Kuna tofauti kubwa sana kati ya kiongozi wa kuchaguliwa na kiongozi aliyekaimishwa madaraka kwa mujibu wa katiba.
Pamoja na mapungufu ya katiba ya 1977 iliyotoa mianya ya uvunjaji sheria na uporaji haki kwa wananchi,bado viongozi wanaaminika walichaguliwa bado waliheshimu katiba ya nchi,hawakuwahi kuikejeli. Nini kimekipata chama hiki CCM kutoa zao la katiba kuwa kejeli kwa katiba hiyo,huku wapambe wakishangilia na simanzi kubwa kwa wazee wa Taifa hili.
Je ni ulevi wa madaraka au kuyazoea madaraka na kuwapima wananchi ukomo wa mamlaka yao!?
Kwenye kongamano la vyama vya siasa na wadau wa demokrasia kauli za kuidharau katiba inayotambua uwepo wa taasisi zao Kuna pelela ujumbe gani kwao.
Ni kweli katiba iliyoitwa kitabu haileti maendeleo katika nchi na kama haileti kulikuwa na haja gani ya kuwa na katiba?
Je ni kweli kitabu hiki ni kwa ajili ya ethics na mambo mengine isipokuwa maendeleo ,na kama ndivyo hivyo kwani alikubali madaraka yaliyotokana na hicho kitabu.
Kama Rais haamini katika katiba,anakosa uhalali wa urais wake maana kapatikana kwa zao la katiba hiyo hiyo.
Ndiyo maana kwa hata mikataba tunayoingia kama nchi inaukiukwaji Mkubwa wa katiba yetu.
Kwa hili Rais anapaswa kujitafakari kama anastahili kuendelea kuwa Rais.