Rais Samia: Nani kasema Maendeleo yanaletwa na Kitabu? Mbona Vitabu vya Dini tunavikiuka?

Rais Samia: Nani kasema Maendeleo yanaletwa na Kitabu? Mbona Vitabu vya Dini tunavikiuka?

Yy mwenyewe yuko pale kama Rais kwa mujibu wa katiba na katiba ndio inaongoza nchi kama hajui hilo basi ni bahati mbaya sana,na unajua hakuna mtu aliamini kama Rais anaweza kufa kirahis madarakani kumbe hata kuweka makamu walikuwa wanajiwekea tu bora liende.

Sasa nadhani funzo limepatikana sidhani kama makosa yatafanyika tena. Ndio maana unaona mtu ni Rais lkn hajui umuhimu wa katiba ni tatizo kubwa tena kubwa sana.
 
HOTUBA YA RAIS KWENYE UFUNGUZI WA KIKAO JANA: IMEACHA MASWALI MENGI KUHUSU KATIBA.

Mh. Rais yuko kwenye nafasi aliyopo kwasababu ya hiyo katiba, anawezaje kusema ni kitabu ambacho hakiwezi kuwaletea maendeleo wananchi, na kwamba hata vitabu vitakatifu havifuatwi!! Je, hicho kikao kinachoendelea ni kwa ajili ya kubatiza au kusilimisha watu? Kuna wengine ni wapagani na Imani tofauti hawana habari na hivyo vitabu vinavyoitwa vitakatifu, hao anawaweka kundi gani? Haya mambo ya Imani ni ya kuepukwa kwenye majukwaa ya siasa na kuacha mikononi mwa watu binafsi, Mashehe na Wachugaji.

Ni wanyama pekee wanaoweza kuishi bila kujiwekea utaratibu. Nchi nyingi uingia kwenye misukosuko na pengine serikali kuangushwa kwasababu ya kutokuheshimu hicho anachokiita kitabu. Na si kwamba nchi zilizoendelea hazina na wala hazifuati katiba eti kwasababu katiba haileti maendeleo. Siamini mtu kama Rais ambae alisha kuwa makamu mwenyekiti wa bunge la kutunga katiba anaweza kutamka haya maneno, lah sivyo ama ameshaanza kulewa madaraka au kuna force nyuma yake inayomfanya aogope hiyo katiba mpya.

Maswali ya kujiuliza, alikuwa akitafuta kitu gani hadi akawa makamu mwenyekiti ndani ya Bunge la katiba ili hali akijua ni kupoteza fedha na wakati? Akijua ni kitabu ambacho hakiwezi kuleta maendeleo? Akijua wananchi hawana uelewa na katiba, ni darasa lipi atakaloliandaa watu wafundishwe na kuilewa hiyo katiba? Anawezaje kukaa madarakani kwa katiba ambayo wanchi wake hawailewi? Je, viongozi watangulizi wake hasa JK, Warioba na tume yake ya katiba hawakuyaona haya au hawakuwa na ulewa kuhusu wananchi wa nchi hii. Katika hili Rais aje na sababu za maana kuliko kutusimanga juu ya uelewa wetu wa katiba.
 
Pale hakuna Rais ndugu yangu kwa yale aliyo yaongea jana watanzania wenye akili timamu wameelewa vzr kwamba tunaongozwa na mtu wa aina gani, nilimuona mzee wangu Joseph Sinde Warioba akiwa ktk mshangao mkuu na butwaa hasa kwa kile alichokuwa anasikiliza na zaidi kikitoka kwa mtu ambaye mzee warioba alimwamini.

Bila shaka mzee alijiuliza Hv kweli Rais anajua kwa nn yuko pale,na kama anajua,je ni kwa mujibu wake yy kama SAMIA au ni kwa mujibu wa katiba. Hao ndio viongozi wanaotuongoza hakika inafikirisha sana na kusikitisha pia.
 
Taifa linapitia kipindi kigumu sana. Rais ana halalisha ukanyagwaji wa katiba kwa reference ya ukanyagwaji vitabu vya dini akisema amelelewa kwenye maadili mema.

Maanake yanayofanyika chini ya utawala wake si lazima yazingatie katiba,ndiyo maana umakusudi wa kuingia mikataba isiyo na tija kwa wananchi Ina ukiukwaji Mkubwa wa katiba aliyoapa kuhifadhi na kuilinda.
 
