Rais Samia ni dereva hodari, shupavu jasiri na mahiri wa taifa letu, Watanzania waridhishwa na kasi yake

Rais Samia ni dereva hodari, shupavu jasiri na mahiri wa taifa letu, Watanzania waridhishwa na kasi yake

Nchi hii ina vijana wa hovyo sana, miaka 60 sasa ya uhuru watawala ni wale wale hakuna jipya halafu unakuja kunambia mwehu mmoja shupavu fyokofyoko.
Kwanza huyo siyo Rais wa nchi hii, ni Rais wa kwenye makaratasi tu...
 
Wanamatumaini ya kesho yao kuwa njema kwa kuwa wanatambua mikakati ya serikali yao kuwainua kiuchumi kupitia kilimo na kauli mbiu ya kilimo Ni biashara,ambapo kwa Sasa kilimo Ni biashara inayolipa na inayotoa matumaini kwa wakulima wengi kujikwamua kiuchumi
Hawa wakulima kwenye picha hawako kama watu wenye matumaini wala kutambua mikakati ya aina yoyote ile ila wanaonekana kukata tamaa hawana furaha hata kidogo.
 
Mamilioni ya watanzania wameridhishwa na Kasi ya kiutendaji ya mh Rais katika kupiga hatua za kimaendeleo kwa Taifa letu, watanzania wameridhishwa na mikakati ya mh Rais katika kukabiliana na changamoto zinazojitokeza mbele yetu, watanzania wameridhishwa na dhamira njema ya mh Rais katika kuijenga nchi yetu na kuipeleka mbele kimaendeleo
Mamilioni ya watanzania wapi wameridhishwa, unataka kunambia wale wanaolipwa mlungula waandamane kumpongeza ndo wameridhishwa au?.
Kwanza ameingia na laana tu kwenye hii nafasi ya mchongo...njaa, ukame, vimeandama watanzania km wako kuzimu..
 
Watu wanakwenda kwenye mikutano ya mh Rais kwa hiyari yao wenyewe kwa kutambua kazi kubwa na yakutukuka inayofanywa na mh Rais wetu katika kututumikia watanzania
 
Kuteuliwa kufanya nini
Kuwa chawa mkuu wa mama rasmi.
Maana mpaka dakika hii umejitwika uchawa usiokuwa na maslahi yeyote kwa matumaini utaonekana.

Huna tofauti na mtu anae bet ila kwa dalili zilizopo odds zote ziko dhidi yako maana unasifia mpaka unaemsifia anajua kabisa kuwa hapa napigwa.
 
Watu wanakwenda kwenye mikutano ya mh Rais kwa hiyari yao wenyewe kwa kutambua kazi kubwa na yakutukuka inayofanywa na mh Rais wetu katika kututumikia watanzania
Kaaa kimya, nashangaa hata TAKUKURU wamo humu lkn km vile hawaoni kinachoendelea.
Wanachi wanaenda kushangaa mz*m* unaosababisha laana na mikosi kwenye nchi yao
 
Kaaa kimya, nashangaa hata TAKUKURU wamo humu lkn km vile hawaoni kinachoendelea.
Wanachi wanaenda kushangaa mz*m* unaosababisha laana na mikosi kwenye nchi yao
Watanzania wanaonesha namna wanavyompenda kumkubali na kumuunga mkono Rais wao
 
Rais Samia kaonyesha ushupavu mkubwa Sana katika kukabiliana na changamoto. Alionyesha ushupavu kipindi Cha mfumuko wa Bei ya mafuta nabolea kwa kutoa Ruzuku ya billion Mia moja kila mwezi katika mafuta na billion Mia moja hamsini katika mbolea na hivyo kupelekea kushuka kwa Bei sokoni.
Uharo mtupu ulioandika,amekabiliana na changamoto zipi!!!! Mchele kutoka 1800 mpaka 2800 kwa kilo,sauti za majenereta kila sehemu umeme hakuna,hiyo ruzuku imesaidia nini kama kila kitu kimepanda bei.Acha kusifia ujinga ili upate uteuzi wakati watanzania wenzio wanaumia hizo ni roho za kiibilisi.huyo mama hakufaa kuongoza hata kwa masaa matatu yajayo .
 
Kwamba Ruzuku ya billion Mia moja hamsini katika mbolea hujaona faida take? Kwamba hufahamu kuwa imesaidia kushuka kwa Bei? Kwamba hujuwi kuwa mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu baada ya kutolewa Ruzuku? Au wewe siyo mtanzania? Au huelewi chochote kile kuhusu kilimo? Au hata jembe hufahamu linafananeje? Au hata mvua yenyewe ukiiona unaikimbia Kama kuku?
 
Kilimo Ni biashara mkuu,hata wewe unaweza kulim tu maana Tanzania tumebalikiwa kuwa na ardhi tele yenye rutuba na kusitawisha kila zao

Ndio shida yenu machawa wageni, hamna kitu mnakijua zaidi ya kuweka namba za simu na kuimba mapambio tu
 
Kwamba Ruzuku ya billion Mia moja hamsini katika mbolea hujaona faida take? Kwamba hufahamu kuwa imesaidia kushuka kwa Bei? Kwamba hujuwi kuwa mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu baada ya kutolewa Ruzuku? Au wewe siyo mtanzania? Au huelewi chochote kile kuhusu kilimo? Au hata jembe hufahamu linafananeje? Au hata mvua yenyewe ukiiona unaikimbia Kama kuku?
Ruzuku ya mbolea kwa kilimo kipi?, watu wanalima kwenye ukame.
Acha kuwa na ubishi usiokuwa na maana, kwanza watu wanakula mbolea?. Hivi wanyakyusa kumbe wapo wendawazimu km ww eeh?, ila hapana, wanyakyusa ni watu smart sana.
 
Nawe Mayalla msomi unaunga mkono upumbavu! Mmelogwa nini! Takataka zote hizi!
Ana usomi gani huyo naye mbona unampa sifa asiyostahili,hao ni vijana wa ovyo wa bongo daslam wenye tamaa za kifisi ambao wanakamatia kila fursa inayokuja mbele yao,uhandishi wa habari,uwakili,uanasheria,udalali,uchawa,ukuadi,wizi ilimradi mkono uende kinywani .ogopa sana watu wa namna hiyo na kwa jinsi kulivyo na urasimu katika nchi yetu ndio watu wa namna hii wamejaa huko juu eti wanatuongoza na matokeo yake ni nchi iko katika umasikini wa kutisha hadi leo hii.
 
Ruzuku ya mbolea kwa kilimo kipi?, watu wanalima kwenye ukame.
Acha kuwa na ubishi usiokuwa na maana, kwanza watu wanakula mbolea?. Hivi wanyakyusa kumbe wapo wendawazimu km ww eeh?, ila hapana, wanyakyusa ni watu smart sana.
Kwa hiyo unafikiri mvua haitanyesha? Mimi niliko mvua imeshaanza kunyesha na tayari tunaendelea kupanda
 
Back
Top Bottom