Rais Samia: Nani kasema Maendeleo yanaletwa na Kitabu? Mbona Vitabu vya Dini tunavikiuka?

Hapa tulipigwa na kitu kizito Sana, hizi habari za makamu kua Raisi baada ya Raisi kufariki inabidi zitupiliwe mbali kabisa ili kuepusha kua na kiongozi mkuu wa hovyo, japo hata wanao chaguliwa na wenyewe ndio wale wale
 
Tangu lini Mwanamke akawa Kiongozi?,Mwanamke anafaa akae nyumbani amfulie mumewe,kupika na kuosha vyombo
Kikwete kwa kuwa sponsor wa huyu bibi alikuwa anajitengenezea namna ya kutengeneza himaya ya kuwarithisha watoto wake!! Baada ya Mangulla kuondoka simuoni mtu mwingine kwenye safu ya uongozi wa ccm atakayeweza kumthibiti Mkwere na genge lake!!
Kama mnakumbuka kuwa ni Kikwete huyu huyu ndio aliiweka rasimu ya Katiba iliyopendekezwa na wananchi kwapani ili kulinda maslahi ya kikundi chao! Na watatatumia kila mbinu ili uchaguzi wa serikali za mitaa na ule wa 2025 ufanyike bila marekebisho yoyote ya maana ya katiba ili institutions zitakazohakikisha anashinda zibaki intact!!
Unfortunately, Samia hajui kusoma alama za nyakati, kwani Tanzania ya leo sio ya jana na haya anayosema maendeleo hayaji wakati nchi ina machafuko!! Vijana hawana ajira kwa sababu ya katiba iliyopo na hawatakuwa tayari kuona kuwa ndoto zao hazitimii kwasababu ya kikundi cha watu kutaka kukaa madarakani bila kuwa na uwezo wa kuwakwamua kutoka kwenye lindi la umaskini!!
 
 
Kwani Katiba ya Sasa haileti hayo mazingira mazuri ya kiutawala? Ingekuwa haileti Tanzania ingekuwa unarudi nyuma.

Katiba haileti maendeleo na Wala haijawahi leta maendeleo popote.

Kwa kuwa mnadhani Katiba itawasaisia kushika Dola Rais aipige chini mazima kwanza haipo kwenye ilani ya ccm,yeye anatekeleza ilani ipi Kwa kuzungumzia Katiba?
 
Hoja yake kubwa ni kwamba wananchi wasiendeshwe kwa kisingizio cha Katiba Mpya. Hiyo hiyo Katiba ya 1977 mbona imeleta mambo mengi mazuri!! Kimsingi hata hiyo Katiba ya 1977 ambayo inapondwa kama ukiiheshimu inaweza ikakupa maendeleo.

Wapinzani wanataka katiba mpya ili waweze kuitoa CCM madarakani, na CCM wanataka Katiba ya 1977 ili wasitoke madarakani.

Kimsingi matakwa ya wananchi walio wengi siyo katiba bali maendeleo. Wanaotaka Katiba Mpya wanataka kuingia madarakani.

Hata wao wenyewe wanaotaka Katiba Mpya, vyama vyao havina Katiba Mpya. Na vina Udikteta kuliko hata wa CCM. Kuna Mbowe ni M/Kiti wa CHADEMA toka 2003, je kweli hicho chama kina Katiba?

Clean your linen first before raising your hand to others.

Ukutuliza akili utamuelewa Samia.
 
Mwamakula na Warioba wakikunja nyuso ndiyo kiashiria cha katiba mbovu? Kweli hii nchi ina mahayawani wengi, yaani tuangalie uso wa Mwamakula badala ya kuangalia content.?

Nyinyi mlijiandalia hotuba yenu, lakini Samia ametoa hotuba yake
 
Kosoa kwa staha na adabu na siyo kutumia lugha kama kichaa na mwendawazimu.
Yeye hiyo staha na adabu anayo? Kusema Watanzania hawajui katiba huoni ni kukosa adabu?

Wangekuwa hawajui katiba maana yake hata yeye angepingwa asiwe Rais, lakini tunajuwa katiba inasema nini baada ya Rais Magufuli kufa.
 
