ukipata jibu lake nafikiru utajua kwa nini tuna lalamika.
 
Kama hujui watu wanalalamikia nini, basi inawezekana hata maana ya maendeleo hujui. Kama ungejua maana yake nafikiri ungejiuliza kwanza kwanini unatumia smart phones badala ya kitochi. Ukipata jibu lake nafikiru utajua kwa nini tuna lalamika.
What matters is movement, at a speed of 160km/hr max.
Everything else does not matter.
Sasa malamiko yako nini?
 
What matters is movement, at a speed of 160km/hr max.
Everything else does not matter.
Sasa malamiko yako nini?
Unasema hivyo kwa sababu hujapata nafasi ya kulinganisha vitu. Subiri ukija pata nafasi hiyo utasema vingine. Kuna watu walipoiona bahari ya Indi wakajua hakuna maisha mengine tena. Walivyo kwenda Ulaya mambo yakawa mengie ghafla. Sishangai misemo ya watu kama nyie.
 
Unasema hivyo kwa sababu hujapata nafasi ya kulinganisha vitu. Subiri ukija pata nafasi hiyo utasema vingine. Kuna watu walipoiona bahari ya Indi wakajua hakuna maisha mengine tena. Walivyo kwenda Ulaya mambo yakawa mengie ghafla. Sishangai misemo ya watu kama nyie.
Mkuu huongei na mkulima, nina uhakika hujapanda Shinkansen at 300km/hr!
Wenzio huko nyumbani!
Ndio maana tunakushangaa!
 
Mkuu huongei na mkulima, nina uhakika hujapanda Shinkansen at 300km/hr!
Wenzio huko nyumbani!
Wanajamii hapa ni nyumbani jamvini nawasihi sana tusimame zaidi kwenye mijadala ya kujenga lakini na utani tusiuache kwa sababu nikimkuta mtani wangu hapa ametoa hoja lazima kale ka bond ka togetherness kanakuwepo lakini siyo kushambulia kama unataka kutoa uhai kwa sababu ya hoja tu. Maarifa uzosfu undugu ujirani ukaka umoja vyote tunavipata hapa. Mwalimu wa sanaa tunamuhitaji hapa daktari tunamuhitaji mvuvi name them. Haya sasa tuendelee na hoja ya kumsaidia mama samia kuhusu swala hili la reli. Nawakilisha
 
Mkuu huongei na mkulima, nina uhakika hujapanda Shinkansen at 300km/hr!
Wenzio huko nyumbani!
Ndio maana tunakushangaa!
Hata mkulima anapanda High-Speed treni. Ulaya nzima zimejaa hizo za aina tofauti. Wajerumani wana ICE ambayo inapiga mpaka 330 km/h. Wafaransa wana TGV Dupplex mpaka 400km/h na waitalia nao hivyo hivyo. Sasa sijui utakuja na lipi? Wakati Ulay yote ni moja. Angalia vitu nilivyo vipanda.










Treni ambayo ningependa kusafiri nayo, kwa kukupa siri, ni Maglev Train. Nataka nipate feeling ya Maglev Train. Kama wewe umebahatika kusafiri na Maglev basi nakuvulia Kofia. Mimi bado.
 
Wanakupa kile kinachoendana na uwezo wako wa kiuchumi. Tube train haiwezi kutumia reli ya 1.435 M hii ni kwa ajili ya Boxcab (Diesel/Electric Locomotives) tu na ndio itakayonunuliwa na TRC. Tube trains kwa Afrika bado tutasubiri sana.
halafu kaenda mbali zaidi kumuhusisha rais na ununuzi wa vichwa vya train. rais anaenda kuchagua vichwa!?! naamini yeye anaishia kwenye kuidhinisha pesa tu. wengine hawa hawajui kama zipo tube train wao mradi ya umeme tu
 
Pesa ya beetle old model ununulie Mercedes new model?? Aisee inawezekana vipi?NA USIKUTE UNALALAMIKA TU,NA KODI UNAKWEPA(HAULIPI)
 

Kusema kweli leo nimesikitika sana kuona aina ya muundo wa treni ambayo serikali yetu imeweka mkataba na kampuni ya Hyundai-Rotem ni treni zenye mwonekano wa ki-Hitler!

