Rais Samia ni dereva hodari, shupavu jasiri na mahiri wa taifa letu, Watanzania waridhishwa na kasi yake

Ana usomi gani huyo naye mbona unampa sifa asiyostahili,hao ni vijana wa ovyo wa bongo daslam wenye tamaa za kifisi ambao wanakamatia kila fursa inayokuja mbele yao,uhandishi wa habari,uwakili,uanasheria,udalali,uchawa,ukuadi,wizi ilimradi mkono uende kinywani .ogopa sana watu wa namna hiyo na kwa jinsi kulivyo na urasimu katika nchi yetu ndio watu wa namna hii wamejaa huko juu eti wanatuongoza na matokeo yake ni nchi iko katika umasikini wa kutisha hadi leo hii.
Gombea uongozi ili uje utuongoze na uone Kama utachaguliwa kwa Sera zako hizo za matusi
 
Tambua kuwa Hata idadi yetu inaongezeka kila Siku na kila mwaka hivyo Mahitaji nayo lazima yaongezeke na kupelekea kuongezeka kwa baadhi ya changamoto ambazo serikali yetu inakuwa inapambana nazo kuzimaliza, embu fikria kuwa tulipokuwa tunapata Uhuru tulikuwa millini 12 na point lakini Leo hii tupo million 61 na laki Saba, je huoni kuwa hata changamoto lazima ziongezeka kulingana na mahitaji ya watu kuongezeka

Kama kuongezeka kwa watu ndio kunaleta changamoto za mgao wa umeme, basi China ilitakiwa iwe gizani jumla.
 
Gombea uongozi ili uje utuongoze na uone Kama utachaguliwa kwa Sera zako hizo za matusi
Serikali yako inayoendeshwa kijuha ndio imesababisha niongee maneno makali kuwakilisha watanzania walio wengi wenye hasira na mgao wa umeme unaoendelea nchini,mimi ni mfanyabiashara wa samaki wabichi unajua hasara niliyopata mpaka sasa kutokana na kukatika umeme!!!??? Muda sio mrefu nitafunga biashara kwa kufirisika unadhani hiyo serikali yenu ya majambazi itanisaidia nini na familia yangu!!!!! MKITAKA TUSITUMIE LUGHA KALI HEBU KUWENI NA HURUMA NA WATANZANIA WENZENU
 
Ndugu Zangu Hivyo Ndivyo unavyoweza kusema kuwa Rais Mama Samia Ni Dereva Mahiri na shupavu Sana katika kuliendesha gari hili la Safari ya maendeleo ya Tanzania, Ni dereva Ambaye ameonyesha umaridadi na uzoefu wa kuendesha gari,ameonyesha umakini mkubwa katika safari,ameonyesha kuwajari abiria wake,ameonyesha usikivu,unyenyekevu ,busara ,hekima na upendo mkubwa Sana kwa abiria wake.

Ameonyesha kufahamu na kutambua kuwa amebeba Roho za watu na siyo wanyama,ameonyesha kutambua umuhimu wa Roho alizozibeba ndani ya gari yake, ameonyesha kutambua kuwa Roho zote zipo mikononi mwake,ameonyesha kutambua kuwa kosa dogo na moja linaweza hitimisha uhai wa abiria wake, ameonesha kutambua kuwa uhai wa Mwanadamu haununuliwi kwa Fedha ya aina yoyote Ile, Rais Samia amekidhi kiu ya abiria wake,amewaondolea hofu na Mashaka,Amewapa matumaini ya kufika salama bila uchovu Wala hofu,hakuna aliyeshika Roho mikononi maana Dereva ameonyesha kuzifahamu vyema njia aipitayo na mahali anakokwenda

Mwendo ni wakuridhisha, sauti za abiria Ni za furaha na amani,maongezi ya abiria Ni pongezi na sifa kwa Dereva wao,kwa hakika Hakuna mwenye kutamani kushuka,Hakuna mwenye kutamani kupanda gari jingine,hakuna mwenye kujuta na safari,Hakuna mwenye kujutia Nauli yake,hakuna mwenye kujilaumu kusafiri naye.

Kila abiria anatamani kupanda gari hili Tena, kila abiria anamuombea Maisha marefu na Afya njema Dereva huyu.

