Kwako mama yetu Samia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Natumai umzima wa afya njema na unaendelea na shughuli zako za kiofisi.
Mama, ndugu yetu Elia Wilinasi ni kijana safi mwenye weledi na mzalendo anayetamani kukitumikia chama cha mapinduzi katika ngazi za juu na taifa kwa ujumla.
Alichukua fomu ya kugombea ujumbe wa hamshauri kuu ya CCM taifa kama karata yake ya kwanza kulitumikia taifa lake.
Safari hii anasubiria mkeka wa ukuu wa wilaya kwa hamu, bado anatamani kulitumikia taifa katika ngazi ya ukuu wa wilaya.
Ahsante sana.
Kazi iendelee
KUVAA VIZURI NA KUJICHEKESHA HOVYO SIO ISHARA YA UELEWA.
Wanaccm ni lazima tujikumbushe kila mara
Tuna jukumu la kuiongoza nchi hii na kuisimamia Serikali ili iweze kuitekeleza ilani ya CCM 2020 ambayo ni
mkataba Kati yetu CCM na Wananchi.
Ili tufanikiwe ni lazima tuwachague Viongozi wenye Uelewa Mpana na wenye Maono Makubwa.
Viongozi Aina hiyo tunao wengi nchini ila maisha wanayoyaishi wamezungukwa na watu walio wengi
wajinga kabisa ambao nyakati za
Uchaguzi huleta mizaha na ushabiki wa kipumbavu ambao Matokeo ya hayo hupelekea kupenya watu wasio na sifa za Uongozi na Matokeo yake Viongozi hao
Maboya huonekana vituko mbele ya Viongozi wa Serikali ambao Viongozi hao wa Serikali Daima Wana
viapo vya
uhakika na hulazimika kuishi wakisimamiwa na baadhi ya Viongozi wenye Uelewa Mdogo ambao viapo vyao huwa ni
Danganya toto .
Pia history ya baadhi ya Viongozi wa Chama husomeka walivyopatikana kwa
Rushwa ila wao huwa
Makauzu hujitoa *
Ufahamu na kujifanya na wao wanakemea*
Rushwa ilihali wao wametokana na Rushwa.
Ifikie Mahali Wanaccm tujielewe tuache kutumika na kushangilia Mambo ya hovyo hovyo.
Wasomi wa Serikalini baadhi
wanatushangaa na wanasikitika hata
Post tunazo Post kwenye Magroup hasa kwa kuzingatia Sisi ndiyo watawala.
Ni lazima Sasa tuanze kuwakabili watu
wajinga wajinga pale
wanapopotosha Raia
NI kwa kufanya hivi tutakuwa pia tunayatekeleza Mapenzi ya Mwenyezi Mungu anayetutaka kutumia Uelewa wetu kuwasaidia wasio
jielewa.
Nakumbuka Tarehe 22/08/2021
Askofu Dkt Josephat Gwajima alisema,
" Mimi kumkabili mtu Mjinga Mjinga , nimeambiwa hivyo na Mungu.
Akitokea mtu Mjinga Mjinga
mkabili hasa
anayechezea Mungu na nguvu zake..
Wanaccm
tukibahatika tukakuza
Uelewa tukakataa kutumikishwa na kufikiri kwa mizani ya njaa zetu naamini kabisa hata Sisi hatutakuwa Omba Omba na kuishi kwa kutegemea huruma za Viongozi Baadhi walio kwenye Vyombo vya Dola ambao wakinuna TU Sisi huku na familia zetu tunachanganyikiwa na kutafuta umbea wa kuwapelekea ili wacheke walau kidogo ili nasi familia zichangamke.
π€π€π€π€π€π€π€
Tubadilike turudi kwenye malengo mapana ambayo Wananchi wenzetu Makapuku wenzetu walituamini na tukakubaliana nao kupitia ilani.
Nakumbuka Tarehe 07 / July/2021
Comrade Kanali Mstaafu
Mheshimiwa Ngemela Lubinga .
Katibu NEC Siasa na Mahisiano ya Kimataifa
Alisema,
" Kazi kubwa tunayokuja kufanya ni
kusimamia ilani kwamba tulipoingia
Madarakani tuliwaomba Wananchi kura .
Tukisema tutatekeleza hili tutatekeleza hili, tutatekeleza hili, Sasa tunataka
kuona je, hayo yanatekelezwa?"
