Rais Samia: Nani kasema Maendeleo yanaletwa na Kitabu? Mbona Vitabu vya Dini tunavikiuka?

Rais Samia: Nani kasema Maendeleo yanaletwa na Kitabu? Mbona Vitabu vya Dini tunavikiuka?

Rais Samia amesema " Viongozi wa Kisiasa tunadhani tuna Haki ya kuburuza watu tunawageuza watu Makasuku, nenda kamuulize kifungu gani cha Katiba kinakuudhi, hajui sasa Katiba mpya ilete nini anakujibu Maendeleo tu, nani kasema Maendeleo yanaletwa na Kitabu? Kama kuheshimu Vitabu tungeheshimu Vitabu Vitakatifu, mbona Vitabu vya Dini tunavikiuka?"

Source: East Africa TV

Nimependa huu Ujumbe na utakuwa ndio Ujumbe bora wa mwezi September!
Vitabu vya dini ni nadhalia , vya dunia hukum zake zipo wazi kiongozi akizingua
 
Hii quote haihusiani na hichi ninachoandika...

Umeongea kwa uchungu sana legend...na point tupu...

japo uko ughaibuni... unaonyesha nini maana ya uzalendo halisi.

Kiukweli Tanzania kama kuna janga kubwa lililowahi kutupata...

basi halizidi janga hili la kuwa na raisi wa hovyo! Kabisa tangu Taifa hili kuundwa.
Siku hizi sipo active sana humu.

Lakini baada ya kusizikia zile pumba jana, nikasema haiwezekani nikae tu kimya.

Yaani Rais mzima anasimama mbele ya hadhira na kuongea pumba tupu!

Hivi hii katiba iliyomfanya yeye awepo hapo alipo kwenye hiyo nafasi, wakati inaandikwa watu walipewa elimu gani? Nani aliwapa hiyo elimu? Na ulitumika utaratibu gani kutathmini watu wameipata hiyo elimu vya kutosha?

Na walimu wa hiyo elimu walikuwa akina nani?

Tuna Rais mwenye akili ambayo haitoshi kwenye hiyo nafasi….
 
Jana alidhihirisha alivyo kiazi 'bogus'

Hii katiba ya 1977 ilipoandikwa ilitolewa elimu kwa miaka yote ile (miaka 3)?

Na wananchi anaowadharau kuwa hawaijui katiba ya sasa ajue ndio waliokubali kumpokea kama raisi baada ya Magufuli kufariki...wangelikuwa hawaijui katiba ya sasa wasingelimpokea kuwa raisi baada ya kifo cha Magufuli 'wangelibisha kuwa makamu anapaswa kurithi madaraka ya uraisi'

Stupido! (say it in Luca voice)
Well Noted Mkuu!!!!
 
Kauli ya rais kuiita katiba " ni kitabu tu" inadhihirisha viapo wanavyoapa waingiapo madarakani si ya dhati toka moyoni. Rais anatakiwa kuilinda katiba kama asemavyo wakati wa kiapo.
Watanzania upo ulazima wa kuhakikisha kuwa katiba ijayo inatuwezesha kumfungulia mashitaka rais kwa kukiuka katiba ili katiba iheshimiwe na wananchi wote bila kujali vyeo.
Hii kauli ya uyu mama imeniumiza sana , sana , mpaka sasa naitafakari wala sipati jibu, kama kauli hii imewahi tolewa na moja ya watangulizi wake naomna mnijuze,
MUNGU LIVUSHE ILI TAIFA
 
Jibu swali Katiba ndio inaleta maendeleo? Vinginevyo ishia kuokota ma box huko huko hakuna Cha diaspora Tzn
Hebu muulize kwanza huyo sijui ndio mama yenu wa ukubwa kuwa "YUPO HAPO KWA KUPIGIWA KURA AU KATIBA?". Akikujibu muulize katiba ni nini na inatumikaje akikujibu haya utaona wewe au mtoa mada nani ni kiazi na huyo mama yenu asiyokuwa na maana.
 
Hii katiba, ndiyo iliyomsimika mama kuwa Rais wa JMT. Nafikiri aliteleza tu. Tuendelee kumuombea
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Jinsia yake haihusiki. Dini yake haihusiki. Sehemu ya Kijiografia anayotokea nayo haihusiki.

Kinachohusika hapa ni uwezo wake mdogo alionao.

Uwezo mdogo wa kiuongozi. Uwezo mdogo wa kuchanganua mambo. Na uwezo mdogo wa kujenga hoja.

Mara kadhaa sasa nimeona ona humu baadhi ya watu wakisema kwamba Rais Samia kaonyesha na kuthibitisha kuwa wanawake hawafai katika nafasi kiuongozi.

Mimi hilo nalikataa. Mtu mmoja mwenye uwezo mdogo si mwakilishi wa wanawake wote nchini wala duniani, kwa ujumla.

Uwezo wake mdogo alionao ni wa kwake yeye tu, Rais Samia.

Kilichonisukuma kuileta hii mada hapa ni yale maoni yake aliyoyatoa hapo jana.


View: https://youtu.be/O8SVrOeYtck?si=zAtsS1VP_q_B5Hmo

Rais anahoji kuwa kwani katiba ndo inaleta maendeleo?

Hivi huyu Rais hajui kuwa katiba ya nchi ndo framework ya uongozi na utawala ulio bora?

Bila uongozi na utawala ulio bora, kuna maendeleo gani yaliyo ya maana yanayoweza kupatikana?

Huo ni uwezo mdogo sana wa kufikiri ambao siutegemei utoke kwa kiongozi aliye wa juu kabisa nchini.

Au labda yeye anadhani maendeleo yanatoka wapi au yanakujaje?