Tanzania Ni Gari aiongozayo na kuliendesha mama Samia,Hakuna anayejuta kuzaliwa Tanzania kwa Sasa,hakuna anayetamani kuhama Tanzania kwa Sasa, Hakuna anayehofu juu ya kesho yake ndani ya Tanzania, Kwa sasa Tanzania Ni nchi inayotoa matumaini kwa kila mtanzania mwenye kutumia fursa za kiuchumi zilizopo, Ni nchi inayomiminisha fursa kila mahali, Ni nchi ambayo kwa Sasa Ni Tumaini kwa wanyonge katika kuinuka kiuchumi, Ni nchi na mahali palipo salama kwa kila mmoja wetu kusonga mbele na kupiga hatua za kimaendeleo.

Rais Samia anazidi kuchanja mbuga katika mioyo ya watanzania, anazidi kueleweka na watanzania, Anaendelea kukubalika na watanzania kwa kuwa ameonyesha kuyatambua matatizo na kero za watanzania na kuwa Tayari kupambana nazo,Ameonyesha uzalendo kimaneno na kimatendo katika kuwatumikia watanzania,ameonyesha Ushupavu na ujasiri katika kuliongoza Taifa letu, ametupatia matumaini ya kesho iliyo Bora Zaidi ya leo

Watanzania Tuendelee kumuunga mkono mh Rais wetu, Tuendelee kumwombea Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia, Tuendelee kuwa naye bega kwa bega, Tuendelee kumpa faraja na kumtia moyo mama yetu, Tuendelee kusimama Naye katika Hatua zote za ujenzi wa Taifa letu , Tuendelee kumpa ushirikiano na kuonyesha upendo kwake Kama anavyoonesha kwetu watanzania.

Watanzania Tutambue na kufahamu kuwa viongozi aina ya Rais Samia Hawazaliwi kila Siku na hawapatikani kila mahali, Viongozi Wa aina yake wenye upendo,uzalendo kwa nchi zao huwa Ni nadra sana Sana kuwapata. Watanzania Tumepata bahati ya kumpata Mama Samia. Ambaye ameonyesha ujasiri, uzalendo,ushupavu na umahili katika kuliongoza Taifa hili, Amelibeba Taifa hili kwa moyo wake wote katika mabega take kuhakikisha kuwa analifikisha salama na mbele zaidi kimaendeleo mahali ambapo kila mtanzania ataguswa kiuchumi nakuondoka katika umaskini wa kipato.

Kazi iendeleee,mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627
Nawewe umetoa lamoyoni linalo kunyima usingizi Asante Kwa mapambio
 
Serikali yako inayoendeshwa kijuha ndio imesababisha niongee maneno makali kuwakilisha watanzania walio wengi wenye hasira na mgao wa umeme unaoendelea nchini,mimi ni mfanyabiashara wa samaki wabichi unajua hasara niliyopata mpaka sasa kutokana na kukatika umeme!!!??? Muda sio mrefu nitafunga biashara kwa kufirisika unadhani hiyo serikali yenu ya majambazi itanisaidia nini na familia yangu!!!!! MKITAKA TUSITUMIE LUGHA KALI HEBU KUWENI NA HURUMA NA WATANZANIA WENZENU
Iamini serikali yetu mkuu maana inatambua yote hayo ya hasara ndio maana unaona ikiweka mikakati ya kutumia vyanzo vingine kuzalisha umeme vitakavyosaidia kupunguza changamoto hii ya umeme, umeongea kwa uchungu lakini naomba uwe na Imani na mh Rais wetu maana amedhamiria kulimaliza tatizo hili kwa kuchukua hatua za muda mfupi wa Kati na mrefu
 
Kwa hiyo unafikiri mvua haitanyesha? Mimi niliko mvua imeshaanza kunyesha na tayari tunaendelea kupanda
Miaka 60 bado tunategemea mvua pekee ndo imuokoe Mtanzania?, kweli?.
Umerogwa ww na huyo ndg yako.
Ole wenu kuwe na katiba mpya uone km ccm watapita!...
 
CCM itapita,CCM itachaguliwa ten,CCM itapigiwa Kura za Ndio,CCM itaungwa mkono ,CCM utapewa Ridhaa ya kuunda serikali kwa kuwa Ni chama chenye Sera na ajenda zinazogusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti
 
Ndugu Zangu Hivyo Ndivyo unavyoweza kusema kuwa Rais Mama Samia Ni Dereva Mahiri na shupavu Sana katika kuliendesha gari hili la Safari ya maendeleo ya Tanzania, Ni dereva Ambaye ameonyesha umaridadi na uzoefu wa kuendesha gari,ameonyesha umakini mkubwa katika safari,ameonyesha kuwajari abiria wake,ameonyesha usikivu,unyenyekevu ,busara ,hekima na upendo mkubwa Sana kwa abiria wake.

