Jf ni platiform kubwa kwenye mitandao ya kijamii ya Tanzania. Karibu viongozi wakuu wote wa serikali na taasisi zake wamo kwenye mtandao huu na huwa wanapitia mara kwa mara mijadala inayohusu sekta zao zinazotolewa au kulalamikiwa humu. Hususani tanesco huwa hawachelewi kuzitolea ufafanuzi. Kwa nini Bw. Kadogosa amekuwa kimya kutolea ufafanuzi wa suala hili kama ni la kweli au si la kweli? Waziri wa uchukuzi naye kimya kwa nini? Lazima kuna jambo walilolivurunda hapa. Kimya chao kitaeleweka hivyo ie ufisadi. Ni vyema wakajitokeza kututoa kwenye hisia hizi za ufisadi.
Inauma sana. Yaani treni zetu zinazonunuliwa zinapitwa hadi na zile za Kenya zinazotumia dizeli wakati sisi ni za umeme? SGR yetu ni ya kisasa kabisa inayoruhusu hadi treni za spidi ya 400 kph?
Tazama hapa treni za dizeli za Kenya halafu ulinganishe na hizo za Kadogosa:
View attachment 1851927
Yaani hili halikubaliki. Tunahitaji bullet trains za kisasa. Nchi yetu ni tajiri sana barani Afrika. Tuanze sasa kujionesha hivyo kama tulivyofanya kwenye Dreamliners. We should think Big.Tuanze na bullet trains chache kama uwezo hautoshi kwa sasa, zenye uwezo wa kusafiri masaa matatu kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, sangara wa Mwanza wafike Kariakoo wakiwa fresh kabisa pamoja na senene wa kutoka huko Katerero. Mama yetu wa Taifa aingilie suala hili.