Jibu swali Katiba Mpya imeleta maendeleo Nchi gani hapa Africa.

Kunitukana Wala hakupunguzi ujinga wako
Hebu kamuuliza mpuuzi mwenzio kwamba anaongoza Nchi kwa taratibu zipi?, Au ndio mmebakiza kuhamsisha ushoqer na Kitenge wenu?.
 
Hebu kamuuliza mpuuzi mwenzio kwamba anaongoza Nchi kwa taratibu zipi?, Au ndio mmebakiza kuhamsisha ushoqer na Kitenge wenu?.
Kwa taratibu za Katiba iliyopo ambayo imeivusha Nchi Toka 1961 Hadi Sasa.

Ni hivi kama mliyegemea Kulazimisha Katiba Mpya ya Kisiasa imewakata,kilochobakia toeni mapovu weeee kama ya DP World harafu mtaacha wenyewe baada ya watu kuwapuuza
 
NN , sikuwa disappointed nilikuwa stressed and depressed

Kwamba tuna Rais anayeongoza nchi kwa fikra zake na si muongozo unaoitwa Katiba.
Pengine ndiyo maana alimtuma mwanae Uganda bila kuwa na nyadhifa serikalini

Tuna kiongozi anayedhani ameingia madarakani kwa mazingaombwe na siyo katiba.

Wale waliodai na kulalamikia katiba (Zanzibar) wapo kimyaaaa! angsema Mbowe mama yangu! leo wangekuwa Bumbwini, Kibandamaiti, Kojoawima, wakibwbwaja.
 
Uhusiano wa hawa wawili inabidi iwekwe wazi kwa manufaa ya taifa
Sasa watu wakiandika unwell mnasema wanawatukana!! Wenye kujua kingereza someni hayo aliyoandika Ridhwani Kikwete ambae ni naibu Waziri katika serikali ya Samia ; na next time atapewa wizara kamili! Hicho kingereza ni cha mtu mwenye shahada ya sheria kweli? Ni aibu kwa waliomteua kwenye huo wadhifa kwani inaonesha wazi kuwa aliteuliwa sio kwa sababu ya weledi wake bali kwa sababu ya jina la baba yake!! Shame.
 
NDIYO

Yaliongelewa ya busara kabisa na tena kuwekwa kinaga ubaga kuhusiana na mawili: 'uwepo wa Katiba' na 'kuuishi mwongozo wa kiKatiba'.

Maneno yaliyozungumzwa yanao mwanzo mzuri wa kuuleta uamsho katika Jamii; kila mwanajamii anaowajibu wa kuifahamu Katiba--katiba iliyopo, lau misingi ya Katiba katika Jamhuri... Kuifahamu na Kuiishi.

Hufikirika, kwa kasumba, Katiba ni kitabu kigumu kukielewa labda(?) Jambo hili si ukweli, katiba inaweza kueleweka kwa ufasaha na ufanisi miongoni mwa wanajamii ikiwa kuna 'Uono na Ufikirifu Mifumo' ilivyo ni Elimu 2.0.

Elimu inayoweza kuleta chachu ya Watu na Katiba ni Elimu 2.0 na Elimu 3.0... Hii siyo tu inawajibisha 'Wanajamii'--inawajibisha pia na watu wenye dhamana ya Uongozi katika Jamii.

Rais Samia, kwenye hili kazungumza ukweli mtupu na kaweka 'siasa za hadaa' pembeni, tushukuru.

Ikiwa Rais Samia, katika hili anaweka nia thabiti ya kujisahihisha kitaasisi na mifumo, kuna mengi 'yaliyozorota kitaifa' ambayo yanayosahihishika hata leo na sasa--pasipo kujali 'mtihani' wowote alionao kisiasa.

 
Kwani Rais Dr.Samia je anakosea kila kitu?.Bandari amekosea ,Katiba anakosea. Ivi nyie mnataka nini ? BANDARI AU Katiba? Acheni kukusumbua Rais nyie ndio maana wananchi hata mkitangaza maandamano hatuendi. Ni ujinga kukosoa kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…