Ameonyesha kufahamu na kutambua kuwa amebeba Roho za watu na siyo wanyama,ameonyesha kutambua umuhimu wa Roho alizozibeba ndani ya gari yake, ameonyesha kutambua kuwa Roho zote zipo mikononi mwake,ameonyesha kutambua kuwa kosa dogo na moja linaweza hitimisha uhai wa abiria wake, ameonesha kutambua kuwa uhai wa Mwanadamu haununuliwi kwa Fedha ya aina yoyote Ile, Rais Samia amekidhi kiu ya abiria wake,amewaondolea hofu na Mashaka,Amewapa matumaini ya kufika salama bila uchovu Wala hofu,hakuna aliyeshika Roho mikononi maana Dereva ameonyesha kuzifahamu vyema njia aipitayo na mahali anakokwenda

Mwendo ni wakuridhisha, sauti za abiria Ni za furaha na amani,maongezi ya abiria Ni pongezi na sifa kwa Dereva wao,kwa hakika Hakuna mwenye kutamani kushuka,Hakuna mwenye kutamani kupanda gari jingine,hakuna mwenye kujuta na safari,Hakuna mwenye kujutia Nauli yake,hakuna mwenye kujilaumu kusafiri naye.

Kila abiria anatamani kupanda gari hili Tena, kila abiria anamuombea Maisha marefu na Afya njema Dereva huyu.

Tanzania Ni Gari aiongozayo na kuliendesha mama Samia,Hakuna anayejuta kuzaliwa Tanzania kwa Sasa,hakuna anayetamani kuhama Tanzania kwa Sasa, Hakuna anayehofu juu ya kesho yake ndani ya Tanzania, Kwa sasa Tanzania Ni nchi inayotoa matumaini kwa kila mtanzania mwenye kutumia fursa za kiuchumi zilizopo, Ni nchi inayomiminisha fursa kila mahali, Ni nchi ambayo kwa Sasa Ni Tumaini kwa wanyonge katika kuinuka kiuchumi, Ni nchi na mahali palipo salama kwa kila mmoja wetu kusonga mbele na kupiga hatua za kimaendeleo.

Rais Samia anazidi kuchanja mbuga katika mioyo ya watanzania, anazidi kueleweka na watanzania, Anaendelea kukubalika na watanzania kwa kuwa ameonyesha kuyatambua matatizo na kero za watanzania na kuwa Tayari kupambana nazo,Ameonyesha uzalendo kimaneno na kimatendo katika kuwatumikia watanzania,ameonyesha Ushupavu na ujasiri katika kuliongoza Taifa letu, ametupatia matumaini ya kesho iliyo Bora Zaidi ya leo

Watanzania Tuendelee kumuunga mkono mh Rais wetu, Tuendelee kumwombea Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia, Tuendelee kuwa naye bega kwa bega, Tuendelee kumpa faraja na kumtia moyo mama yetu, Tuendelee kusimama Naye katika Hatua zote za ujenzi wa Taifa letu , Tuendelee kumpa ushirikiano na kuonyesha upendo kwake Kama anavyoonesha kwetu watanzania.

Watanzania Tutambue na kufahamu kuwa viongozi aina ya Rais Samia Hawazaliwi kila Siku na hawapatikani kila mahali, Viongozi Wa aina yake wenye upendo,uzalendo kwa nchi zao huwa Ni nadra sana Sana kuwapata. Watanzania Tumepata bahati ya kumpata Mama Samia. Ambaye ameonyesha ujasiri, uzalendo,ushupavu na umahili katika kuliongoza Taifa hili, Amelibeba Taifa hili kwa moyo wake wote katika mabega take kuhakikisha kuwa analifikisha salama na mbele zaidi kimaendeleo mahali ambapo kila mtanzania ataguswa kiuchumi nakuondoka katika umaskini wa kipato.

Kazi iendeleee,mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627
Chawa bin kiroboto
 
Hivi kule kwenu Mbozi mmeacha biashara ya kuchunana ngozi za binadamu?
Mbozi kwa Sasa ni salama na matukio ya namna hiyo hayapo kabisa, wanambozi wapo bize na kilimo Cha mahindi kahawa maharage karanga alizeti kilimo Cha mbogamboga n.k. karibu Sana Mbozi wilaya yenye ardhi nzuri na inayokubali mazao karibu yote na yenye watu wakalimu upendo na ushirikiano,hatuna ubaguzi kwa wageni
 
Back
Top Bottom