Rais Samia ni dereva hodari, shupavu jasiri na mahiri wa taifa letu, Watanzania waridhishwa na kasi yake

Rais Samia ni dereva hodari, shupavu jasiri na mahiri wa taifa letu, Watanzania waridhishwa na kasi yake

Mamilioni ya watanzania wameridhishwa na Kasi ya kiutendaji ya mh Rais katika kupiga hatua za kimaendeleo kwa Taifa letu, watanzania wameridhishwa na mikakati ya mh Rais katika kukabiliana na changamoto zinazojitokeza mbele yetu, watanzania wameridhishwa na dhamira njema ya mh Rais katika kuijenga nchi yetu na kuipeleka mbele kimaendeleo
Chief usijitoe ufahamu kwa ajili ya tumbo lako kwa tamaa za uteuzi.
Wewe na familia yako hamuwakilishi taifa zima.
Kama kipimo cha kujenga nchi ni kufanya kila kitu kuwa kigumu basi kwa hakika amefanikiwa.
Ndani ya nafsi unajua fika kuwa han dira wala muelekeo ila kwa vile umesikia kasema anataka kila mtu asupport maono yako (yasiyokuwepo) basi na wewe umejitoa ufahamu kusifia visivyokuwepo.
Umeweka jina na namba ya simu kwa matumaini kuwa atakutafuta. Sasa kwa taarifa yako watakaotufuta ni wazee wa tuma kwa namba hii na matangazo ya waganga wa kienyeji pekee.
 
Hizi porojo za kiccm ni toka enzi za Nyerere na hali inazidi kuwa mbaya, udhibitisho ni huu mgao wa umeme na maji.
Tambua kuwa Hata idadi yetu inaongezeka kila Siku na kila mwaka hivyo Mahitaji nayo lazima yaongezeke na kupelekea kuongezeka kwa baadhi ya changamoto ambazo serikali yetu inakuwa inapambana nazo kuzimaliza, embu fikria kuwa tulipokuwa tunapata Uhuru tulikuwa millini 12 na point lakini Leo hii tupo million 61 na laki Saba, je huoni kuwa hata changamoto lazima ziongezeka kulingana na mahitaji ya watu kuongezeka
 
Ndugu Zangu Hivyo Ndivyo unavyoweza kusema kuwa Rais Mama Samia Ni Dereva Mahiri na shupavu Sana katika kuliendesha gari hili la Safari ya maendeleo ya Tanzania, Ni dereva Ambaye ameonyesha umaridadi na uzoefu wa kuendesha gari,ameonyesha umakini mkubwa katika safari,ameonyesha kuwajari abiria wake,ameonyesha usikivu,unyenyekevu ,busara ,hekima na upendo mkubwa Sana kwa abiria wake.

Ameonyesha kufahamu na kutambua kuwa amebeba Roho za watu na siyo wanyama,ameonyesha kutambua umuhimu wa Roho alizozibeba ndani ya gari yake, ameonyesha kutambua kuwa Roho zote zipo mikononi mwake,ameonyesha kutambua kuwa kosa dogo na moja linaweza hitimisha uhai wa abiria wake, ameonesha kutambua kuwa uhai wa Mwanadamu haununuliwi kwa Fedha ya aina yoyote Ile, Rais Samia amekidhi kiu ya abiria wake,amewaondolea hofu na Mashaka,Amewapa matumaini ya kufika salama bila uchovu Wala hofu,hakuna aliyeshika Roho mikononi maana Dereva ameonyesha kuzifahamu vyema njia aipitayo na mahali anakokwenda

Mwendo ni wakuridhisha, sauti za abiria Ni za furaha na amani,maongezi ya abiria Ni pongezi na sifa kwa Dereva wao,kwa hakika Hakuna mwenye kutamani kushuka,Hakuna mwenye kutamani kupanda gari jingine,hakuna mwenye kujuta na safari,Hakuna mwenye kujutia Nauli yake,hakuna mwenye kujilaumu kusafiri naye.

Kila abiria anatamani kupanda gari hili Tena, kila abiria anamuombea Maisha marefu na Afya njema Dereva huyu.

Tanzania Ni Gari aiongozayo na kuliendesha mama Samia,Hakuna anayejuta kuzaliwa Tanzania kwa Sasa,hakuna anayetamani kuhama Tanzania kwa Sasa, Hakuna anayehofu juu ya kesho yake ndani ya Tanzania, Kwa sasa Tanzania Ni nchi inayotoa matumaini kwa kila mtanzania mwenye kutumia fursa za kiuchumi zilizopo, Ni nchi inayomiminisha fursa kila mahali, Ni nchi ambayo kwa Sasa Ni Tumaini kwa wanyonge katika kuinuka kiuchumi, Ni nchi na mahali palipo salama kwa kila mmoja wetu kusonga mbele na kupiga hatua za kimaendeleo.

