Rais Samia, nani kakushauri kununua Treni zenye muundo mbovu namna hii?

Rais Samia, nani kakushauri kununua Treni zenye muundo mbovu namna hii?

Je! Wameeleza mchakato wa ugavi na ununuzi ulivyofanyika? Au ndo yaleyale ya jiwe na bombadia

Watuweke wazi tujue ni shi ngapi, sio watupige hela alafu baadae CAG atulete kumbukumbu zake hatutaki huo mchezo. Msichezee Kodi zetu!!!
Nenda kwenye Website ya Hyundai. Link yake si imewekwa kwenye mada? Utaona kila kitu.
 
Hiyo KTX juu ipo safi, lakini hizo nyingine za chini hapana aise

Hata mimi naona ya juu ni nzuri ila zinapishana bei na sisi naona ndio tumeona bei yetu imefika kwa hizo
Ila sio mbaya maana treni zetu za sasa zina mwendo mdogo sana
Ila hizo at least zinagonga 130m kwa saa na hiyo ya juu ni bullet train nafikiri
 

Kusema kweli leo nimesikitika sana kuona aina ya muundo wa treni ambayo serikali yetu imeweka mkataba na kampuni ya Hyundai-Rotem ni treni zenye mwonekano wa ki-Hitler!

Mimi nilifikiri tunaondokana na treni zenye muundo wa kutisha za enzi za George and Robert Stephenson na kuingia kwenye era ya treni za umeme zenye kuburudisha macho kwa design kama za wenzetu wajerumani.

Mama samia Suluhu Hassan Rais wetu nani kakupa ushauri wa kutua saini ya makubaliano ya kununua treni za aina hiyo? Mimi sitaki kuamini na sikutegema kama aina ya treni ambazo zitatereza kwenye reli yetu zingekuwa na mwonekano huo kwenye hiyo picha ya taarifa tuliyoipata kwenye Website ya hiyo kampuni iliyo shinda zabuni ya Hyndai-Rotem. Mbona inatisha?

Nitashangaa sana kama upande mmoja tumejitahidi kutengeneza Stations nzuri, za kisasa na zenye mwonekano mzuri na wa kupendeza na kupata system yenye technology mpya, alafu leo tunaambiwa kuwa tunapata treni zenye vichwa na mabehewa ya enzi za Hitler? Ama kweli Tanzania tunawatu ambao kweli hawajui kwenda na na wakati. Watu wasiokuwa na test ya biashara. Mnategemea nani mtampata kwenye kwenye hayo ma-wreck yenu?

Mkurugenzi Kadogosa hii sio treni ambazo models zake mtangazaji wako Beni Mwanantala amekuwa akituonyesha kwenye maonyesho uwanja wa sabasaba kurasini.

That's awful! Are you really serious with this mkurugenzi?

Sasa naomba niambie kuna tofauti gani na SGR ya kenya kimwonekano? Inamaana mnatufanya sisi ni masokwe mpaka mnatuletea matakataka kama haya ambayo hakuna mtu anaye yataka?

Waziri wa Ujenzi na uchukuzi hivi ni sahihi kweli sisi watanzania mtusweke kwenye ma-wagon yanayo onekana kama treni za kusafirisha mizigo na wanyama kama haya ambayo hata hayavutii? Mmepewa bure nini? Ama ndiyo tuseme mmedhamiria nini kutuletea? Tuambieni?

Nilipokuwa kwenye jengo lenu la maonyesho ya sabasaba mwaka jana na kujionea mwenyewe models za treni na mabehewa ambayo Mr. Mwanantala alitupa maelezo yake, aisee, nilifarijika sana sana moyoni na niliwaombea baraka nyingi kwa muumba wetu za kuwaongoza vizuri katika shughuli zenu za kuwatumikia Watanzania.

Sikutegemea kabisa kuwa leo ingekuwa siku ya majonzi makubwa kwa kuona au kusikia mashine zitakazo tereza kwenye reli yetu ya kisasa ya SGR kumbe ni madudu ambayo yamepitwa na wakati na yasiyo na mvuto hata lidogo. ES IST SCHRECKLICH!

Hawa Hyundai sijui wanapendewa nini nahisi kuna 10% za wa Msowger humu! Maana yale ma Lift ya Hyundai pale Mloganzila ni mabovu almost 50% of them na hospitali haina hata 10 years toka uzinduzi!

Huo mtreni utakuwa mbovu bovu tu bila shaka! Tunaacha kununua treni za kijapani ama kichina ambao ndio wakali wa hizi kazi mnunue treni la mkorea kweli
 
Jamaa ameleta picha ya nyuma ya Train, mimi sijawahi kufika ulaya ila nazionaga hizo Train kwenye movies na kiuhalisia kwa nyuma ni mbaya zote.hakuna Train nzuri nyuma, kitu cha msingi ni kwamba zinasafirisha watu haraka na kwa usalama
Si kweli. Kaangalie tena hizo movies kwa makini zaidi, alafu ndiyo uje tena uthibitishe hoja yako.
 
Mkuu utamudu kununua treni toleo la kisasa inayoenda kwa supersonic speed iliyotengenezwa na majapan au mkorea? Je, kwa namna miundombinu yetu ya SGR ilivyojengwa inamudu kweli ku operate toleo la kisasa la hizi treni ambazo zinakwenda kasi ya ajabu. Nafikiri pamoja na ubora na kasi lazima wazingatie gharama au bei ya hizo treni, ili angalau kukidhi mahitaji. Huko mbeleni baada ya kukusanya pesa ya kutosha ndo unaweza kuingiza mdogo mdogo matoleo ya kisasa zaidi.......mwanzo mgumu.
 
Hukumbuki jinsi mlivyo mnanga na zile ndege zake za panga boi!
Zile za pangaboi tulizihitaji haraka na kwa wakati ule hatukuwa na Airports nyingi ambazo ndege za jet zingeweza kutua. Bombardier Q400 zinaweza tua kwenye mazingira magumu pia.
 
Bado hatuchelewa wanaweza kurekebisha Ilo. Train zitakuwa tofauti sana na train stations zetu ambazo ziko kisasa. Rekebishani jamani nyie wenye mamlaka, hizo ni za stone age, mostly likely.
Sure.
 
Hizi zenye sura ya nyoka,wanasema zinatumia sana mafuta [emoji125][emoji125][emoji125]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mkuu acha masihala bwana. Mambo ya mfuta yanakujaje?
 
Tumeliwa Sana Ndugu Zangu
Tumelaliwa Sana Ndugu Zangu
[emoji3][emoji16][emoji23][emoji2][emoji1][emoji28][emoji38][emoji28][emoji1][emoji38][emoji2][emoji23]
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Back
Top Bottom