HOTUBA YA RAIS KWENYE UFUNGUZI WA KIKAO JANA: IMEACHA MASWALI MENGI KUHUSU KATIBA.
Mh. Rais yuko kwenye nafasi aliyopo kwasababu ya hiyo katiba, anawezaje kusema ni kitabu ambacho hakiwezi kuwaletea maendeleo wananchi, na kwamba hata vitabu vitakatifu havifuatwi!! Je, hicho kikao kinachoendelea ni kwa ajili ya kubatiza au kusilimisha watu? Kuna wengine ni wapagani na Imani tofauti hawana habari na hivyo vitabu vinavyoitwa vitakatifu, hao anawaweka kundi gani? Haya mambo ya Imani ni ya kuepukwa kwenye majukwaa ya siasa na kuacha mikononi mwa watu binafsi, Mashehe na Wachugaji.
Ni wanyama pekee wanaoweza kuishi bila kujiwekea utaratibu. Nchi nyingi uingia kwenye misukosuko na pengine serikali kuangushwa kwasababu ya kutokuheshimu hicho anachokiita kitabu. Na si kwamba nchi zilizoendelea hazina na wala hazifuati katiba eti kwasababu katiba haileti maendeleo. Siamini mtu kama Rais ambae alisha kuwa makamu mwenyekiti wa bunge la kutunga katiba anaweza kutamka haya maneno, lah sivyo ama ameshaanza kulewa madaraka au kuna force nyuma yake inayomfanya aogope hiyo katiba mpya.
Maswali ya kujiuliza, alikuwa akitafuta kitu gani hadi akawa makamu mwenyekiti ndani ya Bunge la katiba ili hali akijua ni kupoteza fedha na wakati? Akijua ni kitabu ambacho hakiwezi kuleta maendeleo? Akijua wananchi hawana uelewa na katiba, ni darasa lipi atakaloliandaa watu wafundishwe na kuilewa hiyo katiba? Anawezaje kukaa madarakani kwa katiba ambayo wanchi wake hawailewi? Je, viongozi watangulizi wake hasa JK, Warioba na tume yake ya katiba hawakuyaona haya au hawakuwa na ulewa kuhusu wananchi wa nchi hii. Katika hili Rais aje na sababu za maana kuliko kutusimanga juu ya uelewa wetu wa katiba.