Jingine la ajabu alilolizungumzia ni suala la elimu. Kwamba eti watu walio wengi hawajui hata katiba ni kitu gani. Hivyo ni lazima kwanza watu wapewe elimu kabla ya kuiandika hiyo katiba mpya.

Nilichoking’amua hapo ni ‘projection’ yake yeye kuhusu katiba.

Kulingana na kauli zake kuhusu katiba, nadhani yeye ndo hajui katiba ni kitu gani na hivyo anadhani hata wengine nao hawajui katiba ni nini!

Kenya waliandika katiba mpya mwaka 2010 [kama sijakosea].

Afrika Kusini waliandika katiba mpya baada ya kuachana na sheria za ubaguzi wa rangi kwenye miaka ya 90.

Marekani waliandika katiba yao miaka zaidi ya 200 iliyopita na ambayo wameifanyia marekebisho mara 27.

Sehemu nyingi tu duniani zimeandika katiba mpya na zingine kuzifanyia marekebisho katiba zilizopo.

Ni wapi ambako waliielimisha jamii kwanza kabla ya kuandika mpya?

Afrika Kusini walifanya elimu gani kwa wananchi kabla ya kuandika katiba yao mpya?

Waliwakalisha watu madarasani na kuanza kuwafundisha somo la katiba?

Katiba iliyopo sasa hivi wakati inaandikwa elimu ya katiba ilitolewa na nani? Lini? Wapi?

Naona sasa suala la kwamba wananchi hawana elimu ya katiba ndo litakuwa ‘narrative’ ya CCM kukwepa kujadili hoja za katiba mpya.

Kwa nilichokisikia jana, ni dhahiri shahiri kwamba anayehitaji elimu ya kujua katiba ni nini, ni Rais Samia.

Samia hafai kuwa Rais. Alichaguliwa kuwa mgombea mwenza kwa sababu zingine na si kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye uwezo unaofaa.

Tuna Rais bomu ambaye hafai kuwepo madarakani hata kwa sekunde moja.

Nadiriki kusema kuwa Samia ndo Rais bomu kushinda marais wote tuliowahi kuwa nao Tanzania.

Sawa, haya ni maoni Yako. Ila Samia Suluhu Hassan ndiye Raisi wa Tanzania kwa Sasa na kwa kadri Watanzania walio wengi watakavyoamua, ataendelea tena Hadi 2030.

Hamia au endelea kuishi Huko kwa hao ambao hawana Raisi Bomu.
 
Nafikir Rais anadanganywa na alioamua kuwaamini.

She's been cheated by some crooks, sidhanj kama ni uwezo perse.

Kumbuka wengi wao hawakushinda uchaguzi.. akiwemo Spika wa Bunge wa sasa ndugu Tulia Ackson.
Wizi wa kura unawafanya wawe na hofu sana ya Katiba mpya.
Nchi hii bado ina viongozi wasioamini katika uchaguzi, na ni wengi sana huko CCM.

Sasa hivi wamehama kabisa, wanataka na wake zao na waume zao walipwe mishahara.. how disgraceful they can be.

Utawala wa CCM Tanzania wamebaki kwenye wizi wa kura huku wakihubiri amani...

Wizi wa kura kwa kipindi cha 2025 hata kwa katiba hii mbovu ni suala lisilowezekana asilani.... it's an old story.... it's either wanaotaka Kumkwamisha wafanye hivyo mapema tujue moja au aendelee na watu wanaomdanganya kwenda kwenye uchaguzi bila muafaka na CDM.

Kifupi Mama anadanganywa na wezi wa uchaguzi, mambo mengi mno kuanzia uchumi na sasa hili la Katiba.. so sad.
Hata wewe hujui maana ya katiba Mpya kwa nchi yetu! Laiti ungejua, usingemuona mama hajui.

Naona kama amefuzu sawa na JK pale alipoifutilia mbali hoja ya katiba Mpya.

Kwa kukusaidia, lengo kuu la katiba Mpya ni kuondoa madaraka makubwa ya Rais. Fikiria Nani anaweza kukubali wakati ashasema 2025 anagombea!!!!! Hivi nani hajui kuwa CCM inashinda kwa kuiba kura? Akubali uchaguzi huru ili awe mpinzani?

Kweli hamjui maana ya katiba Mpya tukubaliane
 
Naona sasa suala la kwamba wananchi hawana elimu ya katiba ndo litakuwa ‘narrative’ ya CCM kukwepa kujadili hoja za katiba mpya.
Ccm inatumia "wana.nchi wapate elimu kwanza juu ya katiba" kama chaka la kukwepea kuandika katiba mpya. Kwasbb wanajua katiba mpya ikiandikwa hawana chao.

Yapo makurumbembe ndani ya ccm yamekuwa yakipora utashi wa kila rais anayetaka katiba mpya na yanafanikiwa kumpindisha. Tuliyaona kwa Kikwete na Sasa tunayaona kwa Samia
 
Sawa, haya ni maoni Yako. Ila Samia Suluhu Hassan ndiye Raisi wa Tanzania kwa Sasa na kwa kadri Watanzania walio wengi watakavyoamua, ataendelea tena Hadi 2030.

Hamia au endelea kuishi Huko kwa hao ambao hawana Raisi Bomu.
Kwenye uchaguzi ulio wa huru na haki, Samia hatoboi.
 
Hebu muulize kwanza huyo sijui ndio mama yenu wa ukubwa kuwa "YUPO HAPO KWA KUPIGIWA KURA AU KATIBA?". Akikujibu muulize katiba ni nini na inatumikaje akikujibu haya utaona wewe au mtoa mada nani ni kiazi na huyo mama yenu asiyokuwa na maana.
Katiba
 
Back
Top Bottom