Mimi nilifikiri tunaondokana na treni zenye muundo wa kutisha za enzi za George and Robert Stephenson na kuingia kwenye era ya treni za umeme zenye kuburudisha macho kwa design kama za wenzetu wajerumani.

Mama samia Suluhu Hassan Rais wetu nani kakupa ushauri wa kutua saini ya makubaliano ya kununua treni za aina hiyo? Mimi sitaki kuamini na sikutegema kama aina ya treni ambazo zitatereza kwenye reli yetu zingekuwa na mwonekano huo kwenye hiyo picha ya taarifa tuliyoipata kwenye Website ya hiyo kampuni iliyo shinda zabuni ya Hyndai-Rotem. Mbona inatisha?

Nitashangaa sana kama upande mmoja tumejitahidi kutengeneza Stations nzuri, za kisasa na zenye mwonekano mzuri na wa kupendeza na kupata system yenye technology mpya, alafu leo tunaambiwa kuwa tunapata treni zenye vichwa na mabehewa ya enzi za Hitler? Ama kweli Tanzania tunawatu ambao kweli hawajui kwenda na na wakati. Watu wasiokuwa na test ya biashara. Mnategemea nani mtampata kwenye kwenye hayo ma-wreck yenu?

Mkurugenzi Kadogosa hii sio treni ambazo models zake mtangazaji wako Beni Mwanantala amekuwa akituonyesha kwenye maonyesho uwanja wa sabasaba kurasini.

That's awful! Are you really serious with this mkurugenzi?

Sasa naomba niambie kuna tofauti gani na SGR ya kenya kimwonekano? Inamaana mnatufanya sisi ni masokwe mpaka mnatuletea matakataka kama haya ambayo hakuna mtu anaye yataka?

Waziri wa Ujenzi na uchukuzi hivi ni sahihi kweli sisi watanzania mtusweke kwenye ma-wagon yanayo onekana kama treni za kusafirisha mizigo na wanyama kama haya ambayo hata hayavutii? Mmepewa bure nini? Ama ndiyo tuseme mmedhamiria nini kutuletea? Tuambieni?

Nilipokuwa kwenye jengo lenu la maonyesho ya sabasaba mwaka jana na kujionea mwenyewe models za treni na mabehewa ambayo Mr. Mwanantala alitupa maelezo yake, aisee, nilifarijika sana sana moyoni na niliwaombea baraka nyingi kwa muumba wetu za kuwaongoza vizuri katika shughuli zenu za kuwatumikia Watanzania.

Sikutegemea kabisa kuwa leo ingekuwa siku ya majonzi makubwa kwa kuona au kusikia mashine zitakazo tereza kwenye reli yetu ya kisasa ya SGR kumbe ni madudu ambayo yamepitwa na wakati na yasiyo na mvuto hata lidogo. ES IST SCHRECKLICH!

Hivi jamani sisi tunaopenda kununua vyakula kama mayai, hafu keki, mahindi ya kuchomwa/kuchemshwa safarini kama pale Chalinze, kwenye hayo madude tutayapatia wapi? Yani mimi kupanda chombo bila ya kununua hizo bidhaa kwa dirishani naona kama sijasafiri.
 
Hiyo ya chini ni ICE 5. Bado iko katika majaribio. Kampuni ya Siemens ndiyo wanatengeneza wakishirikiana na wataalam wa DB (Deutsche Bahn).
Mahali inapofanyiwa majaribio ndipo ninapoishi mimi NRW kwenda münchen ambako nimeishi miaka 20 pia. Nadhani target ya hii ICE 5 hadi 2022 iwe imekidhi kiwango cha 330km/h kwa hivyo utaona tofauti ya kuwa nayo bado pia kuna kuwa na muda wa kuifanyia majaribio kama inakidhi kile haswa kinachohitajika. Ndiyo maana ninaona mjadala huu una umuhimu mno kwa maendeleo ya hiyo SGR yetu
 
Back
Top Bottom