Rais Samia: Nani kasema Maendeleo yanaletwa na Kitabu? Mbona Vitabu vya Dini tunavikiuka?

Katiba ni instrument inajiendesha kwa kupitia walioapa kuilinda. Ndiyo maana kwa marekani Rais anapokiuka senate haisubiri inakaa Ina frame case anaitwa kujieleza.

Na kuwa na mawazo kama hayo basi katiba kweli haileti maendeleo ila Ina filisi nchi.
 
Mtu aliyeapa kuilinda katiba, ameapishwa kwayo, leo anasema ni karatasi tu, kiukweli inafikirisha na anapaswa kujifikiria kama anatosha kwenye Hiyo nafasi.

Ni sawa na Shekhe au Pastor leo aseme Kur'an au Biblia ni Kitabu tu (Dharau), Kuidharau Katiba ni Kuwadharau Watanzania, Kuidharau Kur'an ni Kuwadharau Waislamu, na Kuidharau Biblia ni Kuwadharau Wakristo. Hiyo ni Kauli ya mtu asiyejua yupo kwaajili ya nini.
 
Kwa hiyo Rais Samia alitaka kusema nini?
Hakuna haja ya kuwa na vitabu vitakatifu au katiba?
Ukimwangalia wakati anahutubia ni wazi kabisa haonyeshi staha kwenye body language.

Vidole juu utafikiri yuko kwenye vikoba anamchamba mtu aliyeshindwa kurejesha marejesho.
 
Eti katiba ni kitabu hakileti maendeleo! Rais kafika mbali, kitabu anachokidharau ndio hicho kimemfanya awe Rais.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Jinsia yake haihusiki. Dini yake haihusiki. Sehemu ya Kijiografia anayotokea nayo haihusiki.

Kinachohusika hapa ni uwezo wake mdogo alionao.

Uwezo mdogo wa kiuongozi. Uwezo mdogo wa kuchanganua mambo. Na uwezo mdogo wa kujenga hoja.

Mara kadhaa sasa nimeona ona humu baadhi ya watu wakisema kwamba Rais Samia kaonyesha na kuthibitisha kuwa wanawake hawafai katika nafasi kiuongozi.

Mimi hilo nalikataa. Mtu mmoja mwenye uwezo mdogo si mwakilishi wa wanawake wote nchini wala duniani, kwa ujumla.

Uwezo wake mdogo alionao ni wa kwake yeye tu, Rais Samia.

Kilichonisukuma kuileta hii mada hapa ni yale maoni yake aliyoyatoa hapo jana.


View: https://youtu.be/O8SVrOeYtck?si=zAtsS1VP_q_B5Hmo
Rais anahoji kuwa kwani katiba ndo inaleta maendeleo?

Hivi huyu Rais hajui kuwa katiba ya nchi ndo framework ya uongozi na utawala ulio bora?

Bila uongozi na utawala ulio bora, kuna maendeleo gani yaliyo ya maana yanayoweza kupatikana?

Huo ni uwezo mdogo sana wa kufikiri ambao siutegemei utoke kwa kiongozi aliye wa juu kabisa nchini.

Au labda yeye anadhani maendeleo yanatoka wapi au yanakujaje?

Jingine la ajabu alilolizungumzia ni suala la elimu. Kwamba eti watu walio wengi hawajui hata katiba ni kitu gani. Hivyo ni lazima kwanza watu wapewe elimu kabla ya kuiandika hiyo katiba mpya.

Nilichoking’amua hapo ni ‘projection’ yake yeye kuhusu katiba.

Kulingana na kauli zake kuhusu katiba, nadhani yeye ndo hajui katiba ni kitu gani na hivyo anadhani hata wengine nao hawajui katiba ni nini!

Kenya waliandika katiba mpya mwaka 2010 [kama sijakosea].

Afrika Kusini waliandika katiba mpya baada ya kuachana na sheria za ubaguzi wa rangi kwenye miaka ya 90.

Marekani waliandika katiba yao miaka zaidi ya 200 iliyopita na ambayo wameifanyia marekebisho mara 27.

Sehemu nyingi tu duniani zimeandika katiba mpya na zingine kuzifanyia marekebisho katiba zilizopo.

Ni wapi ambako waliielimisha jamii kwanza kabla ya kuandika mpya?

Afrika Kusini walifanya elimu gani kwa wananchi kabla ya kuandika katiba yao mpya?

Waliwakalisha watu madarasani na kuanza kuwafundisha somo la katiba?

Katiba iliyopo sasa hivi wakati inaandikwa elimu ya katiba ilitolewa na nani? Lini? Wapi?

Naona sasa suala la kwamba wananchi hawana elimu ya katiba ndo litakuwa ‘narrative’ ya CCM kukwepa kujadili hoja za katiba mpya.

Kwa nilichokisikia jana, ni dhahiri shahiri kwamba anayehitaji elimu ya kujua katiba ni nini, ni Rais Samia.

Samia hafai kuwa Rais. Alichaguliwa kuwa mgombea mwenza kwa sababu zingine na si kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye uwezo unaofaa.

Tuna Rais bomu ambaye hafai kuwepo madarakani hata kwa sekunde moja.

Nadiriki kusema kuwa Samia ndo Rais bomu kushinda marais wote tuliowahi kuwa nao Tanzania.
 
Katiba ni nini?
Makaratasi asiyoyaheshimu Mwenyekiti wako, na kuyaona sawa na yale yanayotumika kule chooni. Hii ndiyo tafsiri yenu ya katiba.

CCM hiki kiburi na dharau sasa kimewafikisha pabaya. Ni kama akili zenu zimekwisha kabisa vichwani mwenu?

Mwenyekiti wa Chama na kiongozi wa nchi, anatoa hotuba ya namna ile mbele za watu, na kunakuwepo na watu wanashangilia kabisa na wengine kusifu kuwa ni hotuba bora kabisa ya mwezi wa September!
 
Acha wivu mbona jpm alisema katiba haileti Mvua n ukakubali?
 
Bora hata Majaliwa asinge kiheshimu kitabu alambe Urais.
 
Mama anahisi Katiba Mpya itamfutilia mbali kwenye uongozi. Hiyo hotuba uliyopachika anaongea kwa hasira sana na kapanic
 
Kumbe wewe ni miongoni mwa wasiojua maana ya katiba!
 
Shida ni uroho wa vyeo,wanajua umuhimu wa katiba lkn wanapindisha makusudi ili kundilao waenjoy keki ya taifa!! Shameless fyongozi.
Wajinga wakiskia tuu wanashedadia nakusifu unapigwa mwingi...
Tuchague viongozi wenyeupeo mkubwa na kufaulu vizuri,Hawa wa kuungaunga elimu hatutafika mahali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…