Mwisho wa kunukuu
Tusome Kitabu cha Ilani ya CCM 2020 uk 01 ibara 04 na uk 161-168.
Ili Mambo yaende ni lazima Muhali tuuweke pembeni , tuchukuwe kila hatua
inayostahiki ikiwa ni Pamoja na kuto
wachagua Viongozi wenye Uelewa
Mdogo
Ambao baadhi yao wanapenya kwa Rushwa Kisha kulindwa kwa nguvu zote na baadhi ya Viongozi Wasio Waadilifu kwa visingizio vya kikao ambavyo hufanya Maamuzi vikiwa na Chuki Binafsi na Mitazamo hasi uliogandana na
Uelewa finyu .
Katiba Kanuni Miongozo na Taratibu zetu zinaelekeza wazi na ziko wazi ila zinasiginwa kwa sababu ya baadhi ya Viongozi wetu walio na Uelewa finyu ambao baadhi yao walipata Uongozi huo kwa
Rushwa na walio kosa lishe kwenye ubongo wao.
Watu wameelekezwa Sana watende haki kwa kufuata katiba Kanuni Miongozo na Taratibu ila kwa ukosefu wa lishe baadhi wamekuwa wakifikiri kwa kuwaza matumbo yao. NA faida wajipatazo kwa Rushwa ya kuwapitisha Wagombea Maboya kwa Maelekezo ya Viongozi wenye Fedha na kuwakata wote wenye Uelewa Mpana na ambao wangukuwa chachu ya kukiimarisha Chama.
Nakumbuka Tarehe 30/09/2022
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan
Katika Mkutano wa Mwaka wa Tathmin ya Sita ya mkataba wa lishe September 30, 2022
Alisema,
" Ndiyo Yale aliyoyasema , nadhani Waziri Ummy,
tunagombana huko TAMISEMI huko Chini, hata huko juu Serikalini.
Unamuelekeza mtu kitu mara nne , mara tano,hata
hakimuingii.
Unamuuliza Dharau !?,
Jeuri !?, Hutaki !?
Kumbe
Maskini hujuwi historia
yake.
History yake imefichwa na
suti na
tai aliyoivaa.
Inawezekana kabisa maanake unasema ahaa, mbona mi naona hapa Kuna
tatizo!?"
"Naona (Matatizo) moja , mbili, tatu, hivi inakuwaje huyu niliyemuamini hapa (Yeye haoni )!?"
"Haoni"
"Haiwezekani"
" Kumbe Kuna hayo ( ya Uelewa Mdogo na ukosefu wa lishe)"
"Tuna watu lakini sio Raslimali watu."
Mwisho wa kunukuu
Naye Pastor Mmbaga
Wa Mahubiri TV
Tarehe 26/12/2020
Aliwahi kusema,
"Sasa mnisamehe Sana
Kama hii sentence
itawakwaza"
" Kuna watu
mtaishia kuwa
Wapishi wa (watu) wengine (kwa) maana
hamjiongezi
"(Kwa sababu ya )
Ufahamu (Mdogo)"
" Pata Maarifa , na kinachozuia
tusipate Ufahamu ni ka Roho kale ka Nini!?
"Wivu ,
korosho "
" Yaani korosho ilivyo tamu lakini watu
wakasema eti ( mtu) ana Roho ya korosho wakati korosho NI tamu!?"
Tubadilishe TU , tuite (Roho) ya
ndoano ".
Mwisho wa kunukuu
Tuzaliwe Upya
Kifikra Uongozi sio kuvaa nguo zilizo kolea kijani na nyeusi huku tukiwa
hatujielewi tunatumikishwa na kujionyesha kuwaponda wanaotupatia Uelewa ili tukalipwe vihera kwa wenye hela za Rushwa.
Tusome Kitabu cha Katiba ya CCM 1977 Toleo 2020 ibara 15(3)(4)(6)(7) , Ibara 12(1)(a) ili tukasome uk 151 vifungu 1,3,6 na 8.
Nakumbuka Tarehe 28/10/2021
Comrade Humphrey Polepole
Akiwa Mbunge
Aliwahi kusema,
" Leadership is the ability to develop a
Vision that
motivate others to move with a passion towards a common goal."
Mwisho wa kunukuu.
Tuache kucheka check kwenye Mambo yanayoweza kuathiri jitihada za kulisongesha Taifa letu mbele.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Mathias Mugerwa Kahinga