Rais Samia amesema " Viongozi wa Kisiasa tunadhani tuna Haki ya kuburuza watu tunawageuza watu Makasuku, nenda kamuulize kifungu gani cha Katiba kinakuudhi, hajui sasa Katiba mpya ilete nini anakujibu Maendeleo tu, nani kasema Maendeleo yanaletwa na Kitabu? Kama kuheshimu Vitabu tungeheshimu Vitabu Vitakatifu, mbona Vitabu vya Dini tunavikiuka?"

Source: East Africa TV

Nimependa huu Ujumbe na utakuwa ndio Ujumbe bora wa mwezi September!
Yaani jana kama tungekuwa na kepteni jasiri kutoka jeshi la wananchi wa Tanzania basi leo angetangaza kuchukua nchi kwa maana Rais tulienae hakuapa kwa mujibu wa katiba aliapa kwa mujibu wake yy mwenyewe hivyo basi apatikane raisi atakayeapa kwa mujibu wa katiba na anatambua umuhimu wa kuapa kwa mujibu wa katiba lkn si huyu mama.
 
Rais Samia amesema " Viongozi wa Kisiasa tunadhani tuna Haki ya kuburuza watu tunawageuza watu Makasuku, nenda kamuulize kifungu gani cha Katiba kinakuudhi, hajui sasa Katiba mpya ilete nini anakujibu Maendeleo tu, nani kasema Maendeleo yanaletwa na Kitabu? Kama kuheshimu Vitabu tungeheshimu Vitabu Vitakatifu, mbona Vitabu vya Dini tunavikiuka?"

Source: East Africa TV

Nimependa huu Ujumbe na utakuwa ndio Ujumbe bora wa mwezi September!
Yeye kuunda serikali tu ina mshinda kuisimamia tu bandari anaona kama mlima kilimnajaro italuwa ni hiyo katiba
 
CHADEMA wamekariri kuwa ukiwa na Katiba Mpya tu maendeleo yanakuja yenyewe tu, hata hawajui wenyewe wana Mwenyekiti wao hataki kuachia Chama, anang'ang'ania tu hatoki, alafu wanadai Demokrasia CCM, wakati wao hawana hata demokrasia chamani kwao, CHADEMA nyoko sana, chama binafsi mali ya Mbowe family shida sana.
 
Kwani hivyo vitabu vya dini ni vitakatifu kwa kila mtu, ama ni kwa ajili ya kuleta maendeleo? Inaonekana yeye ndio hajui katiba, hivyo anadhani katiba ni muongozo wa mradi fulani wa uzalishaji mali.
Wamkumbushe kitabu kinachoitwa katiba ndiyo kimemfanya awe rais! Kweli Tanzania tumepata hasara. Ni aibu tupu kusema maneno ya kijinga kama haya yametoka kwenye kinywa cha rais wa nchi.
 
CHADEMA wamekariri kuwa ukiwa na Katiba Mpya tu maendeleo yanakuja yenyewe tu, hata hawajui wenyewe wana Mwenyekiti wao hataki kuachia Chama, anang'ang'ania tu hatoki, alafu wanadai Demokrasia CCM, wakati wao hawana hata demokrasia chamani kwao, CHADEMA nyoko sana, chama binafsi mali ya Mbowe family shida sana.
Nyie lini mlichagua mwenyekiti mbali na kuteua mtu mmoja.
 
Rais Samia amesema " Viongozi wa Kisiasa tunadhani tuna Haki ya kuburuza watu tunawageuza watu Makasuku, nenda kamuulize kifungu gani cha Katiba kinakuudhi, hajui sasa Katiba mpya ilete nini anakujibu Maendeleo tu, nani kasema Maendeleo yanaletwa na Kitabu? Kama kuheshimu Vitabu tungeheshimu Vitabu Vitakatifu, mbona Vitabu vya Dini tunavikiuka?"

Source: East Africa TV

Nimependa huu Ujumbe na utakuwa ndio Ujumbe bora wa mwezi September!
Hataki katiba mpya ,hiki chama lazima uwe na some sort of unafiki!
 
Ina sikitisha Makamu Mwenyekiti wa bunge la katiba hajui umuhimu wa katiba na hata alipokuwa Makamu hakujua wajibu wake nini
 
Inasikitisha sana kwa kiongozi wa nchi alieapa kuihifadhi na kulinda katiba akitoa kauli za kuidharau. Ni sawa na askofu kuidharau biblia au sheikh kuidharau Koran tukufu. Haishangazi kuona nchi inaendeshwa bila ya kufuata katiba.
 
Back
Top Bottom