Rais Samia anazidi kuchanja mbuga katika mioyo ya watanzania, anazidi kueleweka na watanzania, Anaendelea kukubalika na watanzania kwa kuwa ameonyesha kuyatambua matatizo na kero za watanzania na kuwa Tayari kupambana nazo,Ameonyesha uzalendo kimaneno na kimatendo katika kuwatumikia watanzania,ameonyesha Ushupavu na ujasiri katika kuliongoza Taifa letu, ametupatia matumaini ya kesho iliyo Bora Zaidi ya leo

Watanzania Tuendelee kumuunga mkono mh Rais wetu, Tuendelee kumwombea Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia, Tuendelee kuwa naye bega kwa bega, Tuendelee kumpa faraja na kumtia moyo mama yetu, Tuendelee kusimama Naye katika Hatua zote za ujenzi wa Taifa letu , Tuendelee kumpa ushirikiano na kuonyesha upendo kwake Kama anavyoonesha kwetu watanzania.

Watanzania Tutambue na kufahamu kuwa viongozi aina ya Rais Samia Hawazaliwi kila Siku na hawapatikani kila mahali, Viongozi Wa aina yake wenye upendo,uzalendo kwa nchi zao huwa Ni nadra sana Sana kuwapata. Watanzania Tumepata bahati ya kumpata Mama Samia. Ambaye ameonyesha ujasiri, uzalendo,ushupavu na umahili katika kuliongoza Taifa hili, Amelibeba Taifa hili kwa moyo wake wote katika mabega take kuhakikisha kuwa analifikisha salama na mbele zaidi kimaendeleo mahali ambapo kila mtanzania ataguswa kiuchumi nakuondoka katika umaskini wa kipato.

Kazi iendeleee,mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627
Nawewe ni mkulima au WEWE mlamba asari?
 
Huo Ni mtizamo wako tu mkuu, lakini Tambua kuwa mioyo ya wakulima wa Tanzania kwa Sasa Ina amani Sana na Rais Samia
Wazungu wanasema picha inaongea maneno buku hao wakulima na mabango yao hawaonekani kama watu wenye amani mioyoni mwao kwani hata kupauka wamepauka wanaisoma namba hawawezi kusmile.
 
Chief usijitoe ufahamu kwa ajili ya tumbo lako kwa tamaa za uteuzi.
Wewe na familia yako hamuwakilishi taifa zima.
Kama kipimo cha kujenga nchi ni kufanya kila kitu kuwa kigumu basi kwa hakika amefanikiwa.
Ndani ya nafsi unajua fika kuwa han dira wala muelekeo ila kwa vile umesikia kasema anataka kila mtu asupport maono yako (yasiyokuwepo) basi na wewe umejitoa ufahamu kusifia visivyokuwepo.
Umeweka jina na namba ya simu kwa matumaini kuwa atakutafuta. Sasa kwa taarifa yako watakaotufuta ni wazee wa tuma kwa namba hii na matangazo ya waganga wa kienyeji pekee.
Rais wetu anamuelekeo na dira inayoeleweka katika kuliongoza taifa hili,anafahamu wapi tumetoka na wapi tunapaswa kuelekea, anafahamu Mahitaji ya watanzania ,Anayo mikakati ya kuhakikisha kero mbalimbali zinamalizwa na kuleta mwanga katika maisha ya watanzania
 
Wazungu wanasema picha inaongea maneno buku hao wakulima na mabango yao hawaonekani kama watu wenye amani mioyoni mwao kwani hata kupauka wamepauka wanaisoma namba hawawezi kusmile.
Wanamatumaini ya kesho yao kuwa njema kwa kuwa wanatambua mikakati ya serikali yao kuwainua kiuchumi kupitia kilimo na kauli mbiu ya kilimo Ni biashara,ambapo kwa Sasa kilimo Ni biashara inayolipa na inayotoa matumaini kwa wakulima wengi kujikwamua kiuchumi
 
Rais wetu anamuelekeo na dira inayoeleweka katika kuliongoza taifa hili,anafahamu wapi tumetoka na wapi tunapaswa kuelekea, anafahamu Mahitaji ya watanzania ,Anayo mikakati ya kuhakikisha kero mbalimbali zinamalizwa na kuleta mwanga katika maisha ya watanzania
Siku zote kipimo cha uanaume wa mtu ni uwezo wa kulinda utu wake hata ikiwa hana kitu.
Wewe kwa tamaa ya teuzi unautoa utu wako kwa kuhubiri vitu ambavyo hata kipofu anaviona.
Ukute una dhiki mpaka kwenye unyayo (kupelekea kutarajia teuzi kuwa pona yako) halafu uko hapa unaandika upuuzi ili tu uonekane na mtu ambae hatokuja kukaa akakuona.
Muda unaotumia kuandika huu upuuzi bora hata ungekaa kutafakari njia za kujikwamua kimaisha.
 
Embu rudia kusoma halafu uniambie mahali nilipozungumzia habari za uteuzi
 
Mimi Ni mkulima ambapo jembe langu ndio kalamu yangu na Shamba langu ndio daftari langu huku mabega yangu yakiwa ndio begi langu kubebwa jembe langu
Lini unaandamana kumpongeza mama tozo Kwa kuweka tozo mpaka Kwa wanawake wa kimboka?
 
Basi sawa
6DD6B40D-9652-47D9-AFF3-451F8E94C6FE.jpeg
 
Unaweza kukuta huyu mtoa mada ni baba wa familia na anategemewa kuiongoza familia yake na kuwapa ushauri........
 
Back
Top Bottom